Naomba tafsiri

TWANJUGUNA

Member
Jun 6, 2010
28
1
Mimi ni mgeni jukwaani, nataka kushiriki kujifunza lugha.
Lakini kwanza ni na swali: nini tafsiri ya neno MILITARISM. the ideology of building a strong armed force to expand a country's economic and political interests.

Uanamgambo? miundo-jeshi, imla-kijeshi, ubepari-jeshi, uanajeshi-dhulumu, fikra-kijeshi, kiini-jeshi,...........
Ingefaa pia kujadili vipi kila neno katika haya niliyopewa yanahusiana na militarism.
 
Kwanza kabisa sikubali na maelezo yako juu ya maana ya neno hili "militarism"; (naona pia kuna mitazamo mbalimbali). Naona ni zaidi itikadi inyotaka ya kwamba jamii yote ifanye kazi kufuatana na mfano wa jeshi yaani kwa kutii na kutekeleza amri za juu; hii pamoja na nafasi kubwa ya jeshi katika jamii na siasa.

"Militarism or militarist ideology is a view on society. It says society should be like the military. This means that society should follow concepts that can be found in the culture, system and people of the military." (simple.wikipedia.com "militarism")

"Glorification of the ideas of a professional military class" and "Predominance of the armed forces in the administration or policy of the state"
(Militarism - Wikipedia, the free encyclopedia).

Kwa hiyo nisingetafsiri kwa neno moja lakini kwa sentensi kama huko juu. "Ujeshi" inakaribia lakini haieleweki vile.

Mapendekezo yako - hayanivuti sana.
 
Socialism = Ujamaa, socializatioan = Ujamaishi
Militarisim = Ujeshi, militarization = Ujeshishi

Lugha inakua kwa kuwa na kila neno linalojitosheleza kueleze concept kuliko kutunga sentensi ili kutafsiri neno. Sifurahishwi na "live = moja wa moja". kwa nini kutumia sentensi kutafsiri neno.
 
Socialism = Ujamaa, socializatioan = Ujamaishi
Militarisim = Ujeshi, militarization = Ujeshishi

Lugha inakua kwa kuwa na kila neno linalojitosheleza kueleze concept kuliko kutunga sentensi ili kutafsiri neno. Sifurahishwi na "live = moja wa moja". kwa nini kutumia sentensi kutafsiri neno.

Mara nyingi haiwezekani kutafsiri moja kwa moja kutoka lugha moja kwenda nyingine. Hili ni jambo la kawaida kati ya lugha nyingi hasa kwa sababu ya utamaduni tofauti-tofauti nyuma ya lugha mbalimbali. "Ujeshi" unaweza kuwa neno la kufaa likiendelea kusugulikiwa jinsi ilivyo - sidhani inatosha.

Ujamaishi naona ni kichekesho; yaani kwa kawaida "socialization" ni jinsi gani mtu anazoea na kupokea mazingira na jamii wakati "Socialism" ni itikadi ya kisiasa au utaratibu wa kiuchumi. Hayo ni mambo mawili tofauti, haisaidii ukijaribu kuiga Kiingereza.
 
... jamaa asema ni 'kijeshijeshi'....
Vipi maoni yako?
Jamani haya ni swali la mapatano kwangu. Yaani tukizoea kujadili mambo kwa lugha ya Kigeni (Kiingereza) na tukitaka kuendelea kwa Kiswahili hatuna budi kuelewana na kupatana. Yaani tukijadili kitu kisichokuwepo katika utamaduni wa jadi hatuna budi ama ubuni maneno mapya au ubadilisha uzoefu wa maneno yaliyopo. Hivyo ndivyo katika kila lugha. Naona "itikadi ya kijeshijeshi" inawezakana.

Lakini lugha si kitu imara iliyochongwa kwa mwamba (kama maneno ya amri 10) Wengine wanaonaje?
 
Asanteni nyote kwa mchango wenu. nafikiri kila lugga ni kukuzwa na hivyo basi jina militarism naamua ni UJESHIJESHI. tayari nachangia liorodheshwe kwenwe kamusi.
 
Back
Top Bottom