Parabora
JF-Expert Member
- Jul 6, 2019
- 1,504
- 2,180
Wakuu nina Kibiashara changu hapo mjini dar kinachonipatia ridhiki, lakini kwa mda mrefu nimekuwa nikitafiti sehemu za kupata eneo kubwa la kuweza kufanya shughuli zangu kiupana zaidi na hapa Dar ibaki tu kama mmojawapo ya sehemu ya hivi vibiashara vyangu, nimebase katika biashara za mazao karibia yote ya nafaka na mifugo pamoja na samaki ambapo nauza jumla na rejareja, kwenye mifugo hapa nauza walio hai na pia nachinja nauza nyama kwa wenye mabucha na zinazobaki nasambaza kwenye Meat House zangu mwenyewe na kwa vile Mimi sipo huko nchini lakini biashara bado zinaendelea vizuri.
Nilikuwa nafikiria nipate eneo kubwa kwenye mikoa ambayo ni rafiki na hizi biashara zangu maeneo ambayo yamechangamka kibiashara yatakayoniwezesha kufungua vituo vingine vya biashara za aina hii pia niwe nakukusanya malighafi kirahisi na kuzituma Dar zichakatwe ziingizwe sokoni kama bidhaa tayari kwa kuuzwa.., maeneo ambayo nitahitaji kwa ajili ya kujenga miundombinu yangu ya ufugaji atleast yawe 15km kutoka center ya mji husika na pawe na umeme na usalama wa kutosha na shamba lenye ukubwa usiopungua heka 20 mpaka 30
Miji na sehemu ninazofikiria
1. Morogoro
2.Singida (Iguguno)
3.Geita (Katoro)
4. Shinyanga (Kahama)
Sina uzoefu wa kutembelea maeneo yote haya japo si sana kulingana na mda wangu kunitinga huku ng'ambo kwa waliopo maeneo haya naombeni tuwasiliane ikiwemo kunipa ushauri wa sehemu ambayo nitapata maeneo mazuri yatakayonifaa kwa ajili ya shughuli zangu.
Ahsanteni