Natafuta nafasi ya kazi au internship

Cies

Member
May 26, 2019
12
13
Habari Watanzania wenzangu!

Wakubwa Poleni na majukumu, kijana wenu nimekuja kupitia forum hii kujaribu kutafuta fursa ya kazi au intern ambayo itanisaidia angalau nisikae vijiweni na kuzurura mtaani!

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 25, nimehitimu Shahada ya Uchumi mwaka 2021, naishi Dar es Salaam, nimejaribu sana kuomba kazi bila mafanikio, nimefanya process zote za Taesa hadi interview huu ni mwezi wa 5 bila kupigiwa simu, nimesambaza sana CV bila mafanikio mpaka inafika muda nakosa matumaini, ukizingatia hali ya uchumi wa familia si shwari kiasi kupata mtaji changamoto.

Natanguliza shukrani kwa wote watakaoguswa na Mungu awabariki!

Napatikana kwa namba hii 0716306180.

NB: Nipo tayari kufanya kazi nyingine yoyote iliyo halali.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA!
 
Pole mkuu ila usikate tamaa soon tu utalamba asali
 
Kila la heri Mkuu, ila kwa taaluma yako ya uchumi vipi kwa hali ya uchumi ya sasa unadhani patakuwepo na nafasi za ajira sekta binafsi na serikali pia Mkuu?.

Kama ndio unadhani watakaokuwa na uwezo wa kuajiri wamefanya nini ili kuendana na hali ya uchumi wa sasa?.

Mwisho kabisa unashauri wazalisha ajira wafanye nini ili waweze kuajiri wafanyakazi kwa kuzingatia hali ya uchumi wa sasa?.

Sikukatishi tamaa ila najaribu tu kuona namna unaweza kuitumia elimu ya uchumi uliyonayo Mkuu.
 
Kiuhalisia swala la Ajira bado ni changamoto kwa nchi, tunashauriwa tujiajiri ni good point but mtaji unautolea wapi? ukitazama wazazi wameuza karibia assets zote ili uweze kusoma, ukitaka kwenda kukopa bank au kausha damu dhamana ya mkopo changamoto!

Sisi kama graduates tunajitahidi sana kupambana pale tunapotoka chuo wengi wetu hatupendi kukaa vijiweni wala kumlaumu mtu au mifumo iliyopo lakini tunajikuta tunakwamishwa na vitu vingi sana ambavyo mwisho wa siku vinatufanya tukate tamaa.
 
Kweli chief, nini kifanyike sasa?

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Kwa mtazamo wangu, cha kwanza mfumo wa elimu wa sasa hauendani na mfumo wa maisha uliopo sababu ni "theory based" na hauwezeshi kupata skills ambazo zinaweza kuendana na mahitaji ya soko la ajira kwasasa.

Kwa upande mwingine suala la "Nepotism" limekithiri sana, imefika hatua hata kupata sehemu ya kwenda kufanya practical field ni mpaka uwe na "Connection", hata kuomba kujitolea mpaka uwe na "Connection" Je sisi watoto wa wakulima kutoka mwakamwasule ambao hatuna wajomba au shangazi kwenye vitengo tutaweza kweli kutoboa? niliwahi kufanya interview ambayo tayari watu walishaanza kazi muda mrefu, interview ilifanyika kuonekana protocal imefuatwa, fikiria mtu unatumia fedha kiasi gani kufika kwenye interview (nauli, malazi, chakula).

Kuwe na mazingira wezeshi kwa graduates kama kuwezeshwa ya kujiajiri kama ambavyo wanavyotuambia kuwa tujiajiri, niliwahi kufungua kilinge cha kuchoma mahindi sehemu ushuru yaani ndio usiseme bado sijasumbuliwa na wagambo mara wanikamate wanipeleke kwa mtendaji na ukienda kule hakuna cha maana zaidi wanataka "ya maji" Je kwa style hii sisi watoto wa wakulima tutatoboa?
 
Daaah, one day yes mkuu tu push tu.

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Kiuhalisia swala la Ajira bado ni changamoto kwa nchi, tunashauriwa tujiajiri ni good point but mtaji unautolea wapi? ukitazama wazazi wameuza karibia assets zote ili uweze kusoma, ukitaka kwenda kukopa bank au kausha damu dhamana ya mkopo changamoto!

Sisi kama graduates tunajitahidi sana kupambana pale tunapotoka chuo wengi wetu hatupendi kukaa vijiweni wala kumlaumu mtu au mifumo iliyopo lakini tunajikuta tunakwamishwa na vitu vingi sana ambavyo mwisho wa siku vinatufanya tukate tamaa.
Sawa Mkuu, ila swali langu haujalijibu kabisa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom