Natamani kuionya Young Africans makundi ya CAFCC

MombaDier

Senior Member
Jul 24, 2022
102
205
Natamani kiongozi mmoja amshike bega mtoto pendwa mwana Kalala amwambie kuwa katika mechi hii inahitajika nafasi moja ili kulipata goli moja, natamani amwambie kuwa pindi azam tv na king’amuzi chao bora watakapotoa takwimu za mwisho na tukaona upande wa njano na kijani una on target 3 basi natamani kuona wakiwa wameandika goals 3.

Natamani atokee kiongozi mwingine akamng’ate sikio “The Zanzibar finest” Mwana Salum akimwambia kwamba piga uwezavyo popote utakapokuwa ila kuna mimi ninayetamani kuwa kama atapiga mashuti 4 basi lisitokee hata moja likawa off target.

Natamani kiongozi mmoja kutoka katika kitengo cha kumbukumbu kiwaweke wachezaji chini na kuwakumbusha kuwa Young Africans ni timu kutoka Tanzania ambayo kwa siku za karibuni imekuwa ikicheza mpira mzuri hata ikiwa nje ya Taifa lake. Tukitupilia mbali yale makofi ya pongezi kutoka kwa mashabiki wa Al’hilal pale Omdurman ni timu ambayo ikitokea imefungwa ugenini basi si kwa tofauti ya goli mbili ama zaidi, mbali na matokeo yale waliyoyapata kule Egypt dhidi ya Pyramids wakiwa na mzee wa vipensi Mwinyi Zahera. Natamani wawathibitishie hili kwa kuwaonesha matokeo dhidi ya Zesco United, Rivers United, Township Rollers na hata yale ya juzi dhidi ya Al’hilal.

Natamani wasiishie hapo, waendelee kuwaambia kuwa licha ya kuwa Club African ni timu kubwa yenye historia nzuri ndani na nje ya nchi yao, lakini pia wanatoka katika ligi ambayo iko nafasi ya 4 kwa ubora barani Afrika kwa points zao 113 ambapo mbali na ukweli kuwa ligi tuliyopo imekuwa ikiimarika kila siku lakini ndiyo kwanza ipo nafasi ya 11 kwa points 30.5, hivyo wawakumbushe kuwa ni muhimu kiasi gani kumaliza mechi mapema palepale kwa Mkapa kabla ya kwenda kwao.

Natamani yule Profesa wa kitunisia ajue kuwa licha ya kuwa hawa ni ndugu zake kweli lakini wanapokuwa kwao undugu huweka pembeni hivyo basi aachane na Habari za kuwajua ama kuijua nchi ya Tunisia na badala yake awakumbushe namna ya kuwaheshimu wapinzani hao na kuwaambia defensive line ni muhimu kiasi gani kuwazuia wasipate goli lolote kabla ya kwenda kushikilia bomba kule kwao.

Mwisho wa siku natamani atokee mtanzania mmoja afikishe ujumbe huu kwa viongozi na wachezaji wa Yanga, awaambie kuwa natamani kuliona vibe la WANANCHI katika hatua za makundi ya CAFCC.

DAIMA MBELE NYUMA MWIKO.
 
Shida yenu moja tu, huwa mnahisi timu zingine hazina uwezo kabisa wa kufanya chochote unavyosema utafikir timu hii ni zalan , sikia wewe utopolo kushinda mnaweza kushinda au kufungwa pia,

Kumbuka mashindano haya timu nyingi ni Bora sana na zinamakocha Wana mbinu kweli kweli

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Mtatamani sana Mkuu ila ndo... Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.
 
Yes mtaingia kwenye yale makundi yenu rasmi ya manyani na mambwa wa kubweka bweka hovyo
 
Back
Top Bottom