Nape: Ruge alipofariki nilijifunza faida ya kuishi vizuri na Watu, mliona jinsi alivyozikwa na Watu wengi!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,036
142,116
Akihojiwa na mtangazaji Salama Jabir wa Eatv mh Nape amesema yeye, January Makamba na marehemu Ruge Mutahaba walikuwa marafiki wakubwa sana

Nape amesema yeye na January ni ndugu kwa sababu baba zao ni ndugu japo haukuwa undugu wa damu hivyo wanashirikiana wao na Watoto wao katika mambo mbalimbali

Anasema January na Ruge walisoma Marekani hivyo walivyorudi nchini ndio urafiki wa mapacha Watatu Nape, January na Ruge ukaimarika

Nape amesema kifo cha Ruge kilimpa somo juu ya faida ya kuishi vizuri na Watu na hasa ukiangalia namna alivyozikwa

Source: Eatv

Mlale unono 😀
 
Mlale unono
Nape chamatusi ndiye anajua kuishi na watu vizuri?
 
Kwa hiyo Kwa Magufuli hajikufunza kitu watanzania waluvyomlilia misafara yote Tanzania bara na visiwani? Hadi watu kufa Kwa kukanyagana wakimuaga? Hilo vipi hakujifunza kitu ?
Magu alizikwa na misafara ya kulazimisha. Ruge alizikwa na watu wengi kwa ridhaa yao na sio mafuriko fake ya nguvu za dola.
 
Hao watu wengi labda wangekuwa na maana kama wangefukiwa nae kaburini, huu upuuzi wa 'Kuzikwa na watu wengi' naona umejaa sana vichwani mwa waafrika, sijui wanaona watu wakiwa wengi kwenye mazishi ndio marehemu atapokelewa salama huko aendako??!!

Kuna mtu anazikwa na watu wengi kweli kwa mguso wa watu hao. Sasa Hawa viongozi wa kiafrika wanatawala kimabavu, na wakifa wapambe wao wanalazimisha watu wawe wengi ili kuhadaa umma na Dunia kuwa walikuwa wanapendwa sana.
 
Kuzikwa na watu wengi hakufundishi lolote, kinachotakiwa ni kuangalia ni kuwa alililiwa na wangapi; au ni watu wangapi waliskitishwa na kifo chake. Mtu anaweza kuzikwa na watu wengi wasiompenda ila wanataka kuhakikisha amezikwa na hatarudi duniani tena.
 
Kwa hiyo Kwa Magufuli hajikufunza kitu watanzania waluvyomlilia misafara yote Tanzania bara na visiwani? Hadi watu kufa Kwa kukanyagana wakimuaga? Hilo vipi hakujifunza kitu ?
Kwa jpm alisema hivi "Mungu akaamua ugomvi"
 
Hao watu wengi labda wangekuwa na maana kama wangefukiwa nae kaburini, huu upuuzi wa 'Kuzikwa na watu wengi' naona umejaa sana vichwani mwa waafrika, sijui wanaona watu wakiwa wengi kwenye mazishi ndio marehemu atapokelewa salama huko aendako??!!
Hakika
 
Napinga hii dhana kuwa ukizikwa na watu wengi ndio kupendwa na wengi.

Wengi wengi wa watu wanaohudhuria misiba yao ni sababu ya nafasi zao na sio utu wao.
 
Back
Top Bottom