Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

UPDATES;

=======

13:08hrs: Nipo hapa Protea hotel, Mheshimiwa Nape bado hajafika. Ntamsubiri hapa hapa.

Ametokea mtu anayeitwa Iddi Suleiman ambae ni meneja wa Protea na kudai mkutano hautakuwepo na waandishi walipombana nani kazuia, alisema akaulizwe RPC wa Kinondoni.


Hii hoteli ilikuwa inatoa ukumbi bure?
Je gharama alizoingia mteja inakuwaje?
 
Pongezi kiduchu zimfikie Nape Nnauye kwa kuonesha kuwa kinyume na ufedhuli, lakini pongezi hizo kiduchu na hatua yake ya kuwa kinyume na ufedhuli, havifuti ufedhuli wake.
Kwa maneno machache tu;

Nape ni kijana wa kitanzania, mwanachama wa CCM aliyetumia njia anazojua kujipenyeza hadi kufikia kushika nafasi za juu za uongozi wa chama na serikali. Huyu na vijana wenzake wa CCM ndio waliozunguka nchi nzima kumtukana Lowassa, ambaye wakati huo alikuwa moja kati ya watu muhimu ndani ya Chama chao, lakini kwa sababu ya kutumikia makambi na makundi ya chama, wakazunguka kutukana na kupakaza uongo kwa manufaa ya kundi fulani.

Huyu ndiye aliyetangaza ushindi wa CCM kwa goli la mkono.

Huyu ndiye aliyewatolea maneno machafu waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi mkuu mwaka 2015
Huyu ndiye alifungia gazeti la mawio na kutishia uhuru wa vyombo vya habari nchini
Mbaya kuliko zote, Nape Nnauye ndiye aliyekuwa injinia wa kupitisha muswada wa sheria mbaya kuliko zote ya habari, ambao tofauti na lengo linaloelezwa, ukiisoma sheria ile na kuielewa, utagundua sio tu inaminya uhuru wa kupashana habari lakini pia inapingana na stratejia za kupambana na ufisadi, stratejia ya 'Whistle blower policy' inayotajwa kuwa bora kabisa katika kupamabana na ufisadi, inawekewa ukinzani na sheria ya Habari ambayo Nape alihusika moja kwa moja katika kuipitisha.

kwa upande mwengine,Nape amekuwa mtu muhimu sana ndani ya CCM, mambo ya kutukana Lowassa yanaweza kuwa ni ujana tu, na haya ya shetria ya sheria ya Habari ni uovu usiosameheka lakini ni kwa manufaa ya CCM, sio kwa Taifa. Hakuna ushahidi kwamba vijana wa vyama vingine wangefanya kwa manufaa ya Taifa tu kinyume na manufaa ya chama chao. kwa hivyo, ikiwa anahitaji huruma, basi atahitaji zaidi kutoka kwa wanaCCM wenzake.

Ushauri wa bure:

Huku nikiwa na hakika kabisa kuwa Nape ni mzoefu wa mambo ya siasa za Tanzania, nikitambua pia kuwa yeye kama mwanasiasa ana tamaa ya madaraka makubwa zaidi ya aliyowahi kushika, ni vema akawa mkimya kwa kipindi hiki kuliko kipindi chochote kile. Akae kimya, arudi kuwatumikia watu wa Mtama na watanzania,atafute namna (hapo baadaye) ya kukubalika na watu (sio wafuasi). Anaweza pia kurudia kusoma kitabu cha Robert Green; 48 laws of power, aangalie amekosea wapi.
zaidi ya hayo, amtafute mzee Lowassa amuombe radhi na kuomba somo zaidi la siasa, ajifunze kwa nini Lowassa bado ni mtu mwenye ushawishi mkubwa pengine kuliko aliyemteua na kumtumbua.
 
Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kinondoni amezuia kufanyika mkutano ambao Mhe. Nape ailkuwa aufanye na waandishi wa habari pale Protea Hotel
 
Nasikia RPC Kinondoni kazuia mkutano wa Nape na wandishi wa habari.. Is it true!??
 
NI aibu kuwa na rais ambae anazuia hadi press conference!! Wale mbwa wanaosemaa kwamba JPM ni jasiri; sasa kama ni jasiri anaogopa vp hata press conference!! Huyu mtu hafai hata kidogo na lazima uwe mgonjwa wa akili ndipo unaweza kumuunga mkono!!

Aibu sana.
 
Nape Mwenyewe Huyu Hapa.
0128869490610b2578480d4033134f42.jpg
 
Back
Top Bottom