Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,599
Binafsi najikuta mara nyingi nikipata shida kuamini kama kweli kuna kitu kinachoitwa mapenzi ya kweli katika ndoa zetu. Hata hivyo, siku ya Jumapili (1 Aprili 2012) kulikuwa na story kwenye kipindi cha Njia Panda katika Clouds Radio ambacho kimedhihirisha kuwa inawezekana kabisa kukawepo na mapenzi ya kweli. Ingawa nimechelewa kipindi kwa karibia dakika 30, hata hivyo nimeweza kupata undani wa story iliyokuwa inaongelewa.
Story yenyewe inamhusu Bwana Kassimu, ambaye ni dereva wa pikipiki (boda boda) anayeishi eneo la Mabibo jijini Dar. Kassimu alienda siku moja kwenye bar moja ambayo hakuitaja, iliyoko jirani na kwenye kijiwe chake, ili kupata mchemsho wa kuku. Alihudumiwa na msichana aliyeitwa Nasra ambaye alitokea kuvutiwa naye. Jamaa alimwomba wakae wote katika meza aliyokuwa ameketi na wakapata chakula pamoja. Baada ya hapo, Kassimu alihisi mvuto wa ajabu na alirudi kwenye ile bar jioni, wakala chakula cha jioni pamoja.
Ingawa alijaribu kujizuia kwenda kwenye ile bar mara kwa mara, alijikuta anashindwa na kulazimika kwenda. Siku moja akiwa kwenye ile ba na amekaa na Nasra, ulitokea ugomvi kati ya Nasra na boss wake (meneja wa bar) hadi ikambidi Kassimu kuingilia kati. Alimwomba Meneja amwache Nasra kwa kuwa ni mpenzi wake. Baada ya ugomvi kuisha, Nasra alimweleza Kassimu kuwa Meneja alikuwa anamlazimisha kwenda kufanya ngono na mwanamume ambaye Nasra mwenyewe hamfahamu na wala hakuongea naye. Ilielezwa kwamba huyo meneja alikuwa na tabia ya kuwauza wafanyakazi kwa wanaume na malipo kupokea yeye. Wale waliokubali kufanya ngono na wanaume waliotafutwa na Boss wao, hawakulipwa chochote kwani ilichukuliwa kama sehemu ya kazi yao. Kutokana na ugomvi huo, Nasra alifukuzwa kazi na Kassimu alipokuja tena pale kwenye bar hakumkuta.
Kassimu aliwauliza wenzake Nasra ambao walimpa msaada hadi akampata. Bila kusita, alimwomba Nasra aende kwake wakaishi pamoja. Nasra alikubali na walipanga kutafuta pesa ili wakafanye taratibu za ndoa, ikiwemo kwenda kwa wazazi wa Nasra huko Sengerema. Hata hivyo, Nasra alipata mimba na ikawabidi kuahirisha mipango ya ndoa. Ilipofika wakati wa kujifungua, Nasra alipelekwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa ajili kupata huduma. Alikaa pale hadi siku ya pili alipojifungua mtoto wa kiume (amepewa jina la Kudra) ila mama hali yake haikuwa nzuri na akapelekwa Muhimbili kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU). Baada ya jitihada za madaktari kushindikana, Nasra alifariki dunia kwa kile kilichoelezwa kuwa ni pulmonary edema (kujaa maji kwenye mapafu) na kuzikwa maeneo ya Mabibo . Hata hivyo, Kassimu bado hawajui ndugu zake ikiwa ni pamoja na familia ambapo Nasra alifikia na kufanya kazi za nyumbani.
Kutoka na ukata, Kassimu ameshindwa kumlea mtoto wake ambaye ana umri wa mwezi mmoja na nusu, na sasa anasaidiwa na jirani yake ambaye ameamua kumchukua mtoto na kuishi naye. Hata hivyo msaada zaidi kwa ajili ya kununua maziwa ya mtoto na mavazi unahitajika. Kassimu anapatikana kwa namba 0713 540 760.
Karibuni tena kwenye jukwaa letu tukufu la MMU, na naamini kwamba matokeo ya Arumeru na kwingine yanatupa nguvu ya kusonga mbele !!
Babu DC!!