Naomba tafsiri ya sentensi, 'Baba mimi ni mtoto wa ngapi kuzaliwa kwenye familia?' kwenda lugha ya Kiingereza

"Father, What number in the sequence of your birth am i fit"

"Father, Where do i fit in the family"

"Where am I in the birth order of my family?"

Ukiuliza hivi. Kati ya hizi sentence 3 hapo juu a native English speaker atalewa kabisa ulichouliza
Father, what is my position in the family birthwise
 
Kaniuliza anawezaje kusema sentensi hii kwa kiingereza?

"Baba, mimi ni mtoto wa ngapi kuzaliwa kwenye familia?"

Msaada Tafadhali.
Dad, among your children age chronologically, what number am I on?
 
Sio kila kitu kinatafsirika moja kwa moja katika lugha moja kwenda nyingine, lugha ni utamaduni wa jamii husika, ndiyo maana sisi husema mama mdodo/ mkubwa au shangazi tunatofautisha, tamaduni nyingine za Kimagharibi hkn tofauti wote ni ant, sisi tunapiga vigelegele Wachina au Wahindi hawajui wala siajabu hawana neno lake

Hivyo usiumize kichwa, isitoshe ni swali lisilo na mantiki, kwani kila mtoto anajua yeye ni wangapi kuzaliwa.
km ulijirusha nje huko mwingine hajui, una watotot nje, mlta mada ameuliza usimponde hana mantiki kiswali!
 
Kaniuliza anawezaje kusema sentensi hii kwa kiingereza?

"Baba, mimi ni mtoto wa ngapi kuzaliwa kwenye familia?"

Msaada Tafadhali.



Hakuna swali hilo katika kiingereza, lipo kwa kiswahili na lugha zingine.🤣
 
Kaniuliza anawezaje kusema sentensi hii kwa kiingereza?

"Baba, mimi ni mtoto wa ngapi kuzaliwa kwenye familia?"

Msaada Tafadhali.
Mkuu nilikuwa natania tu, jibu lake ni hili:-

Father, what is my birth order?

Yaani, Baba mimi ni mtoto wa ngapi?

Na baba naye atakujibu, (mfano) you are a first born, au you are a third born, nk, yaani wewe ni mtoto wa kwanza au wewe ni mtoto wa tatu, nk.

Birth order ni nafasi ya kuzaliwa kwa kiingereza.
 
This is not so easy to put simply, but here are some possible examples for this question:

Dad, what number child am I in the family?

Dad, where do I come in the family? (In this question the context for the question is already understood).

Possible answers: You were the second-born. / You were born second. / You were our second child. etc.
 
Back
Top Bottom