Naomba ushauri

ndamally

Member
Sep 16, 2014
11
1
Habari waungwana,

Wadau Mimi ni masikini ila kwa kipindi hiki nimebahatika kupata tzs 4,000,000 natamani sana niizalishe sijui niizalisheje naomba ushauri wenu nifanyeje?

Natanguliza shukraan
 
Usitumie hata shilingi subiri wataalam waje wakufahamishe biashara ya kufanya
 
Nitumie kwenye m pesa nikufundishe namna ya kuzitumia, kwa sababu somo la vitendo ni bora zaidi,

kwa hiyo baada ya kuzitumia nitakurundishia na wewe utakuwa, umepeta somo ni jinsi ngani kuwekeza kwa kuona live.
Mkuu hebu muhurumie mwenzio, sio kiulaini kama hivyo
 
Wadau Mimi ni masikini ila kwa kipindi hiki nimebahatika kupata tzs 4,000,000 natamani sana niizalishe sijui niizalisheje naomba ushauri wenu nifanyeje ?

1.5 M
Nadhani utainua kipato chako
 
Attachments

  • 1411056914782.jpg
    1411056914782.jpg
    72.1 KB · Views: 275
Jibu maswali haya niweze kupata pa kuanzia kukushauri.

1.uko mkoa gani?
2.wewe ni jinsia gan?
3.Unaweza kufanya kazi yoyote, isiyo vunja sheria za nchi na sheria za Mungu? nijibu hayo maswali tafadhari naweza kukushauri mawili au matatu ukachagua moja.
 
Hizo 4m umezikusanya kwa muda gani?
Cha muhimu wewe toa wazo la biashara unayataka watu hapo ndipo wadau wataweza kukushauri.
 
Hiyo hela sio ndogo na wala siyo nyingi sana cha msingi Kama hujajuwa nini chakuifanyia tafuta watalam wa ujasilia Mali wakupe makati JINSI ya kuitumia hiyo hadi ikitoe kimaisha.kikubwa ni nichamu tu juu ya matumizi ya hela.
 
Wadau Mimi ni masikini ila kwa kipindi hiki nimebahatika kupata tzs 4,000,000 natamani sana niizalishe sijui niizalisheje naomba ushauri wenu nifanyeje ?

Umasikini ulionao ni wa akili tu.Hiyo hela uliyonayo inatosha kabisa kuanzisha biashara au kilimo.
 
Mala nyingi biashara uanzia kwenye wazo, sasa wewe inavyo onekana bado hujawa na wazo. Mimi nitakueleza biashara mbali mbali ya kufanya, na hivyo labda unaweza kupata wazo la kukusaidia mkuu. Nime kuhuliza kwamba uko tayari kufanya kazi yoyote isiyovunja sheria za nchi pamoja na Mungu, ukasema ndio.Nili mahanisha kuna biashara zingine ni ngum kufanya wanawake zinaitaji wanaume kwa sana.
1.Kwanza kwa kua uko dar, nenda kwa wale jamaa wanao fundisha ujasiliamali nafikiri wengine wako sinza sina uhakika sana, wao watakuonyeshe bidhaa za wewe kujifunza mfano, kutengeneza sabuni za aina yote,kutengeneza mikate, vipodozi n.k. Ukisha jifunza mfano sabuni jiunge na wale wanao tengeneza na ili kupata ujuzi zaidi. Baada ya apo unaweza kutengeneza mwenyewe na kuanza kusambaza kwa watu. Kumbuka bidhaa kama sabuni zinaenda sana maeneo ya uswahilini na vijijini. Uko mjini wanapenda kutumia sana sabuni za viwanda vikubwa. Ukifika pale nahisi unaweza kupata wazo zaidi kaka.

2.Kwa kuwa wewe ni mwanaume na uko tayari kufanya kazi yoyote, nunua mahidi peleka mkoa wa mwanza. Mkoa huu ni mkoa ambao chakula kinatumika sana kwasababu ya kuwa na ziwa Victoria na hivyo ndani ya hilo ziwa kuna visiwa vingi sana ambavyo viko chini ya mkoa wa mwanza. Visiwa hivi vyote havifanyi shughuri ya kilimo zaidi ya kuvua tu. Kisiwa kimoja tu ambacho angalau kinafanya kilimo japo si kwa sana ni ukerewe. So wewe nunua mahindi peleka mkoa wa mwanza visiwani kwa wavuvi.

