Nape: 78% ya Watanzania wanasikiliza Redio tofauti na mitandao ambayo Watumiaji ni 10% tu. Mitandaoni kuna mambo Mengi yasiyofaa, tumia Redio

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,803
143,273
Waziri wa Habari Nape Nnauye amewapongeza Upendo Media kwa Kazi Nzuri wanayoifanya kuchochea Maendeleo nchini.

Nape amesema Watanzania 78% Wanatumia Redio na waliobaki ndio wako kwenye TV na Mitandao ya Kijamii.

Nape amesema mitandao ya Kijamii ina mambo Mengi yasiyofaa hivyo Wazazi tuwazoeshe Watoto wetu kutumia Redio FM badala ya mitandao.

Upendo Redio FM Inaponya, amesisitiza Mhe. Nape.

Source: Upendo TV
 
Waziri wa Habari Nape Nauye amewapongeza Upendo Media kwa Kazi Nzuri wanayoifanya kuchochea Maendeleo nchini

Nape amesema Watanzania 78% Wanatumia Radio na waliobaki ndio wako kwenye TV na Mitandao ya Kijamii

Nape amesema mitandao ya Kijamii ina mambo Mengi yasiyofaa hivyo Wazazi tuwazoeshe Watoto wetu kutumia Radio FM badala ya mitandao

Upendo Radio FM Inaponya, amesisitiza mh Nape

Source: Upendo TV
Radio zipi? hizi FM zenye watangazaji weupe mno vichwani? Radio zina vipindi vya mipasho masaa yote? Zamani yes nilikuwa nasikiliza ila now day labda nikutane nayo sehemu wanasikiliza mdio nisikilize
 
Radio zipi? hizi FM zenye watangazaji weupe mno vichwani? Radio zina vipindi vya mipasho masaa yote? Zamani yes nilikuwa nasikiliza ila now day labda nikutane nayo sehemu wanasikiliza mdio nisikilize
Radio ya Kijiji 😂😂😂
 
Waziri wa Habari Nape Nauye amewapongeza Upendo Media kwa Kazi Nzuri wanayoifanya kuchochea Maendeleo nchini

Nape amesema Watanzania 78% Wanatumia Radio na waliobaki ndio wako kwenye TV na Mitandao ya Kijamii

Nape amesema mitandao ya Kijamii ina mambo Mengi yasiyofaa hivyo Wazazi tuwazoeshe Watoto wetu kutumia Radio FM badala ya mitandao

Upendo Radio FM Inaponya, amesisitiza mh Nape

Source: Upendo TV

Mwambie Nape kuwa hizo redio zipo mitandaoni pia...
 
Mtu mmojawapo VIAZI anayepatikana ndani ya SISIEMU.

Nadhani ameshapitiliza kwenye rangi zao, pengine kwa sasa rangi za upinde zitampendeza zaidi.
 
Nape amesema Watanzania 78% Wanatumia Redio na waliobaki ndio wako kwenye TV na Mitandao ya Kijamii.

Nape amesema mitandao ya Kijamii ina mambo Mengi yasiyofaa hivyo Wazazi tuwazoeshe Watoto wetu kutumia Redio FM badala ya mitandao.
Akienda kwenye TV atasema 78% wanattazama TV, kama alivyosema kwenye mitandao kabla hajjaenda kwenye redio
Mwaka jama alisema "..watanzania wa sasa wanatumia zaidi mitandao kuliko media nyingine yoyote, hivyo anawashauri wahamie kwenye internet maana mitandao ina mamboo yasiyofaa"
 
Si kweli, tulikuwa wengi wetu twatumia mitandao hii ya kijamii, hatuzitaki hizo radio zao kwa sababu: radio zote zinafuata matakwa ya Serikali na chama chao. Ukweli hizo radio hazitufai kabisa.
Ni kweli, Watanzania walio wengi wanasikiliza radio kuliko mitandao. Watanzania wengi hawapo mijini, wapo vijijini.
 
Ni vigumu sana mtu kusikiliza radio maana zimebanwa sana hazina uhuru wa habari hasa TBC na hata radio nyingine watu wamehamia kwenye mitandao
 
Back
Top Bottom