Natafuta housegel

mami kupata house gel ni issue nowa days...
cku hizi kuapata ni kuashawishi kutoka huko wanako fanya kazi kwa kuahidi mishahara mikubwa, malazi na maisha bora kwako..
 
Dah namimi natafuta ila awe amemaliza form 4 mshahara 30000 chakula na malazi kwangu!

Naamini utampata utapa kiongozi!!
 
Mie ninao wawili. Naombeni tangazeni viwango bvya malipo na muda wa kazi. Siyo mnafanyisha watu kazi toka asubuhi hadi asubuhi. Naombeni muhakikishe kuwa wana muda wa kupumzika siku za wiki na jumapili iwe off day kwao. Aliyetayari aweke mambo hadharani. Wote wamemaliza kidato cha 4
 
Elfu 30 ni ndogo sana kwa sasa maana hata pad ziko juu kila kitu kimepanda, kama kweli uko serious ukipata HG mlipe vizuri mpe muda wa kupumzika utaona kazi zinakwenda vizuri labda iwe bahati mbaya upate sikio la kufa, ila mi nina bahati na wasichana wachapa kazi, namshukuru Mungu sana kwa hilo.
 
Mhh jamani nami nimetingwa natafuta saana Mdada/Mkaka wa kazi. Mi nakaa Dar, Majumba sita. Nyumbani kwangu tupo mimi na mke wangu na watoto wawili. Mtoto mmoja ana soma darasa la sita wa kiume na mwingine ni mdogo wa miezi kumi. Mimi na mke wangu twafanya kazi hivyo twatoka asubuhi na kurudi jioni. Hivyo twahitaji mtu wa kukaa nasisi. Atakuwa ni sehemu ya familia yetu. Kulala, Chakula na matibabu ni kwangu. Mshahara ni 40,000/= kwa mwezi. Shule awe amemaliza darasa la saba, akiwa wa form four ni added advantage. Umri asiwe chini ya miaka 18 na sio zaidi ya 30. Kama waweza nisaidia naomba uni-PM
 
jaman nyinyi mbona mnawalipa kdg sana ao mahaus gal?
dah nikija muwa mam mwenye nyumba stakuja kumlipa kaela aka msaidiz wangu wa ndani

ivi ukikaa weknd home na kuamua kupiga kaz zote za nyumban lazima uchoke,....znachosha hasaaaaaaa..

wewe upo job ,kuna vidil vya apa na pale jaman ...mwenzio yupo tu hm hana ata mishe mishe ,mikaz kibao..na wengne ata kula hawali nao mezan wanaenda kula jikon au nje afu wampa efu 30 sjui 40?

jaribun kuwapa kaela kazuri kdg...tuwafikirie wenzetu jaman...we efu 40 ata ukiamua kutoka wknd AITOSH NA MARAFIKI ZAKO...au ata km aujatoka lakin 40 ndg sana.....

muwape fresh waweze kufanya poa kaz zao..
na km mungu amaekubariki na msaidiz wako ana adabu basi si mbaya km ukimsomesha pia km ana mwamko uo...
 
kwa 40,000/= itakua ngumu kupata pandisha dau!

wao hawa wanadai marupurupu ya mishahawa kwa waajiri wao wakati huo huo wanalipa kiduchu kwa wafanyakazi wao. Inatakiwa mshahara na marupurupu iwe kama ifuatavyo:-
1. mshahara wa h.girl ni 85,000/= .
2. Kula bure na kulala bure.
3. Matibabu bure akiugua na pia nauli ya kwenda kwao na kurudi kila mwaka pamoja na zawadi kwa wazazi wake (baba na mama)
4. Pesa zipelekwe benki si kumpa mkononi ashauriwe namna ya kutunza pesa
5. apewe ushauri njisi ya kujisaidia yeye mwenyewe in future lets say after 5 to 10 years
6. Awe ni mmoja wa wanafamilia, (asinyanyaswe kwa namna yoyote ile) hapo ataweza kuwapenda ninyi pia pamoja ya watoto wenu

Haya wengi hawayatimizi na ndiyo tatizo kila siku wafanyakazi wanasepa tu unabaki unahangaika kama hivi.
 
Upo sahihi ndg. Fuso. Kama hayo yatatimizwa maisha majumbani mwao yatakuwa kama peponi. Tatizo bongo wamejaa mizulumati. Eti binti hata akivunja ka glasi ka mchini anakatwa mshahara mara kumi ya bei ya glasi. Sasa hivi wasaidizi wa kazi wameamua kuchuakua sheria mkononi. Akiona kuna dalili zoooooote za kudhulumiwa lazima amfanyie mtoto kitu mabaya ndo anaingia mitini. Matajiri tumwogope Mungu, tuwalipe wasaidizi vizuri na maisha yatakuwa matamu
 
Ukimpa mshahara mdogo anatoka na mwanao wa kiume wanabalance au baba mwenye nyumba akikaa vibaya nae anaingia mtegoni.
 
jaman nyinyi mbona mnawalipa kdg sana ao mahaus gal?
dah nikija muwa mam mwenye nyumba stakuja kumlipa kaela aka msaidiz wangu wa ndani

ivi ukikaa weknd home na kuamua kupiga kaz zote za nyumban lazima uchoke,....znachosha hasaaaaaaa..

wewe upo job ,kuna vidil vya apa na pale jaman ...mwenzio yupo tu hm hana ata mishe mishe ,mikaz kibao..na wengne ata kula hawali nao mezan wanaenda kula jikon au nje afu wampa efu 30 sjui 40?

jaribun kuwapa kaela kazuri kdg...tuwafikirie wenzetu jaman...we efu 40 ata ukiamua kutoka wknd AITOSH NA MARAFIKI ZAKO...au ata km aujatoka lakin 40 ndg sana.....

muwape fresh waweze kufanya poa kaz zao..
na km mungu amaekubariki na msaidiz wako ana adabu basi si mbaya km ukimsomesha pia km ana mwamko uo...
Mhhh jamani si kweli kuwa 40,000 kwa mwezi ni pesa ndogo ukizingatia kuwa hanunui kitu chochote. Anakula kwako, Nguo unamnunulia, akiugua unamtibia. Hebu fikiria kama unampatia 80,000/= kwa mwezi kama ambavyo wafanyakazi wa kampuni za usafi huwalipa lakini kila siku wanalipa nauli, wanalipia nyumba, chakula na nguo zao. Mi nafikiri 40 thousands is very fair
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom