Nape awapokea wanachama wapya CHUO Kikuu cha Tumaini Kampasi ya SMMUCO - HIMO (Moshi)

Albano

Member
Jul 21, 2009
41
10
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM ndugu Nape Nnauye amewapokea wanachama Wapya wa CCM Tawi la SMMUCO Tawi la Tumaini HIMO.

Jumla ya wanachama Wapya 193 wamejiunga na CCM na wamefungua Tawi lao rasmi leo.

Pia RAIS WA serikali ya wanafunzi wa CHUO hicho ndugu Paul K. Laurent amejiunga na CCM. Mchana kutakuwa na Mkutano MKUBWA wa Hadhara Moshi Mjini katika viwanja vya Polisi mkutano unaosubiriwa kwa hamu sana.

HUU utakuwa mkutano wa kwanza kwa Nape kuhutubia katika mkoa WA Kilimanjaro toka ateuliwe kuwa KATIBU WA Itikadi na Uenezi wa CCM.
 
Si aliwatukana watu wa Moshi huyu?? Aliwaita wabaguzi na ndiyo wenye Chadema. Au wachaga wamesahau nini??
 
je wanajiunga na ccm kwa maslahi au kwa sababu ya Nape inabidi kujiuliza hilo swali ndo muhimu sana..
 
SMMUCO wana campus Moshi mjini (Zamani kiwanda cha Kibo), Mwika, na ofisi kuu ziko Kibosho. Hiyo campus ya Himo wamefungua lini? (Manake mpaka leo asubuhi haikuwepo kwenye orodha!)

Sasa, kama hilo tu dogo limekutatanisha, je hizo tarakimu unazozijua wewe na Nape itakuwaje?
 
CCM ni taasisi kubwa sana inautaratibu WA kuwa na matawi kamili katika taasisi ya Elimu ya Juu. So hao wameingia kwa maslahi ya Chama chao na siyo mtu.
 
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM ndugu Nape Nnauye amewapokea wanachama Wapya wa CCM Tawi la SMMUCO Tawi la Tumaini HIMO. Jumla ya wanachama Wapya 193 wamejiunga na CCM na wamefungua Tawi lao rasmi leo. Pia RAIS WA serikali ya wanafunzi wa CHUO hicho ndugu Paul K. Laurent amejiunga na CCM. Mchana kutakuwa na Mkutano MKUBWA wa Hadhara Moshi Mjini katika viwanja vya Polisi mkutano unaosubiriwa kwa hamu sana. HUU utakuwa mkutano wa kwanza kwa Nape kuhutubia katika mkoa WA Kilimanjaro toka ateuliwe kuwa KATIBU WA Itikadi na Uenezi wa CCM.
Hao wanafunzi watakuwa wamedanganywa kupewa ukatibu wa matawi ya Magamba wakimaliza chuo. Waulizie wenzao wa UDOM walidanganywa wakatoa na hela kumchukulia fomu JK na baada ya ushindi wa JK wakapigwa marungu na mabomu na Polisi wa CCm, ndo ije hao na hicho chuo chao cha Kata ya Himo. Sisi yetu macho tu, ila Nape hana hoja za kuweza kuzungumza na wanafunzi wa Campus yoyote kwa kuwa yeye Nape kasomea ngumbalu.
 
Jamani walivyopiga marufuku Siasa vyuoni walikuwa wanamaanisha nini! Au vyama vya Upinzani pekee ndivyo havipaswi kufanya siasa vyuoni!

Wachaga wanachoangalia Nape amekuja na nini mkononi! na si mdomoni. Kwa leo anaweza kuwapata hata wachaga wote, so long as anamwaga za GST Account vinginevyo hampati mtu.
 
Hao wanafunzi watakuwa wamedanganywa kupewa ukatibu wa matawi ya Magamba wakimaliza chuo. Waulizie wenzao wa UDOM walidanganywa wakatoa na hela kumchukulia fomu JK na baada ya ushindi wa JK wakapigwa marungu na mabomu na Polisi wa CCm, ndo ije hao na hicho chuo chao cha Kata ya Himo. Sisi yetu macho tu, ila Nape hana hoja za kuweza kuzungumza na wanafunzi wa Campus yoyote kwa kuwa yeye Nape kasomea ngumbalu.

