Nape: CCM itashinda tu uchaguzi mkuu ujao hata kwa goli la mkono

EmmaGMangwela

Senior Member
May 11, 2015
139
53
Habari Jf..

Nape Nnauye Juzi akiwa Mkoani Kanda ya Ziwa aliwaambia CCM Ushindi ni Lazima hata kwa Goli la Mkono ili mradi tu Referee apulize Kipenga.

"Goli ni Goli tu Hata Kama ni la Kuotea"

Hapa Swali la Kujiuliza Je Referee wa Mechi ya CCM na UKAWA atatuvusha Salama?, Kwa Maana Team zote Zimejipanga Vilivyo na Washahabiki Safari hii Naona Hawanunuliki na Hawataki hata Jezi za BURE.

UKAWA Kazi Kwenu Sasa,Wananchi Hawatawasaidia Kulalamika na Kulialia Baada ya Mechi Kuisha Kwa Bao la Mkono wa Mungu.

CCM imesema kuwa itahakikisha inarudi Ikulu hata "kwa bao la mkono" wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25.

Katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye alisema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye viwanja vya Nyehunge wilayani hapa.

Neno "bao la mkono" hutumiwa kama goli lililofungwa kwa kuupiga mpira kwa mkono kinyume cha taratibu za mpira, lakini hukubaliwa kwa kuwa mwamuzi anakuwa hajaona kitendo hicho.

"Rangi inayoenda Ikulu ni hii (anaonyesha shati lake la kijani ambayo hutumiwa na chama hicho). Tuna uhakika na ushindi wa Rais. Kwa namna yoyote ile, CCM itarudi Ikulu hata kama ni kwa bao la mkono... bao ni bao tu ili mradi refa hajaona," alisema Nape.

Nape, aliye kwenye ziara ya katibu mkuu wa CCM, aliwataka wananchi wa Sengerema kusubiri ushindi wa chama hicho na kuwakumbusha kuwa wanapaswa kuiweka CCM kuanzia udiwani mpaka ubunge kwa nafasi ya urais tayari kuna uhakika.

Katika mkutano huo, Nape alisema ana uhakika CCM itashinda baada ya kushuhudia mwitikio wa Watanzania tangu alipoanza kuongozana na Kinana katika ziara zake za kuizunguka nchi na kuzungumza na wananchi pamoja na kusikiliza kero zao.

Amebainisha kuwa amejifunza na kujiridhisha kuwa chama chake bado kinapendwa miongoni mwa wapigakura waliofikiwa tofauti na vyama vya upinzani.

"Tumefika maeneo mengi ambayo upinzani haujafika. Huko tuna hazina kubwa ya wanachama. Hakuna namna Ukawa wanaweza kuingia Ikulu mwaka huu," alisisitiza.

Wapinzani waja juu

Kauli hiyo ya Nape ilipingwa na viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani waliosema kuwa mtendaji huyo anamaanisha kuwa CCM itaiba kura.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa hakutaka kabisa kuzungumzia kauli ya Nape zaidi ya kusema watakutana Oktoba.

"Kwa bahati mbaya kauli za Nape siwezi kuzijibu. Kauli za Nape zichukue kama zilivyo, ingekuwa ni (katibu mkuu wa CCM, Abdulraham) Kinana, ningemjibu lakini ajue kuwa tutakutana Oktoba," alisema Dk Slaa alipoulizwa na Mwananchi kuhusu suala hilo.

Naibu mkurugenzi wa habari wa CUF, Abdul Kambaya alisema kauli ya Nape inamaanisha kuwa CCM itaiba kura kwani kwa kawaida bao la mkono ni bao haramu.

"Kauli hiyo inaonyesha dhahiri kuwa wataiba kura na kwa sababu katiba yetu ni mbovu matokeo yake yatatangazwa kama yalivyo… hiyo ndiyo maana ya bao la mkono," alisema.

Kambaya alisema hata hivyo CCM isijiaminishe kwa lolote kwani hivi sasa wananchi wamebadilika kimtazamo kutokana na matatizo mengi yanayoiandama nchi kama vile afya, elimu duni na migogoro ya ardhi.

"Lakini CCM wajue kuwa kutatokea machafuko makubwa iwapo wamejipanga kuingia Ikulu kwa njia hiyo ya bao la mkono. Kauli ya Nape ni ya kidikteta na inaonyesha dhahiri kuwa wamejikita kwenye utawala wa mabavu," alisema.

