Natafuta fremu ya biashara maeneo ya Mbezi Louis na jirani

kibebi

Senior Member
Feb 22, 2013
108
247
Hello!

Heri ya mwaka Mpya. Nilipata changamoto nikapotea kidogo Ila nimerudi (wakulungwa wanaelewa nimepotea wapi).

Back to business.

Ninaomba mnisaiaide kupata eneo zuri la biashara ya mahitaji ya nyumbani (unga, mchele, maharagwe, sukari, chumvi, diapers, mafuta na mahitaji mengine mengi ya nyumbani). Napendelea kuuza reja reja...

Eneo hilo niweze pia kuwa nauza fresh juice na maziwa kwa kuwasambazia watu waliopo eneo hilo na jirani na duka (kwa hiyo uwepo wa vijiwe na mzunguko wa watu ni muhimu).

Nitatoa kifuta jasho kwa atakayenielekeza chimbo La kueleweka nisije kata mtaji wangu.

Eneo napendelea liwe mitaa ya Mbezi ya Kimara, mitaa ya Kimara, pia Goba japo Goba sio kipaumbele.

Nasisitiza kutoa chochote kwa atakayenipa ushirikiano wa eneo zuri na ikiwezekana frem kabisa.

Asanteni kwa ushirikiano.
 
Kabla sijaenda kwa dalali nataka nipate maoni ya wapi nielekee...
Nimekuwa muoga Sana nisije Zika mtaji. HeLa saa hivi ni ngumu
Nasisitiza kutoa chochote kwa atakayenipa ushirikiano wa eneo zuri na ikiwezekana frem kabisa. Hapo lazima mtu kati ahusike mkuu.
Ila JF ni kubwa unaweza kupata mmiliki wa flem na mkayajenga.
All the best 🙏
 
Nasisitiza kutoa chochote kwa atakayenipa ushirikiano wa eneo zuri na ikiwezekana frem kabisa. Hapo lazima mtu kati ahusike mkuu.
Ila JF ni kubwa unaweza kupata mmiliki wa flem na mkayajenga.
All the best
Asante Sana
Nitampa chochote kitu atakayenipatia password
 
Ushauri wako pls
Nini kingine kifanyike?
Ki ukweli inategemea upo sehemu gani je unakaa kwako au umepanga? na passion yako ni nini? maana ukifanya kitu ambacho sio hobby yako basi utaishia kupoteza pesa tuu.
 
Back
Top Bottom