Natamani iandikwe katiba ya Muungano na United States Of America!

Weakman

JF-Expert Member
Jul 23, 2021
861
1,384
Nawasalimu!

Nimekuwa nikiwaza Sana! Sometimes inauma Sana unapowaza Jambo ambalo haliwezi kutokea. Naam, si rahisi kuwa na Muungano na USA. Lakini, je, ni kweli haiwezekani? yes haiwezekani kabisa! Hapa shida si Raia wa kawaida wa Tanzania, bali wanasiasa waliowekeza maisha yao ktk siasa. Yaani wapoteze ulaji wao Tena, ohooo!

Ni kweli Kama Taifa haiwezekani kuungana na USA? Inawezekana Sana, Ni ishu ya kukubaliana Kama Taifa kuwa tunataka Tanzania liwe Jimbo la USA, Rais wa USA awe Rais wetu. Tanzania iwe na Gavana, aisee maisha yangekuwa bambam. Tanzania ingetoboa asubuhi mapema!
Maendeleo, uchumi, siasa, usalama vingebalika na kukua kwa speed ya light!

Tunalia juu ya Elimu, ajira, umeme, sgr, kilimo, ufisadi, afya, mishahara waalimu n.k yote yangekwisha ndani ya siku moja. Ninaamini kabisa, ukipeleka kura ya maoni kwa Watanzania, ya kusudio la kuungana na USA, asilimia 80 au zaidi wataunga mkono.

Leo tumezaliwa tunaishi maisha hovyo Hadi tunakufa. Watoto na wajukuu watakuta maisha hovyo na watakufa
Kumbe tungeungana na USA, ustawi ungetufikia mapema na maisha ya hovyo yangeondoka

Mimi ninaamini tumezaliwa for life not for Tanzania, kwa hio Tanzania iwe for benefit of our lives!

Wengi wanaamini idea Kama Hii Ni kutweza utu. Unautwezaje utu wakati unaufanya uwe Bora zaidi? Mtanzania anayeishi Marekani ameutwezaje utu wake? Mtanzania anayeishi Michigan si mjinga mjinga Kama anayeishi Tabora au Mwanza! Jambo Ni lilelile, badala ya Watanzania wote kwenda kuishi Florida Marekani, tunaamua kubadili Tanzania kuwa sehemu ya Marekani!

Ukweli Ni kwamba ndoto ya kuistawisha Tanzania Ni ya Safari ndefu. Na naumia kuwa, haiwezekani pia kufanya Tanzania kuwa part of USA!
 
Kuungana sio rahisi sisi hapa Tanzania hatujaungana yaani sisi wabara tu na mikoa yetu bado tuna rivalry wenyewe kwa wenyewe kikanda na mikoa ...Bado hatuna mahusiano mazuri na Zenji.


Hao USA kuna lugha kibao ila ni watu ambao wanajivunia kuwa wamoja sio kama sisi ujuaji mwingi na upendeleo ..

kila mtu anajikuta yupo juu kutokana na sehemu aliyotoka ...Ukipata nafasi kula na familia acha kutetea wabinafsi.
 
Marekani Tena, Marekani ikisema inatafuta wanaume wa kuwaowa humu naona kuna watu watakuwa tayari. Zingatia neno kuwaowa
 
Marekani Tena, Marekani ikisema inatafuta wanaume wa kuwaowa humu naona kuna watu watakuwa tayari. Zingatia neno kuwaowa
Yah, watapatikana!
Si humu tu every where in the world wanaume wa kuolewa wapo
Ukumbuke kwamba wamarekani wanaweza kuwaoa Watanzania na Watanzania wanaweza kuwaoa wamarekani
Kuoa ama kuolewa Ni Jambo la muingiliano, halina direction moja!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom