Roulette
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 5,579
- 5,381
Natanguliza salam kwa members wote, hasa wazowefu wa jukwaa hili.
Leo nimeona swali langu nililete hapa ili ninufaike kwa mawazo yenu kama great thinkers.
Katika pita pita zangu nimeona picha ya world wealth distribution (usambazaji wa mali duniani) ambayo ikanipeleka kuchimba zaidi ili nijue ni kitu gani kinasababisha dhulma hii, hasa tukizingatia malighafi (raw material) ya kujenga muindombinu ulaya na north america zinatokea in 'underdeveloped world'.
Picha yenyewe hii hapa:
Utafiti wangu ukaendelea kwa kuelekea taasisi zinazohusika na maendeleo kimataifa ambazo ni International Bank for Reconstruction and Development (ikijulikana kama The world Bank, au THE Bank), na International Monetary Fund (zote pamoja zikijulikana kama Bretton Hood institutions). hawa watu wanafanya nini? na mbona reconstruction ya nchi za ulaya baada ya WWII ilienda haraka sana ila za Africa na Asia zinachelewa? Nilisoma reports zao, na methods zao nikagundua (nadhani) kosa lipo kwenye Ufafanuzi wa neno Maendeleo.
Hizi institution zinachukulia maendeleo ya nchi kama "kuishi kama ulaya". Kwa hiyo, nchi yoyote isio na GDP kama ulaya, wasomi kama ulaya, mabarabara kama ulaya na kadhalika inaonekana kua nyuma kimaendeleo. Na hata leo, indices za kusema nchi fulani iko 'developed' au 'developing' inatumia vigezo hivyo.
Tabu ni kwamba ressources zilizo leo duniani haziwezi kutosha ikiwa kila mtu ataamua kuishi kama watu wanavoishi ulaya, na chanzo cha vita nyingi ni kujaribu kupigania na kuwahi kudhibiti ressources hizo. Tabu ingine ni kwamba wenye kumiliki hizo institutions wanabadili vigezo mara kwa mara ili nchi fulani zibaki kua 'developed' na zingine 'developing' na category hizo ndio zinatoa nguvu katika uwanja wa kimataifa. kwa kifupi, tunaendelea kukandamizwa sababu hatuwezi kujitoa katika hali ya maendeleo duni sababu wanaosema nani kaendelea na nani hajaendelea ni wale wale.
Na kufatana na vigezo hivyo wanatoa 'misaada' (mikopo yenye very high interest) na kuzilazimisha nchi zinazofaidi mikopo mitazamo yao ya namna ya kusimamia uchumi wa nchi (kupunguza ushuru kwa biashara toka nchi zao, kupunguza ushuru kwenwye malighafi zinazoenda kwao, na kuongeza ushuru kwenye biashara zinazotengenezwa nyumbani, kupunguza mishahara ya watumishi wa umma na kadhalika).
India na china zimejitoa katika harakati za maendeleo, kama ilivyo fafanuliwa na Bretton Whods institutions, na kuleta ufafanuzi wao wenyewe, toka kwa wanainchi wao. Leo katika vigezo vya hizo institution bado wako nyuma sana ila ukweli ni kwamba nchi hizo zinaenda kuitawala dunia.
Hivi, tukijaribu kufikiria, sisi kama waafrika kuhusu swali hili, nini maana ya maendeleo kwetu? Kweli tunataka kuishi kama wazungu (destruction of social and environmental stability for the benefit of consumerism and industrialization) au tuna matarajio tofauti ?
Swali langu, wana JF, na hasa wazoefu wa jukwaa hili: Maendeleo ni nini kwetu sisi? na tunajitoaje katika hali hii?
Nawakilisha