Natamani kujiunga na Takukuru

Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
3,197
3,930
Je, ni sifa zipi zinazohitajika?

Labda elimu, umri, umbile nk. nk.
Wakuu naomba nifahamisheni ili kama kuna ku-apply basi nifanye hivyo soon!
 
Kwa nini unataka kujiunga na Takukuru ili tujue pa kuanzia

Lengo kuu ni kutaka kuwa mpiganaji mzuri juu ya vitendo vyote vya rushwa. Lakini pia kufanyakazi bila kuangalia cheo au dhamana aliyonayo mtoa rushwa, kwangu mie sintaogopa wadhifa wa mtu. Na muhimu zaidi lililo nishawishi ni kuona namna gani dhuluma ilivyo nchi hii (mfano ishu ya Kilimanjaro).

Binafsi sintoogopa kuwa mmoja wa wahanga, ni heri nikapoteza kazi kuliko kuogopa kumkamata mla/mtoa rushwa.

Naombeni maelekezo je, nifanyeje ili nijiunge na Takukuru?
 
Ukitaka kujiunga nao nenda wizara ya mambo ya ndani. Wasiliana na mkurugenzi wa mambo ya TAKUKURU. Au tuma barua pepe kwenda ps@moha.go.tz. Atakupa maelezo yote jinsi ya kufanya. Ukikosa kabisa msaada ni PM.
 
Kijana upiganaji ndani ya nchi hii (TZ) una-limits zake, hivo sikushauri ubebe unnecessary risky...........working environment sio favourable. Mkuu wa takukuru mwenyewe Hosea anamtetemekea Rais ( Ambaye ni Mgombea wa Urais), usije ukategemea hata siku moja maofisa walioko chini yake watafanya kazi kwa uhuru na kwa kufuata misingi ya kazi ( working guidelines while observing professionalism and due diligence).
Ukienda mbali zaidi utagundua ya kwamba Takukuru wanafanya kazi kwa uwazi sana ukifananisha na Tanzania secret services, hii ni hatari kubwa kwa usalama wa muhusika hasa ukizingatia nature ya kazi za Takukuru ni sawa sawa na za usalama wa taifa. Sasa unamu-expose huyu then huyu unamuambia tumia approach ya kujifichaficha.

Hitimisho: Sina maana ya kukuogopesha lakini ukweli ndo huo, Sikushauri ukimbilie moto :)A S-fire1:). Maamuzi ni yako mwisho wa siku

"Think outside the Box"
 
We nenda tu wengine yalitushinda huko. Kama kweli una nia ya kulifanyia kazi taifa....utakuwa na kibarua kigumu na
usipoangalia wenzio watakubambikia kesi ya ula rushwa au utapoteza maisha...or else utaungana nao na kuwa kiongozi wa kupokea rushwa.
TAKUKURU ni TAKATAKA. Period!
 
Wakuu asanteni sana kwa ushauri na maoni yenu, nitakaa na kutafakari kabla ya kuchukua hatua.

Nawashukuruni wote na nina yaheshimu maoni/ushauri wenu, na hasa:
  • Tzpride,
  • Payuka,
  • Pape - baada ya kutafakari kwa kina nita ku-PM
  • Mkeshahoi- cku zote mabadiliko yanaletwa na wachache na hasa wale wanao amua kuji sacrifice. Asante ila bado natafakari!
  • Bujibuji- naimani siyo wote ila wapo kweli wala rushwa wakubwa huko Takukuru, na waaminifu pia wapo.
  • FirstLady1- mbona hukurudi tena? nilikuwa nasubiri maoni/ushauri wako baada ya swali ulilo-niuliza.
Asante sana na nina heshimu michango yenu.
 
je, ni sifa zipi zinazohitajika?

Labda elimu, umri, umbile nk. Nk.
Wakuu naomba nifahamisheni ili kama kuna ku-apply basi nifanye hivyo soon!

pole ndugu aiitaji elimu wala nini swala unamjau nani na yuko nafasi gani hilo ndio muhimu ukishaweka sawa hayo tu pemiane tujue pa kuanzia...shule aipo kule wapo darasa la saba nawajua ...na makadi yao feki lakini wanakula kuku kama awana akili nzuri kazi kwako...
 
Back
Top Bottom