Kwanza wanafunzi wa Himo hawawezi kuwa makritiko, ni rahisi kwao kurubuniwa, pia hiyo namba ya 193 new members, ni ndogo sana, CDM huwa wanafagia, ndo maana ccm hawapendi wafanye mihadhara, utasikia waliojiunga 2845, mara 1909 n.k..

Kweli nape kilaza hawezi ongea campus zenye kritiko akasikilizwa, si unakumbuka hata kwenye mjadala ya nafasi ya vijana katika Taifa (TBC-waliirusha), alikuwa anauma uma maneno, lugha kongana, kiingereza no).

Mimi kuna chuo nasoma Masterz na Nape, cjawahi kumwona darasani, na tupo full time, ila kwenye exams namwona.. Tumekubalia akipata hata alama"C", TUNAANDAMANA! uwezo wake kitaaluma tunaujua!

Moshi mfukuzeni huyo, alishawakosea adabu
 
Nina mashaka na ukweli wa habari hii. Idadi ya wanafunzi wanaodaiwa "kujiunga na CCM" hailingani na idadi halisi ya wanafunzi wa campus moja moja (ambazo hata hivyo hazipo kwenye orodha). Labda ili tuchambue ukweli wa habari hii, tuambiwe, tukio hilo lilitokea campus ipi, na saa ngapi ndipo tuendelee.
 
Mimi kuna chuo nasoma Masterz na Nape, cjawahi kumwona darasani, na tupo full time, ila kwenye exams namwona.. Tumekubalia akipata hata alama"C", TUNAANDAMANA! uwezo wake kitaaluma tunaujua!

Moshi mfukuzeni huyo, alishawakosea adabu
kumbe anasoma masters?ni chuo gani hicho!
 
Kampasi ya Himo ni ipi hiyo?

Idara ya Uenezi yenye taarifa mbovu namna hii...
 
Huyu aliyekuwa Rais wa campus ya Mwika Paul Laurent, ni kati ya wanafunzi 68 wa BED mwaka wa tatu wanaotarajia kumaliza chuo siku chache zijazo. Nadhani anatafuta "mradi" wake kwa mlango wa CCM.

Kwa mtu ambaye serikali yake haikuisha tuhuma za ubadhirifu, si ajabu sana kusikia amejiunga na CCM.

Hata hivyo, mbona idadi ya wanaodaiwa kujiunga CCM haiwiani na idadi ya wanafunzi wote wa campus ya Mwika? Walifikaje himo kuhudhuria mkutano huo (mbali kabisa na chuo chao kilichopo Mwika)? Walisafirishwa? Ufafanuzi unahitajika zaidi
 
Jamani walivyopiga marufuku Siasa vyuoni walikuwa wanamaanisha nini! Au vyama vya Upinzani pekee ndivyo havipaswi kufanya siasa vyuoni!Wachaga wanachoangalia Nape amekuja na nini mkononi! na si mdomoni. Kwa leo anaweza kuwapata hata wachaga wote, so long as anamwaga za GST Account vinginevyo hampati mtu.
Safi sana Said, Nape upo?
 
Hao wanafunzi watakuwa wamedanganywa kupewa ukatibu wa matawi ya Magamba wakimaliza chuo. Waulizie wenzao wa UDOM walidanganywa wakatoa na hela kumchukulia fomu JK na baada ya ushindi wa JK wakapigwa marungu na mabomu na Polisi wa CCm, ndo ije hao na hicho chuo chao cha Kata ya Himo. Sisi yetu macho tu, ila Nape hana hoja za kuweza kuzungumza na wanafunzi wa Campus yoyote kwa kuwa yeye Nape kasomea ngumbalu.
UDSM mbna haendi?
 
Kweli nchi yetu haina wasomi, bali kufka chuo kikuu ni ulazma wa mfumo wa elimu. Hakika siamini wasomi wa chuo kikuu kurubuniwa na Nape, kama ni umaskini ni heri nif e nao.
 
Huyu aliyekuwa Rais wa campus ya Mwika Paul Laurent, ni kati ya wanafunzi 68 wa BED mwaka wa tatu wanaotarajia kumaliza chuo siku chache zijazo. Nadhani anatafuta "mradi" wake kwa mlango wa CCM.

