Natafuta kazi ya udereva

Msorokoto

Member
Aug 23, 2023
21
8
Habari za muda huu?

Nina miaka 19 ni kijana wa kiume nina leseni ya udereva daraja D, nina cheti cha Veta pamoja na cheti cha form four.

Ninaishi mkoa wa Kigoma wilaya ya Kigoma mjini, ninatafuta kazi ya udereva iwe, kwa watu binafsi, mashirika, makampuni, taasisi n.k.

Kwa yeyote mwenye kujua wapi ninapoweza kupata kazi hiyo au mwenye uhitaji wa dereva naomba uniambie tafadhali iwe hapa mkoani Kigoma au hata nje ya mkoa.

Lakini pia kama kuna ushauri unaweza kuniambia. Asanteni!
 
Kwa kigoma udereva andika cv yako then peleka tarura kigoma mjini ofisi zao zipo mitaa ya pefa wanapakana na Tanroad

Au peleka tarura wilaya ya Kasulu

Kwa umri wako nakushauri ongeza fani usome na mechanics angalau mpaka levo 2 itakupa uwanja mpana wa ajira

Udereva bila ufundi nisikudanganye......HAUTOBOI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom