Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Tulia utawasikia watoto wa mjini!!
Nadha utaipenda wacha mwanga bashite aendelea kumlinda sizonje!!
 
Wasalaam wana jamvi.
Wengi hasa UKAWA walivyosikia Nape ataongea leo walijua wanapokea mwanachama mpya au anakwenda kuropoka wanayopenda kuyasikia.

Lakini Kibaya zaidi Nape amewakatisha tamaa maana waliokuwa wanamsikiliza walitamani kusikia akisema sasa basi naachia ubunge.....

Leo ndio nimegundua waandishi walio wengi wana ushabiki wa vyama kabisa kabisa maana walikuwa wanashangilia huku wakisema semaa baba semaa...hahaha lakini alichokisema Nape kimewavunja moyo waandishi na UKAWA.

Hongera rafiki Nape umetimiza wajibu wako sasa ni zamu ya mwenzio.
 
BILA KIFICHO HUYU JAMAA NA KINANA WAMEKISAIDIA SANA CHAMA KUANZIA 2012 =2015 MAGU ATAMBUE UMUHIMU WAKE
ila hata kama sio leo kesho atautambua wana ccm tuache unafiki katika haya
 
Kuanzia uchaguzi ujao tunaomba tume ya uchaguzi iweke utaratibu wa kupima akili wgombea wake kuanzia ngazi ya chini kabisa.
 
TUFUNGE, KUSALI NA KUOMBA, Kila mtu kadiri ya IMANI yake

wee MERCIFUL, niache kula kwa sababu gani? nijitese na njaa kwa sababu zipi? waache watifuane wanajuana wenyewe walipotoka, walipo na wanapokwenda! Labda nifunge, nisali na kuomba kwa ajili ya matatizo yangu mengine na familia yangu lakini si haya ya akina Nape, JPM na Makonda
 
Najuta kumpa Magufuli kura yangu,tena najuta kweli kweli.Hivi Nape yule aliyepambana na upinzani mpaka kuiweka ccm sawa leo hii ndiye anayedhalilishwa hivi???tena sababu ni Makonda????

Najuta walahi.Mungu nisamehe mie mkosefu,katu sitorudia kosa.
 
Wagalatia 4:15-17 "Mlikuwa wenye furaha; sasa kumetokea nini? Naapa kwamba wakati ule mngaliweza hata kuyang'oa macho yenu na kunipa mimi. Je, sasa nimekuwa adui yenu kwa sababu ya kuwaambieni ukweli? Hao watu wengine wanawahangaikia ninyi, lakini nia zao si njema. Wanataka kuwatenganisha nami ili ninyi muwahangaikie wao.

Yohana 8:32 "Nanyi mtaijua kweli, nayo kweli itawaweka ninyi huru.”


My Take: Lisomeni neno la Mungu, limesema yote kwa kila hali tuipitiayo kama binadamu. Kila hali, iwe ya furaha, ya huzuni, ya taharuki au ya utusitusi, ina majibu yake ndani ya Maandiko Matakatifu
 
Back
Top Bottom