NASAKA MKE WANGU NASAKA MKE WANGUuuuuuuuu

Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,937
1,437
Teh teh teh teh .

michezo gani mnakumbua ya utotoni.

Kuna ule mchezo wa Nasaka mke wangu naska mke wangu......

A anasema : Nasaka mke wangu nasaka mke wangu uuuuuu
B wanajibu : Hapa hayupo hapa hayupooooooo

A anasema: Kaenda wapi kaenda wapiiiiiiiii
B wanajibu kaenda kusuka kaenda kusuka

A : anasema; Kachukua nini kachukua niniiiii?i

B
wanajibu : Kachukua chanuo namafuta
............

Dah nimesahau wimbo hu ulivyouwa unaishia ila mwisho wa mchezo kama sikose ilikuwa mnavutana. kunakuwa na makundi mawili

Mchezo gani unakumbuka wa utotoni ? Je ulitengeneza magari ya maboski na visoda, Tiara au vishada kubumba watoto kwa udongo?

Tuendelee watoto wa jana.
 
chanuo kampa nani chanuo kampa nani?
chanuo kampa msusi chanuo kampa msusi!!

huu mti gani,
wa mchongoma
nikiukata,
haukatiki
nikiuvunja
hauvunjiki!
......................................
 
mimi nimekuwa mkubwa
nimeshangazwa na ule wimbo wa ukuti ukuti....

kwa sababu kwenye ule wimbo wanasema tumpeleke mnazi mmoja...

enzi tupo watoto tulikuwa tunatumia hospitali ya mnazi mmoja na sikuona ajabu

leo tanzania nzima wanaujua ule wimbo but swali ni kwa nini wote tuliimba mnazi mmoja?????
 
chanuo kampa nani chanuo kampa nani?
chanuo kampa msusi chanuo kampa msusi!!

huu mti gani,
wa mchongoma
nikiukata,
haukatiki
nikiuvunja
hauvunjiki!
......................................

Misss ulicheza kombolela wewe au ulikuwa mtu wa Sheki redi sijui
 
duh kombolela..
wengi walijifunza mengine kwa huu mchezo..lol
pamoja na baba na mama...lol
 
mimi nimekuwa mkubwa
nimeshangazwa na ule wimbo wa ukuti ukuti....

kwa sababu kwenye ule wimbo wanasema tumpeleke mnazi mmoja...

enzi tupo watoto tulikuwa tunatumia hospitali ya mnazi mmoja na sikuona ajabu

leo tanzania nzima wanaujua ule wimbo but swali ni kwa nini wote tuliimba mnazi mmoja?????

hapo sasa nadhani ndio utoto wenyewe au nyimbo zilitungwa na wakubwa????
 
hapo sasa nadhani ndio utoto wenyewe au nyimbo zilitungwa na wakubwa????

sijui asili ya hii nyimbo,natafuta asili yake....

yaani sasa unakuta watu wazima waliozaliwa na kushi labda mwanza,au kigoma..
but na wao utotoni waliimba hivyo hivyo........

so nashangaaa...........
 
kioo kioooo alikivunja naniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii....lol
Sijuiiii Sijuiiiiiii. Wa mwisho akamatwe......

Haaaa huu wa kioo ndio nimeuchanganya na huo nasaka mke wangu. Huu w aki ndio ulikuwa wa kuvutana. Au sio Jestina? Nishasahu Nasaka mchezo wa nasakam mke wangu scene ya mwisho nini kilitokea. kuna yeyote anakumbuka
 
sijui asili ya hii nyimbo,natafuta asili yake....

yaani sasa unakuta watu wazima waliozaliwa na kushi labda mwanza,au kigoma..
but na wao utotoni waliimba hivyo hivyo........

so nashangaaa...........

uko sahh ii kabisa na mm ni mmoja wao sikuwa dar lakini huo wa mnazi mmoja nimeimba sana enzi hizo teh teh teh
 
Back
Top Bottom