Natafuta wadau ama wawekezaji katika uzalishaji wa biodiesel

jchris

Senior Member
Aug 6, 2013
125
40
Biodiesel ni mafuta yatokanayo na mimea kama karanga,mawese,alizeti na mengineyo,yanayofanya kazi kwenye vyombo vya moto vyenye kutumia engine za diesel kama magari na majenereta.

Nimefanya mafunzo katika hii fanii na kusoma makala mbali mbali mtandaoni ikiwa ni pamoja na kuangalia videos za wenzetu walioendelea wanaotumia technology hii ya uzalishaji wa mafuta mbaadala ya diesel ya kawaida tuliyoizoea.

Nimeshaandika mchanganuo wa biashara upo tayari, ikiwa ni pamoja ma faida itakayopatikana na uzalishaji wa mafuta haya mfano ni uzalishaji wa sabuni pia utatokana na huu mradi ntatoa apo baadae maelezo zaidi,zile zinazotumika kwenye laundary cleaning na za vipande vya kawaida vya sabuni za matumizi ya kawaida.

Ni mambo mengi yaa kuandika lakini ntaandika kwa uchache kutokana na kutumia simu. Niliichokwama ni kupata mtaji wa kuuanzisha huu mradi ndoo nimekuja apa tujadiliane kaa tunaweza kupata wadau tuweze kuanzisha huu mradi utakao tupunguzia utegemezi wa mafuta machafu toka njee kwa maelezo zaidi unaweza kuuliza.

Note:nitatumia malighafi za mafuta ya mimea machafu kutoka majumbani ,hotelini,restaurant na yale mafuta yaliyokataliwa wakati wa kusafisha katika viwanda vya uzalishaji wa mafuta katika viwanda vya uzalishaji mafuta ya kupikia yatokanayo na mimea.

Endapo atajitokeza mwekezaji tutafanya naye usajiri wa biashara na taratibu zote kufwata tutakuwa pamoja ili kuweza kupata vibali vya uuzaji wa aina hii ya mafuta. Nimeandika hii ni summary wadau karibuni kwa kuanza ni vema tuanze polepole kwa mtaji wa 3milion only natanguliza shukurani.

Kwa mimi ntachangia eneo la kuweza kujenga au kuuweka huu mradi ni ra ndugu yangu na alinikubali ombi liko maeneo ya bunju ili kupunguza gharama ya kodi ya pango.

Nipo Dar es salaam Bunju
 
Mradi huo uanze kwa mtaji wa 3Milion?? Are you jocking? Embu fafanua how?
 
Yes inawezekana kutokana na vitu unavyoweza kuanza navyo kikubwa ni mtambo unaoitwa boidesel processor,chemical used methanol,saodium hyroxide na iso pro-ply na ma containers au mapipa ayo ndoo ya muhimu sana
 
Am not joking nimefanya uchunguzi kwa muda kaka adi kuna kuandika haya
 
Yes inawezekana kutokana na vitu unavyoweza kuanza navyo kikubwa ni mtambo unaoitwa boidesel processor,chemical used methanol,saodium hyroxide na iso pro-ply na ma containers au mapipa ayo ndoo ya muhimu sana

Vyote hivyo vi cost 3M?? Comeon be serious go back to the drawing board.
 
Naona hujanielewa nisema tuanze kidogo kidogo ukiipanua ni project kubwa sana mkuu naona umelenga labda plant kubwa
 
Yec@crocodile ngumu kidogo ni hiyoo methanol kutokana na nature yake
 
nimefanya tafiti ya biodiesel na nimezalisha pia kwa level ya maaabara, naijua vizuri sana. Na kwetu Moshi.nimepanda mmea wa JATROPHA ili kuweka hiyo kumbukumbu.

Swali: Najua kwa 3m unaweza kuzalisha, swali langu ni kwambaa unataka kuzalisha kiasi gani? Utayatumia kwa matumiz gani? Kuhusu wateja umefanya pia tafiti?

Kwa ujumla nishati hiyo inagharama kubwa sana ukitaka kufanya large scale
 
Congrats nyingi kwa kupamba na hasa ktk sekta ya nishati kama hii naamini its doable b'ness.
Kama wengine walivyo na mashaka na kiasi cha mtaji wa kuanzia na mimi hivyo hivyo.
Swali: unadhani kwa mtaji wa 3m unaweza zalisha lita ngapi, na kama alivyouliza Zaidige, unalijua soko?
 
Mimi pia nimependa hili wazo ila naomba unielemishe zaidi je uzalishaji wa hii kitu hauongezi gesi joto angani (CO[SUB]2[/SUB]). Pili huo mtaji mbona kama mdogo sana?! Kama una hakika na huo mtaji ningependa kuona hiyo plan yako tafadhali.
 
Unaongeza kwa kiwango kidogo sana maelezo yote yapo kwenye plan
Hiyo hela nimeweka kama minimum capital lakini unaweza kuwekeza zaidi ya hapo lakini ni vyema tuanze kidogo kidogo maana ni kitu kigen apa kwetu lakini kwa zilizoendelea wanatumia hii product mdadala ya diesel ya kawaida
 
Maelezo yapo kwenye plan kama umependezwa nayo yunaweza kukutana tuongee
Ntaeleza kwa kifupi vitu muhimu kuwa navyo
1.waste vegetables oil or oil rejected befor refining(vegetables oil)
3.Methanol second main componet it as a base
Sodium hydorixed or potassium hydroxide this act as cataylst during mixing of waste vegetables oil and methanol
4.titration apparatus maana lazima ufanye titration kabla ya kuamua kuyafanyia kazi ayo mafuta kufahamu kiwango cha fatty acid kilichopo ndan ya mafuta,hii inakusaidia kujua utatumia catalyst na methanol kiasi gan .apo kuna mahesabu kidogo
4.biodiesel processer huu ndoo mtambo wenyewe wa kuyapata ayo mafuta
Ukiwa navyo ivo zinatosha kuanza uzalishaji samahan kuna sehemu sijatumia kiswahili ilikuwa ngumu kidogo
 
Naona hujanielewa nisema tuanze kidogo kidogo ukiipanua ni project kubwa sana mkuu naona umelenga labda plant kubwa

Mkuu kitu cha kwanza - sina shaka unajua athali za ku-tinker around na METHANOL!!! Pili, changa moto za ku- transesterificate mafuta ya kupikia/kula especially yaliyo kwisha tumika mahotelini au wapika chips yatakugharimu sana especially wingi wa chemicals zinazohitajika kuchanganywa kwenye mafuta machafu ili yaweze kukidhi kiwango cha kuweza kutengeneza methyl esters (BioDiesel) yakichanganywa na Methanol, ukisha fanikisha zoezi hilo je lita moja ya Biodiesel utahuza kwa bei gani, ukiwekea maanani gharama za malighafi i.e ukusanyaji wake kutoka mahotelini nk,Chemicals na overheads nyingine!!

Ukisema labda utumie mafuta ambayo hajatumika utakuta lita moja ya mafuta ya kula inauzwa Tsh.4,000/= (ghali kuliko lita moja ya petrol) je utatumia lita ngapi za mafuta ya kula ili u-sythesize lita moja ya BioDiesel na uta i-sell kwa bei gani? Hayo ni maoni yangu tu na hapa nimezungumzia changamoto chache, sina nia ya kukukatisha tamaa.
 
Back
Top Bottom