Nape Nauye;Hakuna Mgogoro Ccm..Paul Makonda Lowassa anakibomoa Chama, Yupi mkweli?

sokoinei

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,832
566
Ni dhahiri sasa Chama cha Mapinduzi kimekumbwa na mgogoro wa kimaslahi baina ya pande mbili zinazokinzana kuhusu Mh Lowassa kutuma baadhi ya watu kumpigia kampeni kabla ya wakati maalum wa kufanya hivyo kufika.

Ni juzi tu kiongozi wa UVCCM taifa Paul Christian Makonda alitoa tamko mbele ya waandishi wa habari akiwatuhumu baadhi ya viongozi wa dini na vijana wa mjini kwa kukubali kununuliwa na kutumika na Lowassa kuendelea kukibomoa chama.

Ni wazi ukimsikiliza Makonda ktk hotuba yake utamsikia akikiri kua Ccm kimebomoka na anachofanya mh Lowassa ni kuendelea "kubomoa" chama.

Lakini kwa upande wa Nape Nauye Katibu wa itikadi na uwenezi Ccm yeye anakataa kuwa ndani ya Ccm hakuna mpasuko wala hakuna mgogoro zaidi sana kinachotokea ni Demokrasia.

Kama hiki tunachokishuhudia sasa ni demokrasia, (Kwa maneno ya Nape) iweje leo baadhi ya viongozi km mh Malecela,,Sitta,,Sumay na Makonda kumkosoa Lowassa?

Kama ni kweli Ccm hakuna mgogoro wala hakijabomoka,iweje basi Makonda akiri mbele ya waandishi wa habari kua anachokifanya mh Lowassa ni kuendelea kukibomoa Chama?

Kwa maneno ya Makonda ya kumtuhumu Lowassa kuendelea kubomoa chama si ni wazi kuwa Ccm ilishabomoka na anachokifanya Lowassa ni maendelezo?

Je kati ya Nape Nauye na Paul Makonda nani mkweli au nani muongo????
 
Back
Top Bottom