Viko visiwa vingi sana na vina watu wengi na hawana chakula,wanategemea mwanza au watu wapeleke uko. Kama huvijui nakutajia kidogo vingine unaweza kuhulizia ukiwa tayari.
1.Kisiwa cha ukerewe, 2 Ukara,3 Ghana a.k.a mkoani, 4.Goziba, 5.Bulbi,6.bwilo, 7.Ilyamenge, 8.kweru,
9. izinga, 11.siza n.k,

Visiwa hivi shughuri zao ni kuvua samaki tu na watu wanaoishi uko ni wengi na chakula ni bei kwa sababu hakuna anayelima ispokuwa ukerewe. Maduka yapo, umeme sehem zingine upo wa
kutumia majenereta makubwa, mashine za kusaga unga zipo. Hivyo unaweza kupeleka mahindi ukafungua stoo na kuyauza kwa bei nzuri. Unaweza kuyasaga ila wakati mwingine si vyema kupeleka unga kwa sababu njia ya usafiri wake ni wa maji unga unaweza kupata maji. Ila kisiwa cha Ghana,Goziba na na vingine kuna meli kubwa zinaenda uko zikitokea mwanza. Ghana inaenda meli inayoitwa JULIANA nyingine nimeisahau na inapitia na visiwa vingine.

Ukerewe inaenda meli inayo itwa Nyeunge na meli ya serikali si ikumbuki jina, ila ukiwa mwanz a kirumba mwaloni unaweza kupata maelekezo yote ya hivyo visiwa. Visiwa vingine vina hata mashule ya sekondari. Kisiwa kama cha Ghana kinaitwa mkoani kwa sababu ya watu wengi. Ukiwa mwanza mwaloni utapata maelezo mengi mkuu na ikitokea umefika hata hicho kisiwa mfano cha Ghana unaweza kupata wazo la biashara nyingine mkuu.

3.
Dar kuna mahotel ambayo si makubwa sana yako saizi ya kati, nenda uombe tenda ya kuwa kila siku unawapelekea vitunguu, nyanya, karoti, viazi vya chips n.k, waki-kukubalia,viweke kwenye parkage nzuri na uhakikishe kila siku unawapelekea na ongea na meneja kama inawezekana ulipwe hela yako kwa wiki siyo mwezi kwasbb mtaji wako si mkubwa. Jambo hili wakati mwingine unaweza kujidharau na kuona hutakubaliwa,lakini ukimtanguliza Mungu atakufungulia njia.Hapo pia unaweza kuomba tena ya kuwa kila siku unawapekea kuku wa kienyeji au mayai inawezekana pia.

4
.Nenda mkoa wa pwani maeneo ya mto ruvu, kuna sehem watu ukodisha mashamba yao kwa bei nafuu, nenda ukodi eneo la heka 2 tu, lima mazao ya muda mfupi, na nunua pump ya nchi 2 au 3 ya petrol bei yake haizidi laki 4 kwa ajili ya kumwagilia nakupata mazao yako bora. Baada ya muda mfupi unaweza kuvuna na utakuwa umetumia hela ndogo na nyingine itakuwa benk kama reserve.

5.
Kama unapenda kwenda kwenye madini , nenda kwenye machimbo yanayo toa dhahabu kwa wingi,jifunze kuona wenzio wanafanyaje? Na kabla hauja nunua jua hiyo dhahabu yako ikisha chomwa inatoa % ngapi. Hapa usitumie hela zote unaweza uka anza na1.5mil, ukanunua gram zako 22 uka ziuza tena kwa wenzio kwa bei ya faida au ukaleta dar mtaa wa kitumbini ukauza Inategemea utakavyo piga hesabu ya nauli na faidi kama vitakuwa na uwiano sawa.

