Natafuta kazi zinazohitaji mahesabu, kuandika au kutumia kompyuta

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
4,425
9,823
Habari zenu wote? ni matumaini yangu wote ni wazima. Naomba niende moja kwa moja kwenye dhumuni kuu
Mimi kijana wa kiume umri miaka 30, mwenyeji wa Dar es salaam ila kwa sasa nimeamishia makazi mkoani Iringa kujaribu maisha na huku baada ya kufanya ivyo nikiwa Dar kwa muda mrefu sana bila mafanikio wala matumaini yoyote, hapa Iringa nimepewa hifadhi na dada angu ambae nae ni mpambanaji kama mimi sio mambo safi

Lengo kuu la andiko hili ni kutafuta ajira, elimu yangu nimesoma bachelor degree in business management, nimesoma diploma in procurement and logistic management pia nina ujuzi wa mambo ya accounting, finance na banking maana nilifanya field CRDB BANK, nimehitimu bachelor degree mwaka 2016 tangu kipindi hicho sijawahi kupata ajira rasmi, kwa yoyote atakae niwezesha kupata nafasi kulingana na nilichosomea, proffesional field yoyote ambayo inafundishika (nina elewa mambo kwa urahisi na haraka sana) au kazi yoyote ambayo halali nitashukuru sana.

Najua wengi wanaweza kubeza kwa kusema mvivu, mzembe, jiajiri n.k lakini tujaribu kuelewa maisha hayapo poa kwa kila mtu muda mwingine unaweza kuwa na elimu nzuri, afya nzuri, upo vizuri kichwani, mpambanaji lakini bado maisha yakakupiga

Historia yangu kwa kifupi, shule ya msingi nimesoma mkoani Iringa nikafaulu vizuri darasa la 7 na kupangiwa kwenda Azania Secondary School mkoani Dar es salaam, nilivyofika form 3 mwanzoni tu nilipatwa na tatizo la masikio kushindwa kusikia vizuri, baada ya hapo nikawa nasoma notes tu maana kumsikia mwalimu ubaoni ni shughuli pevu, baada ya kumaliza form 4 nilisoma certificate na diploma ya procurement and logistic management na nikajiendeleza bachelor degree of business management, tatizo la kusikia bado linanikabili mpaka leo, nashindwa kumsikia mtu akiongea akiwa mbali, nashindwa kumsikia mtu akiongea kwa sauti ya chini sana, namwelewa kwa shida mtu mwenye kigugumizi na nashindwa kumsikia mtu kwa kuongea nae kwenye simu ila mtu ambaye yupo karibu yaani ile face to face tunaelewana vizuri tu, nishaenda hospitali kadhaa bila mafanikio mara ya mwisho miaka kama mitatu iliyopita nilipata msaada wa jirani yetu kipindi nikiwa Dar es salaam alijitolea kunisaidia gharama za matibabu hospitali ya CCBRT lakini ilishindikana kutibika tatizo langu licha ya kuingia gharama kubwa, nikasema ngoja nikubaliane tu hali halisi nikachagua kuishi ivyo ivyo maana nishaangaika sana na hospitali acha nikubali tu ndo mtihani wangu huo hapa duniani ki ukweli ni tatizo ambalo limenigharimu sana nashindwa kuchangamana na watu ambao sijuani nao, hata kwenye interview nashindwa kusikia vizuri nilichoulizwa sometimes napigiwa simu kuitwa kwenye interview ni shida kuelewana ikabidi nijaze namba za ndugu yangu kwenye C.V incase akipigiwa ananitaarifu ila bahati mbaya waajiri wanachukulia kama sipo serious nafanya ujanja janja fulani kwaiyo nikiwaambia hali halisi kupitia ujumbe wa maneno wanajibu tu "sawa asante" na mchakato unakua umeishia hapo.

Naomba sana msaada wenu wana ndugu kazi zinazohitaji mahesabu, kuandika au kutumia kompyuta naweza kuzifanya bila shida yoyote kwa sababu najua kuandika vizuri lugha za kingereza na kiswahili, nina ujuzi wa kompyuta pia nipo vizuri sana kwenye hesabu. Pia kazi ambayo inahitaji nguvu mfano kupanga bidhaa kiwandani au store naweza kufanya pia. Nipo tayari kufanya kazi mkoa wowote, kwa msamalia mwema aliopo Iringa mjini kama akihitaji kujiridhisha na uwezo wangu kitaaluma nipo tayari kufanyiwa majiribio
Asanteni sana kwa kusoma andiko langu
 
Wakati vijana wenzako At the age of 30 wanatafuta kazi yeyote ile wewe at the Age of 30 bado tuu unachagua kazi za kufanya alafu kula na kulala unamtemea sister ambaye ni mishen town mjini iringa amepanga chumba kimoja unakaa kwake .....
 
Wakati vijana wenzako At the age of 30 wanatafuta kazi yeyote ile wewe at the Age of 30 bado tuu unachagua kazi za kufanya alafu kula na kulala unamtemea sister ambaye ni mishen town mjini iringa amepanga chumba kimoja unakaa kwake .....
Don't judge others. You don't know What they have been through. We need to support each other
 
Wakati vijana wenzako At the age of 30 wanatafuta kazi yeyote ile wewe at the Age of 30 bado tuu unachagua kazi za kufanya alafu kula na kulala unamtemea sister ambaye ni mishen town mjini iringa amepanga chumba kimoja unakaa kwake .....
Mkuu naomba connection au kazi yoyote utakayoona nafaha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom