Nassari si chaguo letu..

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Joshua Nassari,mgombea ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki-CHADEMA si chaguo letu watazamaji,wasikilizaji,wafuatiliaji na washabiki wa vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi Arumeru Mashariki bali ni chaguo la wa-Meru wa Arumeru Mashariki.Wanamhitaji sana Nassari.Hawahitaji mbwembwe za kugawa fedha,kofia,fulana,vyakula na matusi.Wanamhitaji Mbunge aliye karibu yao.Wapo wazee walionidokeza kuwa hata Nassari angegombea kwa tiketi ya SAU,wangemchagua tu.

Jumapili,ingawa ni siku ya wajinga Duniani,ni siku muhimu sana kwa wana-Arumeru Mashariki.Wa-Meru watakuwa wajanja siku hiyo.Wako tayari kuwa-Wade CCM.Wamejiandaa vyakutosha.Wamejiandaa kupiga kura za kumtosha Nassari.Shahada zao za kupigia kura hazinunuliki.Wanasonga kwa mwendo wa ushindi..
 
nina amini atakaeshinda sasa awe makini kwani 2015 nyuma yake watakua watu wachache wa kumpigia debe, zitakua nguvu zake pekee zitakazo mrudisha
 
nina amini atakaeshinda sasa awe makini kwani 2015 nyuma yake watakua watu wachache wa kumpigia debe, zitakua nguvu zake pekee zitakazo mrudisha
Usiwe na shaka, hebu tafuta picha za kampeni zake za 2010 uone kuwa hata bila ya viongozi wa kitaifa angeshinda.
 
NILIPOSOMA HEADING YAKO NILITISHIKA!

Labda nitoe kisa nilichoshuhudia!
Jumamosi nilikuwa kwenye msiba wa ndugu wa MwanaJF mwenzetu katika eneo la Arumeru!
Mara MC akatangaza kuwa kuna salamu za vyama, nikaona kundi kubwa la wanaCDM, wakiwa wamepiga Gwanda, wakasonga mbele kwa machungu mbaya kabisa, na akina mama wakilia, wakasaini daftari la msiba, na kuwasilisha rambirambi yao(fedha) kwa wafiwa...Kisha wakaondoka wakinyanyua mikono, na waombolezaji kwa muda waliacha shughuli ya maombolezo na kufuatilia kwa umakini tukio lile, huku wakipunga mikono kwa nguvu hewani, huku wakizungumza kichinichini kuwa hakika tunaomba uchaguzi uwe kesho! ili magamba wakomeshwe!
Hakika kama kungekuwa na mtu kichaa pale akatamka...Peopleeeeez!, sijui hali ingekuwaje!~

Baada ya tukio hilo MC akaendelea kuita kama kuna chama kingine chochote kilichokuwa na uwakilishi, ambapo hakukuwa na wengineo!
 
Tumuombee Nassari Mungu afanye kitu..nimeanza maombi ya usiku kwa ajili yake.

MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI ARUMERU,MUNGU MBARIKI KIJANA NASSARI
 
Heading ina shida maana kusema Nassari si chaguo letu ina maana Wameru hawamtaki Nassari tofauti na ulichoandika ndani na ndiyo maana kila mtu anasema nimeshituka ama sijakuelewa.
Soma tena Mkuu...hasa aya ya kwanza
 
Back
Top Bottom