Kadhalika Kambaya alisema CUF imeshajipanga na kuhakikisha inaziba mianya yoyote ya wizi wa kura kuanzia kwenye Daftari la Wapigakura hadi katika ujanja wa kuwapigisha kura marehemu, askari na wanajeshi kama inavyodaiwa kufanyika Zanzibar.

Katibu mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema Nape anatoa maneno ya kuvutia kwake kama njia ya kuwakatisha tamaa wapinzani na wanachama, hata hivyo alimuonya kuwa siasa za sasa hazitabiriki kwa njia hiyo.

"Lakini ajue kuwa mambo yanabadilika. Anaweza kushangaa mambo yakawa mengine, sasa hivi wananchi wana mwamko mkubwa na wanabadilika," alisema.

Alisema CCM haina haja ya kujitapa kwa sasa wakati bado haijapata mgombea kwani huenda wakapata ambaye wananchi hawatamuunga mkono hata kidogo.

"Bado CCM wana makundi jambo ambalo kwao ni udhaifu. Lakini pia lazima wajue kuwa wakati wa mchujo utakapofika, wale watakaokatwa hawatafurahia kuachwa na hapo kuna sababu za wapinzani kushinda,"alisema.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema wakati Nape anabishana kwenye majukwaa, NCCR inaendelea kupiga kazi.

"Badala ya kujadili hoja za msingi zenye manufaa kwa wananchi yeye anajadili CCM kupiga bao?" alihoji Mbatia.

Akijibu hoja ya Nape, Naibu Katibu Mkuu wa TLP, Nancy Mrikaria alisema kauli ya kada huyo imekaa kisiasa na si kiuhalisia kwani ni kawaida kwa chama cha siasa kujiaminisha kuwa kitashika dola.

"Unajua chama chochote hata kiwe kidogo lazima kikiri kuwa kitashika dola ili mradi ilani yao inakubalika na unakubaliwa na wananchi kwa sababu chama chochote nia yake ni kuingia ikulu," alisema.

Alisema hata vyama vidogo kama TLP hukiri ushindi kwa kusema kuwa vinataka kuingia ikulu kwa sababu chama hakiwezi kukiri mbele ya wananchi kuwa hakitashinda.


Chanzo: Mwananchi
 
DSC09752.jpg
 
Hizi kauli za Nape ni mbaya sana , mbaya zaidi kwenye Chama chake hakuna anayemkanusha. Zitakuja kuleta machafuko.

Kwa kauli hizi hata kama upinzani utashindwa Oktoba . Hata kama watashindwa kihalali sidhani kama watakubali.

Aina hii ya viongozi kama Nape sijui huwa wanafikiria nini.

Nafikiri Nape ni katibu mwenezi wa hovyo kuwahi kutokea kwenye CCM.
 
Hiyo kauli anairudia mara kwa mara, tume ya uchaguzi nayo imekaa kimya.
 
Nawashauri UKAWA hiyo kauli waitunze ipasvyo ili wakati wa kusubiri matokeo rafu ya aina yeyote ikichezwa likumbukwe hili NENO!!
 
Kama kweli amesema hivyo ccm wamekwisha kuingiwa na hofu kwani wameona wanaojiandikisha kupiga kura wengi ni vijana waliopigika na wanaotaka mabadiliko. Hivyo tume ikichakachua kura au ikichelewesha kutangaza matokeo PATACHIMBIKA!
 
Mlitaka aseme vipi ilihali yeye yupo katika upande wa propaganda...mnajua kauli za kuleta machafuko zaidi ya" nchi hatatawalika"
 
upinzani wanatakiwa kwenye kampeni zao wakumbushie hili neno ili nguvu ya UMA walinde kura zao hakuna kulala ck hiyo :na huyo Nape akiendelea na hizo kaulu ajiandae kuwa mteja wa Bensouda .
 
Kwa sheria za football ukitumia mkono ni faulo inaweza sababisha penati au free kick na uliyetumia mkono unaweza pata kadi ya njano au kadi nyekundu. Labda refa apendelee upande mmoja
 
Nape ni kiongozi wa hovyo kuwahi kutokea Tanzania...

Anafanya siasa za kijima sana..

Sijui elimu aliyo nayo imemsaidiaje?
 
Back
Top Bottom