Nasumbuliwa sana tumbo

ufumawicha

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
504
209
Ni mwaka wa 22 ninasumbuliwa na tumbo.

Mwanzoni ilikuwa ni mara Amiba, minyoo na kichocho cha tumbo! Kila nikitumia dawa napata nafuu kwa wiki moja au mbili kisha gwaride linaanza upya.

Mei, 2015 nimehamia Mbeya lakini hali inaendelea! Cha ajabu nimepima hapa na kujibiwa nina madonda ya tumbo.

Nikawaona wataalamu wa tiba lishe pamoja na kuwalipa sh.600,000/=Hakuna nafuu sasa naishiwa nguvu mwilini naweza hata kuanguka! Mwili unauma sana, mgongo shingo na kiuno ndo usiseme.

Imebidi hata kulala niwe nalalia tumbo vinginevyo maumivu ni makali sana! Nipeni ushauri please!

Naomba kwa jinsi nilivyo serious msiweke utani kwenye hili suala langu!
 
Ni mwaka wa 22 ninasumbuliwa na tumbo.Mwanzoni ilikuwa ni mara amiba,minyoo na kichocho cha tumbo!Kila nikitumia dawa napata nafuu kwa wiki moja au mbili kisha gwaride linaanza upya.Mei,2015 nimehamia mbeya lakini hali inaendelea!Cha ajabu nimepima hapa na kujibiwa nina madonda ya tumbo.Nikawaona wataalamu wa tiba lishe pamoja na kuwalipa sh.600000/=Hakuna nafuu sasa naishiwa nguvu mwilini naweza hata kuanguka!Mwili unauma sana,mgongo shingo na kiuno ndo usiseme.Imebidi hata kulala niwe nalalia tumbo vinginevyo maumivu ni makali sana!Nipeni ushauri please!!Naomba kwa jinsi nilivyo serious msiweke utani kwenye hili suala langu!

Nenda kwa Dr rahabu atakutibu vidonda vya tumbo, ndugu yangu aliponea kwake
 
Jamani, kama kuna mtu ana namba za simu ampe kwa msaada zaidi. Pole sana ndugu na imani humu utapata msaada.
 
Ni mwaka wa 22 ninasumbuliwa na tumbo.Mwanzoni ilikuwa ni mara amiba,minyoo na kichocho cha tumbo!Kila nikitumia dawa napata nafuu kwa wiki moja au mbili kisha gwaride linaanza upya...
Pole ndugu,japo sijui imani yako lakini nakushauli unapoendelea na matibabu mfate mtumishi wa MUNGU akufanyie maombi,yamkini kuna mambo ya giza pia umeyakumba mahali,kimbia Arusha na umtafute mtu anaitwa Christopher Mwakasege akufanyie maombi.

Kumbuka kua na nia ya kuacha dhambi yoyote ile,jambo jingine la kufikilika usiukili sana ugonjwa,ukatae kwa maneno ndani ya nafsi yako na jione kama wewe ni mzima na hakika utapona,usiache pia kuwaona Doctors.pole na MUNGU muumba wa mbingu na inchi akuponye
 
Pole sana ndugu kwa UWEZA WA MUNGU utapona usiache kufata ushauri unaopewa hapa
 
itakuwa una presha nenda hosp. kucheki zaidi, BTW pole sana
 
itakuwa una presha nenda hosp. kucheki zaidi, BTW pole sana

Presha,kisukari na malaria nimepima mno wanasema sina tatizo ni tumbo.Linawaka moto halafu wakati mwingine inakuwa kama miti imesimamishwa tumboni inanichoma sana!
 
tumia juice ya limao sana au weka kwenye chai.

kuna matatizo mengine ya tumbo hayanaga tiba ili yanakua managed.
 
Pole sana,je tumbo umeshawahi kupimwa? wanakuambia tatizo ni nini?hiyo midawa yote ulokula ni sumu tosha!
 
Netragen! Netragen! ni dawa ilikuwa inatangazwa kuwa kiboko ya vdonda vya tumbo ifuatilie inaua H.pyroli wa ulcers.
 
tumia juice ya limao sana au weka kwenye chai.........

kuna matatizo mengine ya tumbo hayanaga tiba ili yanakua managed.

Limao halina urafiki kbs na vidonda vya tumbo. Ushauri wa maana awatafute wataalam kama alivyoshauriwa na wadau hapo juu
 
Anza kutumia juice ya carrot asubuhi na jioni kabla ya chai na kabla ya kula. Kunywa glass moja.
 
Kama utaweza kufika siku ya Jumamosi pale Mwanjelwa stand ya daladala KABWE fika Jumamosi kunasemina nzuri za afya. Ukifika nitafute kwa namba 0763797853

Semina hiyo inafanyikia wapi?Ili nihudhurie na ni nani wanaoisimamia?Maana jamaa wa Lupimo sanitarium walinitibu nao sikupata nafuu,nikahamia kwa fadhaget naye pia bado.
 
Wanasimamia GNLD na pale utapata maarifa ya jinsi ya kuanza taratibu kulipunguza then baadae utakuwa huru kabisa mimi ninaamini hivyo maana wengi wamejikomboa na matatizo sugu kama yako. Nitafute hewani nijue ulipo ilikama itawezekana tujue namna yakufanya kabla ya siku husika.
 
Inafanyika pale MWANJELWA KARIBU NA STENDI YA KABWE kama unapafahamu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom