Naseeb Abdul (Diamond Platinumz), akaliwa kooni na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Nilikuwa najaribu kuonyesha hata wanamziki wakubwa walivoonekana kukerwa na mambo ya kodi!! Huyo dube aliwahi kuulizwa kuwa anapinga watu wasilipe kodi? akajibu.....nataka kujua tu pesa yangu inaenda wapi na inafanya kweli lichokusudiwa! (au ndio zinakusanywa apewe Chenge?)

Hoja yako ni General Sana, kwa mantiki hii hata bakhresa anahaki ya kuuliza makato ya kodi toka kwenye miradi yake inafanya kazi gani?......
 
Ivi unaweza ukawa mtupu kiasi iki?

Nashangaa kwasababu ni diamond watu mnajidai wazalendo sana.
Wakati nchi hii hakuna anayelipa kodi halali zaidi ya waajiriwa tu.
Na hata kama wewe ni mjasiriamali nina uhakika hulipi kodi inayotakiwa
 
"Serikali corrupt haikusanyi kodi!inaishia tu kufukuzana na hivi vimachinga,vi-MPESA,vibodaboda,VI-DIAMOND...."
 
Nashangaa kwasababu ni diamond watu mnajidai wazalendo sana.
Wakati nchi hii hakuna anayelipa kodi halali zaidi ya waajiriwa tu.
Na hata kama wewe ni mjasiriamali nina uhakika hulipi kodi inayotakiwa

Kwa iyo unaona diamond hapaswi kulipa kodi? Sio kila swala linalomhusu huyu msanii uingize swala la mahaba ndugu, if am not mistaken alishawahi kujitapa ana karibu zaidi ya 2 billion.tshs.Alipe kodi bwana.
 
Tunashindwa kuelewa tu kutokana na umaarufu wa dlamond ndio uliofanya jambo ili kujulikana lakini ukwel ni kwamba kulipa kodi ni jukumu la kila raia katika nchi yoyote kinyume chake usipolipa kodi utatoa faini au kifungo jela!!! Tusiingize siasa kwenye mambo ya msingi

Sio kila raia analipa kodi.
Mfano kikwete ni raia wa Tanzania lakini halipi income tax,PAYE halipii customs duties kwa chochote anacho import.
Posho zote anazopata safari anazosafiri wengine wote anaosafiri wanazilipia kodi lakini yake haikatwi.
Mwaka huu wabunge watapata gratuity zao wakati wanafunga bunge lakini hazitakatwa kodi.
Ningekuorodheshea misamaha ya kodi wanayopata wanasiasa,ila nitawavunja moyo watu kulipa kodi
 
Mkuu zipo shughuli nyingi tu zenye kipato na haukatwi kodi kisheria
nyiingi tu......

Na kama sheria bado inakataza muziki kuwa ni shughuli ya kibiashara basi Diamond akipata mwanasheria mzuri halipi hata senti moja

kumbuka wakati wa Nyerere ilikatazwa muziki kuwa shughuli ya kibiashara

Thubutu, kwa sheria ya kodi ya sasa kila kipato lazima kilipiwe kodi, kwa sasa hata pesa ya kustaafu inakatwa kodi
 
Siasa za kijinga hizi ccm amuwezi kumcontrol kila msanii...nyimbo alizoimba Komba na THT haziwatoshi? zipigeni hizo hizo ata km Komba hayupo.

Kodi ni sawa kulipa ila kuwe na usawa, tuone hizo barua anapelekewa mpaka mzee yusuph, rose mhando, jide, MwanaFA, msama ,primetime, ndege.

Kaja T.I mlimkata sh ngapi? Davido mlimkata sh ngapi? Rick ross mlimkata sh ngapi?

Oneni ata aibu.
 
Thubutu, kwa sheria ya kodi ya sasa kila kipato lazima kilipiwe kodi, kwa sasa hata pesa ya kustaafu inakatwa kodi

Pesa ya kustaafu inakatwa kodi kwa wafanyakazi wote isipokuwa kwa wabunge tu.
Bunge la mama makinda likifungwa wabunge watapewa hela za kustaafu ubunge lakini wamejiwekea exemption hawatalipa
 
Hoja yako ni General Sana, kwa mantiki hii hata bakhresa anahaki ya kuuliza makato ya kodi toka kwenye miradi yake inafanya kazi gani?......

We vipi!? tuna mwongelea mwanamziki hapa!! na nimemnukuu mwanamziki pia..unashida gani!? Mbongo bana, kwahiyo unadhani Bakhressa hana haki ya kujua hatma ya kodi yake?... atoe tu..then aone barabara anazopita mbove akae kimyaa.... !! Kumbe hujui hata unachoongea!?
 
esma ni nani??
Na baba yake mtoto wa esma yuko wapi?


esma ni mdogo wa diamond,ana watoto 2 na mimba juu,kuhusu picha m google utampata mme wake anaitwa petit man ni dereva wa wema sepetu uki mgoogle utampata

 
Nimesikitishwa sana na baadhi ya watu mnaowashangaa TRA kwa maamuzi hayo badala kuwapongeza.
Mimi binafsi naona wamechelewa, walitaliwa wafanye hili suala zamani sana.
Kimantiki, mtanzania yeyote anayepata kipato ni lazima alipe kodi.
Yaani mwl anaelipwa laki nne analipa kodi halafu mnashangaa TRA kufuatilia kodi za Diamond?
Tuwekeni mapenzi na itikadi pembeni, kodi ni lazima ilipwe.
Hapa sitaki kuzungumzia hzo kodi wanazosamehewa wakezaji, cziungi mkono hata kwa dawa, ila hazina uhusiano na ulipaji kodi wa Diamond
mbona mkuu wa nchi na mzee pinda hawakatwi kodi yyte kwenye mishahara yao
 
Sheria za nchi ndio zinzoongoza kazi za TRA. Kama Mkapa na Kikwete wameona wachimbaji wakubwa wa Madini wasilipe kodi, TRA haziwezi kufanya chochote.

Lakini kama ipo ndani ya sheria kumdai Diamond lazima alipe kodi. Mfanyakazi mwenye kipato kidogo kwa mwaka kuliko Diamond analipa kodi. Kwa Diamond asilipe?

Biashara pekee ya serikali popote ni kutoza kodi stahiki!

Umeongea kisomi mkuu
 
Na Wabunge pia Mkuu ambao mishahara yao na marupurupu kwa mwezi ni zaidi ya milioni 11 na kiinua mgongo chao baada ya kumaliza Bunge kila baada ya miaka mitano ni 75 million kwa kila mbunge pesa yote hii haikatwi kodi, lakini mwalimu anayelipwa mshahara wa 200,000 kwa mwezi analipwa kodi!!! Kwanini kusiwe na haki hapa na huyu mwenye kipato kidogo asilipe kodi? Na kodi ilipwe na wenye kipato kikubwa kuanzia labda shilingi milioni 1 kwa mwezi?

mbona mkuu wa nchi na mzee pinda hawakatwi kodi yyte kwenye mishahara yao
 
Back
Top Bottom