Naona ipo siku nitaiacha hii kazi ya ualimu ni wakati Sasa wa Kutengeneza mifumo

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,465
4,675
Fikiria hupo chama Cha chakuhawata alafu inatokea tu chama kingine (CWT) wanapitisha makato yako na umeshajitoa, Unaenda kwa afsa utumishi ( Hapo umeshamtafuta mwezi mzima hayupo ofsini) anakujibu short tu kwa dharau kwamba nenda huko CWT wakuandikie kwamba wewe sio Mwanachama wao uniletee hapa nikutoe, anasema hivyo anajua fika wewe kwenda CWT sio jukumu lako maana huo ni mshahara wako sio wa CWT na anajua fika kwamba CWT hawawezi kukusaidia kitu, unaenda huko CWT hawakupi ushiriakiano wowote, unarudi kwa afsa utumishi anakujibu Sasa "Mimi nifanyaje/nikusaidiaje?"

Unarudi shuleni na mawazo. Nafundisha physics na Mathematics form one mpaka form four, nitapata morale ya kufanya kazi? Itoke wapi? Mimi ni mtaaluma majukumu ya kitaaluma nitayatimizaje huku nikiwa na mawazo?

Dharau! Dharau! Dharau sio kitu kizuri, ukimletea mtu dharau sehemu ambayo anaona ni haki yake basi jiandae kuchukua matokeo ya dharau. Huyo Afsa utumishi anadharau kwa sababu Sina power,Sina hela na Sina heshima ndio ni ukweli, Ukiwa maskini lazima udharililike tu. Mshahara wa kwangu Mimi ndio na mamlaka nijiunge chama a au b, mtu anakataa kukuondoa kwa faida gani? Yeye anafaidika kwa lipi mtumishi kukatwa vyama viwili?

Walimu wanapambana sana kazi wanazozifanya ni nyingi mnoo, hawana allowance zozote, wanakaa Shule mpaka saa 11:30 jioni kwa malipo ya elfu 3-6 (remidial) yote ni kwa ajili ya kutimiza majukumu yao, ni sawa hatuna shida na hizo allowance tumeshakubali, Lakini? Wapeni malimbikizo yao ya mishahara (mshahara wangu wa kwanza sijawahi kulipwa Hadi Leo), Wapande madaraja kwa wakati, wakienda huko halmashauri/manispaa na matatizo yao wajibiwe kwa staha na ustaarabu maana huko halmashauri ndio sehemu pekee ya kutatuliwa changamoto, Lakini ajabu ni kwamba walio kwenye position ya kukusaidia hawakusaidii (hawaoni umuhimu wa kukusaidia) kumbuka hata hao Ma-afsa utumishi walikua walimu kabla wakaenda kujiendeleza.

Nimegundua huku ni changamoto kwakweli na Sioni kama nitakuepo kwa muda huku, hiki kijiti nitawaachia wengine wakikimbize na kulijenga taifa. Lakini WAJUE walimu wote sio fairule, tulifaulu vizuri form six tumezaliwa kwenye umaskini mkubwa sana tumekimbilia huku atleast tuanze kujitegemea mapema. Sasa ni wakati wa kuandaa mifumo kwa hasira kubwa na umakini mkubwa hata hiyo siku ikifika isiwe majuto bali ni ushindi.
 
Fikiria hupo chama Cha chakuhawata alafu inatokea tu chama kingine (CWT) wanapitisha makato yako na umeshajitoa, Unaenda kwa afsa utumishi ( Hapo umeshamtafuta mwezi mzima hayupo ofsini) anakujibu short tu kwa dharau kwamba
Vyama vya wafanyakazi wanashirikiana na serikali KUIBA mishahara ya watumishi.


Na sheria inawapa nguvu hiyo.


CWT wanakula na Wakurugenzi, Maafisa utumishi na DHRO ndio maana watafanya kila namna kuhakikisha wanainguza Makato kwenye Mshahara wako.

Ushauri wangu, Kama unataka kupambana piga simu utumishi umuwashe huyo afisa utumishi, usiogope mtu.

Au omba kukutana na DED umchane LIVE
 
We unataka kuacha kazi kwa hasira? Utatoka apo utaenda kujinyonga bure maana mawazo mengi yatakujaa, utaanza kuwategemea watu na kuona ni wabaya,

Sikia Hiko kidgo unachokipata Kuna watu hawana kbsaa, na Kuna wengine wanapata kama wewe na Bado wanafurahia maisha,
Life is not always sweet, Kuna vingine vichungu hata kama ungekua mbunge au rais , shubiri ipo,
We si unasema huna kazi Kuna mwl wa s/m haja ajiriwa 6yr now,

Hapa ni Tz sio ULAYA Wala sio mbinguni
so dance according to the beat , wakipigia lege cheza lege wakiweka buzuki pita nalo,

Makasiliko hayajawahi muacha mtu salama kila sector Ina udhaifu ,

Acha kazi kama umeanzisha shule yako au ushajitengenezea sehem for the purpose to employee your self lakin sio kwa hasira hizo hutavuna kitu,
 
We unataka kuacha kazi kwa hasira? Utatoka apo utaenda kujinyonga bure maana mawazo mengi yatakujaa, utaanza kuwategemea watu na kuona ni wabaya,

Sikia Hiko kidgo unachokipata Kuna watu hawana kbsaa, na Kuna wengine wanapata kama wewe na Bado wanafurahia maisha,
Life is not always sweet, Kuna vingine vichungu hata kama ungekua mbunge au rais , shubiri ipo,
We si unasema huna kazi Kuna mwl wa s/m haja ajiriwa 6yr now,

Hapa ni Tz sio ULAYA Wala sio mbinguni
so dance according to the beat , wakipigia lege cheza lege wakiweka buzuki pita nalo,

Makasiliko hayajawahi muacha mtu salama kila sector Ina udhaifu ,

Acha kazi kama umeanzisha shule yako au ushajitengenezea sehem for the purpose to employee your self lakin sio kwa hasira hizo hutavuna kitu,
Ushauri mzurii sana huu📌📌.
 
Prakatatumba abaabaabaa sikia nikwambie. Tangu nizaliwe sijawahi ona mwalimu anafukuzwa kazi na nimesoma shule za serikali. Wakikusumbua punguza muda wa kujitolea fanya kazi kisheria muda mwingine fanya mambo yako. Usijichanganye kukasirika kuacha kazi na huna plan nyingine.
Wewe jipange ukae mguu nje mguu ndani, kwenye hiyo process utapigwa barua za onyo na kukalishwa kwenye vikao ila hakikisha uhami. It's possible wasikunyonye kisa mnyonge
 
Hawa Ma Afisa utumishi ni watu wapuuzi kupata kutokea katika nchi hii!
Yaani kati ya watu wanyonyaji bongo hapa ni Hawa mafisa waajiri, wanajiona wao ndio wafalme, hata ukiwa na mdai yako wanataka uwaabudu ndio akupe.... Nawambia Maafisa Waajiri, laana ya malalamiko ya wajiriwa mjue itawala na vizazi vyetu... Kule tuI hela za watu, ila mjue Kuna maisha baada ya kuachia kiti... Wanenu watakula zabibu chungu mliowachumia😳😳
 
Back
Top Bottom