Kwa mtu ambaye serikali yake haikuisha tuhuma za ubadhirifu, si ajabu sana kusikia amejiunga na CCM.

Hata hivyo, mbona idadi ya wanaodaiwa kujiunga CCM haiwiani na idadi ya wanafunzi wote wa campus ya Mwika? Walifikaje himo kuhudhuria mkutano huo (mbali kabisa na chuo chao kilichopo Mwika)? Walisafirishwa? Ufafanuzi unahitajika zaidi

Nilishasema wenye taaluma za mashaka usalama wao kisiasa na kimaisha upo CCM. Angeenda kufanyia mkutano Uwanja wa Mashujaa Moshi au Pasua ama Njoro kama angeshuka jukwaani akiwa Mzima.
 
3.+Nape+akimkabidhi+kadi+ya+CCM+Simon+Ndemela+wanachama+wapya+108+wa+CCM+kutoka+SIMCO+walipojpeawa+kadi.JPG

KATIBU wa NEC, Itikati na Uenezi Nape Nnauye akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Silo Swai katika mapokezi yaliyofanyika Chekereni mkoani humo. Kushoto ni Katibu wa mkoa Stephen Kazidi

4Nape+akipokea+saluti+kutoka+kwa+kijana+wa+CCM+wakati+wa+mapokezi+eneo+la+Chekereni%2C+Vunjo+mkoani+Kilimanjaro.+Wengine+ni+Mwenkeiti+wa+CCM+mkoa+wa+Kili%2C+Silo+Swai+na+Katibu+wa+mkoa+steven+Kazidi.JPG

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipokea saluti kutoka kwa kijana wa CCM wakati wa mapokezi ya msafara wake, eneo la Chekereni, Vunjo mkoani Kilimanjaro. Wengine ni Mwenkeiti wa CCM mkoa wa Kili, Silo Swai na Katibu wa mkoa steven Kazidi
5.+Vicky+Nsilo+Swai+mkt+ccm+mkoa+kilimanjaro%2C+Mijo+Laizer+mkt+tawi+la+SIMCO+na+steven+Kaidi+Katb+CCM+Kili.JPG

Katibu wa NEC CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza baada ya kuzindua tawi la wanachama wa CCM la wasomi wa Chuo Kikuu cha Tumaini (SIMCO), katika mkutano uliofanyika katika mji mdogo wa Himo mkoani Kilimanjaro, jana. Wengine kutoka kushoto, wapili ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Vicky Nsilo Swaijaro na kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kaidi na Mwenyekiti wa Tawi hilo Mijo Laizer
6.+Wanachama+wapya+wa+CCM+tawi+la+SIMCO+wakila+kiapo+baada+ya+kupewa+kadi+na+Nape+mjini+Himo%2C+jumla+ya+wanachama+108+ktoka+chuo+hicho+walikabidhiwa+kadi.JPG

Wanachama wapya wa CCM tawi la SIMCO wakila kiapo baada ya kupewa kadi na Nape mjini Himo, jumla ya wanachama 108 ktoka chuo hicho walikabidhiwa kadi
1.+Baadhi+ya+wanafunzi+wa+SIMCO+wakiwa+kwenye+mkutano+na+Nape+mjini+HIMO%2C+wapili+kulia+ni+Rais+wa+SIMCO+Paul+Raurent.JPG

Baadhi ya wanafunzi wa SIMCO wakiwa kwenye mkutano na Nape mjini HIMO, wapili kulia ni Rais wa SIMCO Paul Raurent
2.+Nape+akilakiwa+na+Mwenyekiti+wa+CCM+mkoa+wa+Kilimanjaro+Silo+swai+katika+mapokezi+yaliyofanyika+Chekereni+mkoani+humo.+Kushoto+ni+Katibu+wa+mkoa.JPG

Nape akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Silo swai katika mapokezi yaliyofanyika Chekereni mkoani humo. Kushoto ni Katibu wa mkoa

CHANZO: ZIARA YA NAPE MOSHI MKOANI KILIMANJARO
 
Back
Top Bottom