Kimalingano
JF-Expert Member
- Mar 27, 2023
- 422
- 525
Nilifuatilia maelezo ya Menejimenti ya TPA hivi karibuni waliyoyatoa kupitia vyombo vya habari.
Maelezo yao yalikuwa ni kwamba shehena imeongezeka zaidi ya matarajio yao kwa meli nyingi zaidi kushushia mizigo kwenye bandari zetu hususan bandari ya Dar.
Hata hivyo,viongozi hao hawakutaka kueleza mapato yamepanda kwa kiasi gani kutokana na shehena kuongezeka hadi walipoulizwa na waandishi wa habari ndipo wakalazimika kutoa maelezo yaliyokuwa na ukakasi.
Walijibu kuwa mapato bado hayajafikia lengo ambalo ni zaidi ya bilioni 600 ambapo hadi sasa wamekusanya bilioni 500 tu.
Wakataja sababu kwamba ni kutokana na mizigo mingi bado haijapakuliwa ili ilipiwe.
Maelezo ya namna hii yana ukakasi. Ni vema Bunge likamuagiza CAG afanye ukaguzi maalumu.Kwa sababu tayari kuna fununu kuwa kuna ukwepaji wa ulipaji wa kodi mbalimbali katika bandari zetu.