Nahonyo
JF-Expert Member
- Dec 28, 2012
- 5,374
- 5,016
Nimekua mpenzi sana wa kula pweza, ila kula pweza Dar, kwa hawa wauzaji wetu barabarani, inataka uwe unafanana nao, usijue uchafu ni nini.
Unaona mtu amechagua mkia wa pweza, anaomba akatie vipande, jamaa anashika kwa mkono tu bila kunawa, akili ya kutumia uma, kushikia pweza anaekatwa hawana, mkono huo huo anashika pweza, anapokelea hela, anashikia stick anayojichokonolea kwenye meno.
Bakuli sasa ya kuwekea Supu, ni za plastick mpaka zimeingia rangi ya mchuzi wa pweza, jiulize maji wanayooshea baada ya mteja wa kwanza kuitumia, je vijiko vinanavyoingia ndani ya mdomo, wa kila mteja anekunywa supu, vinaoshwaje.
Ndugu zangu wauza pweza mjipende kwanza nyie ili muwapende wateja wenu pia, Pweza tunapenda ila.