Natafuta soko la vanilla mbichi na kavu popote litakapopatikana

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,605
2,729
Narudi tena kwenu wanajamvi kutaka kupata connection ya SOKO LA VANNILLA mbichi na kavu.

Kagera tuna kilio kikubwa VANILLA imekosa wanunuzi wakulima wanapoteza matumaini kabisa mwaka huu ikumbukwe ata mwaka jana VANILLA ilishuka toka Tsh.70, 000/@1kg hadi Tsh.30, 000/@1kg hali hii ilitokana na serikali kuzuia wanunuzi kutika Uganda kuja kununua VANILLA ya Wakulima wa Tanzania(Kagera)

Sasa baada ya kutafakari na kuona kilio cha wakulima najinsi wanavyovuna na kuirundika ndani uku waliowengi kutokuwa na elimu ya ukaushaji na utunzaji kwa ujumla nimeona binafsi nipitie jukwaa hili nieashirikishe fursa hii muhimu na hadhimu kutafuta soko la VANILLA tena la kudumu.

VANILLA inapatikana kwa wingi bei ni kuanzia T.sh 30, 000/@1kg kushuka chini hii ni VANILLA mbichi.
VANILLA KAVU GRADE ONE =T.sh 350, 000@1kgm kwa yeyote mwenye uhitaji awasiliane nasi kupitia simu No.+255 622 573 467 lengo ni kumsaidia mkulima wa Kagera wilaya zote za Kagera wana kilio hichi.

Tafadhali fikisha taarifa hii kwenye makundi ya WhatsApp, Telegram, Twitter na kwingineko.
Mwisho niwaombe team nzima ya Jf kuweka sawa andiko ili na kulisambaza nisikoweza kufika.

Email-mujunkatikabakama@gmail.comView attachment 2686326View attachment 2686327

IMG-20230712-WA0090.jpg
 
Wamezuia waganda wasinunue vanilla Tanzania ila DP W. waje wakae bandarini 😃😃
 
Matangazo ya hiki kilimo kama ungeyasikia kipindi kile hakuna ambaye angetamani kuwa mkulima anyway tutadikisha ujumbe
 
Wamezuia waganda wasinunie vanilla Tanzania ila DP W. waje wakae bandarini
Unazuia Waganda wakati hauna soko mbadara, mimi ujiuliza Waganda uuza soko lipi la dunia ambako Tanzania hatuwezikufika? Walizuia Kahawa isiuzwe kwa Waganda leo wanazuia Vanilla wanataka tulime nini? Dawa yao ni kuhakikisha hatokei mbunge wa Ccm Kagera.
 
Baba Levo alisema bei ya kilo moja Vanilla ni Milioni, hebu mtafute upige hela.
 
Unazuiaje mganda kununua vanilla ambayo wewe hauwezi kutoa bei nzuri kama sio ujinga ni nini
 
Back
Top Bottom