Naona kama Nape anaelekea muelekeo mbaya

Kuhusu kutofautiana kimawazo ndani ya chama na ukabaki salama nadhani ccm wana nafuu kuliko chadema - sote bado tunakumbuka kilichowatokea akina zito, prof kitila na mwigamba!
Kuna tofautiana mawazo na kuna kupandikiza mamluki kajifunze hivi vitu viwili halafu urudi hapa
 
Nape hajatambua kwamba the simplest ways to stay happy, is just let go of the things that makes you sad.
nakubaliana na wewe mkuu na nawashangaa wanaoshindwa kumuelewa mleta mada!

binafsi namheshimu sana nape na nilisikitika sana sana sana kwa jinsi alivyotolewa kikaraha huku mwenzie akipeta....tena kwa kusifiwa vizuri na mkuu wa kaya.

lakini kwa jinsi anavyoenda sasa, kusemasema (kuponda) kila wakati huku akinukuliwa akisema ana imani na magufuli (hususani wakati anakabidhi ofisi), inamharibia. ukweli utabaki palepale kuwa kwa sasa hawezi hata kidogo kupambana na magufuli kwa vyovyote vile.....yupo madarakani, tena hata nusu ya muhula wake wa kwanza hajamaliza, anao uwezo wa kupanga system ambayo inaweza kumnyamazisha nape milele hata baada ya kuondoka....wapo wapendwa kina makonda.

wapo wanaomsifu na kusema eti amepata akili, hawa wanafanya hivi kwa makusudi....wanajua nape yuko vizuri hivyo wanamtamani ktk timu yao....lakini pia ni furaha yao kuona jirani anafukiwa na moshi, hivyo wapo ktk kuchochea ili wapate burudani hiyo!

ayaache hayo yapite, km ulivyoshauri mkuu. apige kazi kwa kuongea na watu wake vitu vinavyofanya kazi km nini kinajiri ktk bei ya korosho n.k. watu wa mtama walishaanza kutulia juu yake kutokana na mambo makubwa aliyowafanyia kwa muda mfupi aliokaa....upanuzi mkubwa kabisa wa barabara toka mtama hadi chiuta, madingo, mnyambe kuelekea tandahimba; kutoka nyangao kwenda namupa n.k. yalikuwa hayajaonekana haya tangu upatikane uhuru. kwakuwa aliendelea kuyafanya haya hata baada ya kuvuliwa uwaziri basi naamini bado ana nafasi nzuri tu ya kujijenga kihalali.

ingekuwa maisha yake ya kisiasa aliyaanza kama bashe, basi hata asingekuwa kwenye kuwindwa kokote kule....lkn kwakuwa hayakuwa hivyo basi atashangaa pale bashe anabaki na yeye anapotezwa kwa kila hila.......atulie apige kazi.

kama jacob zuma alitimuliwa na mbeki na leo hii ndiye raisi wa afrika kusini basi inawezekana tu naye akapanda chati zaidi siku moja kwa uwezo wa mungu.......kufukuzwa tu, ingekuaje km angefungwa kabisa!!!!!
 
Ni upuuzi na ufinyu wa kifikra kwa mtu aliyefikia hadi ngazi ya uwaziri kulalamikia ununuzi wa ndege ktk nchi ambayo haikuwa na ndege hata moja! Hata kabla ya huo ununuzi wa ndege hiyo matatizo ya wananchi ktk jimbo lake yalikuwepo (tena akiwa waziri).
Kama mbunge inaonekana hana msaada zaidi kwa wananchi hao, hivyo kuleta visingizio vya kijima na kupeleka lawama kwingine. Asaidie kutatua matatizo yanayowakabiri wananchi jimboni badala ya kulaumu ununuzi wa ndege kwa kudhani ndo suluhisho!
 
Ni kwa sababu ayupo tena mezani kula. Na hii utajua tabia ya MTU alivyo. Alipokuwa waziri duuu.... Kila kitu alisifia. Anajisahau kuwa maamuzi mengine yalipitishwa Na yeye mwenyewe alipokuwa kwenye baraza la mawaziri. Has a kuhusu Ndege.
 