6
.Unaweza kwenda kariakoo sokoni ukatafuta watu wanao uza dagaa , ukaomba kuwaletea wewe kutoka mwanza dagaa wazuri. Mfano nimeona juzi kwenye bei ya vitu soko la kariakoo, dagaa gunia la kg 80 linauzwa300,000. Mwanza mwaloni unaweza kulipata kwa 180,000 -200,000 au chini yake kutegemeana na giza. Usafiri wa gunia moja mwanza hadi dar, si zaidi ya 7,000 hii ni maximum. Hela hii siyo wewe kukodi gari, ni kuchangia kwa wengine wenye mizigo ya kuja dar. Sasa mpaka lina fika sokoni linaweza kuwa na shs 210,000. Wewe kama umenunua magunia 10=2,200,000 ukiuza bei ya haraka sana usibaki na mzigo 250,000 utakuwa umepata faida ya shs 40,000 kila gunia,jumla ya faida yote 40,000 x10=400,000. Hivyo ukipata order nyingi angalau kwa mwezi ukaenda mala 3 nafikiri unaweza kupata kafaida mkuu.

7
.Kuna mradi wa kufuga kuku, unaweza kuwauliza wafugaji wa kuku wanafanyaje na faida yake.Nahisi wakikuelezea unaweza kupata wazo mkuu.

8.
Kama uko kwenye centre nzuri, unaweza kufungua kibanda cha chips na vyakula. Jioni ukauza chips sana lakini pia mchana kwa kuwa dar ni joto sana, unaweza kununua machine za kusaga juice za matunda, na pia unaweza kwenda veta ukanunua machine za kukamulia juice ya miwa. Hivyo mchana unakamua juice ya miwa +juice ya matunda ukauza sana kwa sababu ya jua kali. Na jioni kwa sana ukauza chips sana kwasbb mabachela jioni ndo wanapiga misosi ya chips sana.

9
.Kuna biashara ya M-pesa,tigo Pesa, maxmalipo, wahulizie wanaofanya kama kuna faida, nahisi wakisha kwambia utapata wazo mkuu.

10.Fanya biashara ya kusambaza mkaa kwa wafanya biashara ya chips na mahotel yanayo tumia mkaa. Nunua boda boda kwa kusambazia mkaa kwa wateja wako wote. Ukimaliza kusambaza kwa wateja wako wote, kama muda una kuruhusu piga kazi mwenyewe ya kuchukua abiria , hacha mambo ya umwinyi kuajiri mtu wakati wewe unashinda home tu na
bado mtaji wako mdogo eti unajifanya bosi kwa kumiliki boda boda piga kazi mwenyewe . Tafuta wateja wako wa mkaa wanao tumia mkaa dar kote. Ukipata wateja 20 wa uhakika, na kila mteja unampelekea mkaa wa kiroba kidogo cha shs12,000. Hivyo 12,000 x20=240,000 hivyo unaweza kuwa unawapelekea kila baada ya siku 3 au 4. Nafikiri ukitafakari pia kwa hili utapata wazo mkuu.

Naishia apo chukua michango ya watu walio kuchangia +na mchango wangu,nafikiri kama utakuwa serious utapata wazo kaka. Na Mungu akutangulie.
 
Bwana Felix

Sijui nikupe like ngapi? tu utakazo lizika. umetoa somo ambalo ni nandura kulipata hata shuleni
hongera sana

Kwanza sasa hivi naiprint post hii.
kuna ndogo yuko kijijini nitampelekea kwa ajili ya kujifunza.
 
Last edited by a moderator:

Hakika Mkuu Felix Marehemu Dada Yangu Angekuwepo Hai Ningekuozesha. Naomba Mwenyezi Mungu Akuzidishie Baraka Tele, Akupe Mafanikio, Furaha, Amani, Upendo Na Endelea Kuwa Na Moyo Huo. Umetoa Msaada Mkubwa Sana Haswa Kwa Sisi Tulio Na Vihela Vyetu Vya Ngama Kuanza Kujipanga Na Kuthubutu Pia. Mkuu Pokea Baraka Na Dua Zangu Na Uwe Juu Kama Mlima Kilimanjaro. NIMEKUKUBALI! Sina Cha Kukupa Ila Utabarikiwa Sana Na Nahisi Wewe Pia Ni Mtu Wa Imani.
 
daaaaaa......... kaka ubarikiwe wewe ni mtu wa aina yake, all da best
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom