Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 19,095
- 22,855
Usijali yeye anayo pesa ya matumizi yenu, kama umekwisha chumbiwa inekula kwako kumbuka chuoni alikuahidi atakuoa ukakubali.Ndugu zangu naombeni mnishauri katika hili, nimemaliza chuo bado issue ya ajira nimepanga kachumba kamoja ndo najitafuta hapa kimaisha nabangaiza bangaiza.
Nina rafiki yangu tokea chuoni huko wote tunaishi humuhumu Dar sasa alinambia atakuja maeneo ninayoishi. Huwa anakuja mara kwa mara kutembea huku ila huwa halali yeye anakaa kwa mjomba wake huko
Sasa aliniuliza kama nitakua geto siku ya jana nikamuambia sitokuwepo maana nlikua kwenye mihangaiko yangu leo akanipigia asubuhi akanambia kama nitakuwepo nikamuambia kuwa nitakuwepo basi akasema atapita anisalimie nikamwambia haina noma atanikuta
Ghafla mtu kaja na mabegi akayaweka akasema kuna mahali anaenda mara moja kupeleka mafile fulani hivi, akaenda akarudi ndo akanambia haelewani na mjomba wake leo ameamua kuondoka ili akaanze maisha so ndo kaja kwangu na haijulikani ataondoka lini?
Kilichonishangaza kwanini hakunambia mapema? Mimi maisha bado sana, pia hana kazi wala mishe yoyote, na kanishtukiza kabisa kiukweli binafsi nishaurini nifanyeje maana siwezi kuishi na mtu kabisa kwasasa maana ndo naanza maisha na mimi ni muhanga niliwahi kusapriziwa na rafiki hivyo hivyo akasema anakaa wiki ila akakaaa miezi 3 na hakuna rangi sikuiona
Naombeni ushauri maana akili yangu ni kama haipo sawa nina matatizo kibao kwasasa na nina mizigo mingi ya kimaisha yangu bado ni magumu mno sina ajira nabangaizabangaiza tu
MWENDELEZO:Mimi ni muhanga wa kukaribisha marafiki,nilishawahi mkubalia rafiki yangu akaishi na mimi hakuna rangi sikuiona ndo maana toka kipindi hicho sipendi kuishi kabisa na marafiki napambana tu mwenyewe