Kwanza kabisa sina hulka ya kutakakumtetea mtu au kumuonea mtu, sipendi kumjadili mtu kama mtu tu, napenda kujadili dhana.

Kwa hiyo nitajadili hili la Nape kwa dhana, kanuni na kawaida.

Kwa mtu anayejua kanuni za "collective responsibility" atajua kwamba mbunge akiwa Waziri anafungwa na kanuni hizi kuisema serikali vibaya, kwa kuwa yeye ni sehemu ya serikali na maadam yupo katika serikali, anatakiwa kuitetea serikali, au akiona hawezi kuitetea serikali, aishawishi ibadili mambo katika vikao vya ndani, au akishindwa kujenga ushawishi, anyamaze, au akiona hawezi kunyamaza, atoke nje ya serikali na kuisema serikali akiwa mbunge wa kawaida, Waingereza wanaita mbunge huyu wa kawaida asiye na cheo serikalini "backbencher", kwa kuwa hakai viti vya mbele katika "House of Commons", as opposed to "frontbenchers", Ministers and leaders of the opposition/ shadow ministers.

Sasa Nape leo si Waziri. Si sehemu ya serikali, kwa maana ya si Waziri. Haiwakilishi serikali. Ana jukumu la kuwawakilisha wananchi, hafungwi na kanuni ya "collective responsibility" ana uhuru wa kuikosoa serikali kama "backbencher".

Sasa kwa nini mbunge "backbencher" ambaye hafungwi na "collective responsibility" kuikosoa serikali, akitaka kutumia haki yake ya ubunge kama backbencher watu wanamsema kwamba anasema hivyo kwa sababu ya kijiba cha kukosa uwaziri?

Hivi watu wanaelewa kwamba mawaziri wanataka kusema mengi sana kuisema serikali vibaya, lakini wanafungwa na kanuni za kazi, hawatakiwi kuisema serikali vibaya mpaka waondoke kwenye uwaziri?
 
Kuna tofautiana mawazo na kuna kupandikiza mamluki kajifunze hivi vitu viwili halafu urudi hapa
Nyinyi ni wapuuz. Huko kwenu mtu akiwa tofaut na mawazo ya chairman mnasema msaliti au mamluki,ila huku ccm mnasema anajitambua mara mwenyekiti hapendi kupingwa.
 
nape bwana anakwambia wakizengua tu mara paap hiiiiiihi! ni zaidi ya caption so ccm kuweni makini mtamkosa muda si mrefu aje kutupa tafu bao la mkono m4c
nape.JPG
 
Unajua ule msemo wa samaki alie funga mdomo hashikwi na ndowano sasa unakuwa kweli kwa huyu mstaafu mwenezi.

Kiukweli kabisa Nnape anakoelekea na post zake twitter zinafanya ajulikane sio leader na uwenda anakuwa mganga njaa mbaya zaidi wale walio mpa heshima yakuwa kiongozi mkubwa wa chama wanasikitika kile wanakiona kwake wakijuwa huwezi kuwa muwasi ukawa mwanachama wa kweli wa CCM.

Nnape anafanya viongoz wajuu wachama kumuona sio wana CCM
Nape yupo ICU kisiasa! Anataka pambana na dola .angekuwa makini angefunga mdomo wake na kuwa bize ktk ibada na matendo mema,uwenda angekumbukwa katika ufalme huu! Anachofanya sasa akitomsaidia kisiasa wala kiuchumi....hii nchi watu waliigeuza kuwa shamba la bibi!!. Nape ana wakumbatia hao na bado anahamini kuwa hao madhurumati anaowaamini yeye watakuja chukua nchi wampe uwaziri! YUPO MUNGU NA AJALALA NA WALA ALALI! MAFISADI NA VIBARAKA WAO WAJUE HILO!rais anachaguliwa na Mungu! Nape anatakiwa awe mpole ajipime na arudi ktk falsafa na katiba ya chama.nje ya hapo ni msaliti tu kama yuda iskariote
 
Malipo mengine ni hapa duniani,hakuzoea kuwa nje ya tawala kuu,atazoe na kujifunza kuheshimu watu.
Kwani bila siasa hakuna maisha?
 
Back
Top Bottom