Naseeb Abdul (Diamond Platinumz), akaliwa kooni na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Serikali kudai hela ni sawa au sio sawa?

Ni sawa kwasababu sasahivi hali yao mbaya watadai hadi mama ntilie.. walikua wapi miaka yote hiyo mitano?? Diamond ni very popular huwezi kuniambia walimsahau.. Bado msimamo wangu ni ule ule kuna walakini hapo. Alafu kwanini wengine hawajapewa hizo barua, au ndio wanaanza na aliye na kingi
 
Hapa ndio utaona wale wenye vimshahara vya laki 6 ambao wanaomwonea wivu kijana anayepambana watakavyotoa povu.. Wapo hapa wanasubiri jamaa afilisike
yaani nimeshangaa na bado naendelea kushangaa! ni ushirikina live!
 
Hawa wamekurupuka kisa kuona mtu amepanda kimapato ila mafisadi wanagawana mabilioni bila kutoa kodi...

Hii serekali dhaifu sana inapoacha wawekezaji wana safirisha madini kwa bei sawa na bei ya mkaa
 
leo nimeamini watanzania ni WACHAWI! kha!

Uchawi gani bibie, ukifungua kampuni ujue kuna mambo kama haya, lazima uonyeshe mapato na matumizi, faida na hasara, na financial position ya kampuni yako, la sivyo utajificha ila siku ukikamatwa ni kesi ya ukwepa kodi na uhujumu uchumi inakuhusu, kila mwaka mwaka wa biashara

Mishahara unayolipa wafanyakazi wako unatakiwa uwakate PAYE, upeleke TRA, Skills development levy kampuni inatakiwa ilipe, bado social security
 
Nimesoma sehemu nyingine mtandaoni kuwa baru ahiyo ni feki ndiyo maana haina muhuri wala tarehe; TRA hawajamdai kodi. Hata hivyo kulipa kodi ni wajibu wa raia wote siyo wachache tu walipe kdoi wengine wasilipe. Kila mtu anahangaika kupata pesa yake na kila mtu anatakiwa kulipa sehemu ya mapato yake serikalini.
 
Wa kupeleka mil 20 kwa mwezi nani? wewe? Ebu usinichekeshe na kijiba chako.


Hapa ni kariakoo nikiwa nafata mauzo ya nusu siku

Na hayo ni baadhi ya makusanyo, nikukumbushe nimetoka ofisini for lunch
 

Attachments

  • 1425898038653.jpg
    1425898038653.jpg
    68.4 KB · Views: 177
  • 1425898278473.jpg
    1425898278473.jpg
    84.2 KB · Views: 171
Back
Top Bottom