Naomba kujuzwa kuhusu Kampuni ya Global Alliance

Hao ni Kama matapeli tu , maana wanakuelekeza hela za kusadikika ambazo kuuhalisia kuzipata haiwezekan
 
Mambo yao ndo km hayo
20240418_214852.jpg
 
Japo siifahamu hiyo kampuni، lakini nina fahamu baadhi ya kampuni ambazo zinajihusisha na uuzaji wa virutubisho kama Forever, BF SUMA, Neo Life nk

Kwa maoni yangu hizo ni biashara kama biashara nyingine, na sio utapeli.

ila ni ngumu mno kufanikiwa kwenye biashara hizi, kimsingi zinahitaji nguvu kubwa kuliko hata biashara za mtaani.

1. Gharama za kuanzia ni kubwa
2. Gharama za kuendeshea ni nyingi; kuhuhuria semina , bando la kutosha, kulipia matangazo, kuwalipa mentors wakufunze biashara.
3. Gharama za bidhaa ni kubwa mno kiasi kwamba watu wengi hawawezi kununua, mfano kipindi hicho nafanya dawa ya mswaki ilikuwa 23,000 ambapo kwa Sasa nadhani itakuwa ni zaidi ya 25,000

4. Sio biashara za kutegemea mafanikio ya haraka kama inavyosemwa, yaani unatakiwa ujipe muda angalau zaidi ya mwaka wa kujijenga tu bila kupata faida

5. Hizi biashara unaweza kukaa Hadi miezi 6 hujapata mteja hata mmoja.

6. Kuna mentor wangu mmoja aliwahi kuniambia; usinione na mafanikio haya na namna navyoeleza mafanikio kwa urahisi ila nimepitia shida miaka miwili biashara ilikuwa haifanyiki ila siwezi kusema kwenye semina.

7. Kama huwezi kuongea; mdomo mzito kama umemeza keki ya 500, kama mbali na hizi kazi

NB
Kwa mtu anayejitafuta usijaribu kuingia kwenye hizi biashara huku ukitegemea mafanikio ya haraka

Ni kweli baadhi ya watu wachache wanafanikiwa (nathibitisha Hilo) ila wengi zaidi (asilimia zaidi ya 80) wanafeli

AKILI KICHWANI
 
Hao ndio matangazo yao wanaweka kwenye nguzo za umeme, mshahara laki 3 😅.

Nenda mkuu na degree yaki ukatembeze vipodozi.
Kweli kabisa. Hawo ndio wazee wa "mpaka laki 3 kwa mwezi". Jamaa yangu aliwahi kutembeza masufuria kutwa nzima hajauza hata moja.
 
Hatari! Alliance wanahusika na uuzaji wa dawa na virutubisho. Kiingilio ni sh laki 5.
 
🤣🤣🤣🤣 Wajinga kumbe bado mpo! Hiyo nauli na muda utakaochezea bora uweke vocha utafute nafasi nyingine, au unywe hata soda ya baridi!
 
Japo siifahamu hiyo kampuni، lakini nina fahamu baadhi ya kampuni ambazo zinajihusisha na uuzaji wa virutubisho kama Forever, BF SUMA, Neo Life nk

Kwa maoni yangu hizo ni biashara kama biashara nyingine, na sio utapeli.

ila ni ngumu mno kufanikiwa kwenye biashara hizi, kimsingi zinahitaji nguvu kubwa kuliko hata biashara za mtaani.

1. Gharama za kuanzia ni kubwa
2. Gharama za kuendeshea ni nyingi; kuhuhuria semina , bando la kutosha, kulipia matangazo, kuwalipa mentors wakufunze biashara.
3. Gharama za bidhaa ni kubwa mno kiasi kwamba watu wengi hawawezi kununua, mfano kipindi hicho nafanya dawa ya mswaki ilikuwa 23,000 ambapo kwa Sasa nadhani itakuwa ni zaidi ya 25,000

4. Sio biashara za kutegemea mafanikio ya haraka kama inavyosemwa, yaani unatakiwa ujipe muda angalau zaidi ya mwaka wa kujijenga tu bila kupata faida

5. Hizi biashara unaweza kukaa Hadi miezi 6 hujapata mteja hata mmoja.

6. Kuna mentor wangu mmoja aliwahi kuniambia; usinione na mafanikio haya na namna navyoeleza mafanikio kwa urahisi ila nimepitia shida miaka miwili biashara ilikuwa haifanyiki ila siwezi kusema kwenye semina.

7. Kama huwezi kuongea; mdomo mzito kama umemeza keki ya 500, kama mbali na hizi kazi

NB
Kwa mtu anayejitafuta usijaribu kuingia kwenye hizi biashara huku ukitegemea mafanikio ya haraka

Ni kweli baadhi ya watu wachache wanafanikiwa (nathibitisha Hilo) ila wengi zaidi (asilimia zaidi ya 80) wanafeli

AKILI KICHWANI
Hamna lolote ni utapeli Sasa weweutawndeshaje biashara na kuwaa minisha watu wakati unajua haitembei
 
Mkuu, anaeijua kampuni inyoitwa Global Alliance anijuze, naona walinipigia simu nifike kwenye interview yao wanfanyia Kibo palace Arusha, kwa anaejua baadhi ya maswali wanoweza kutoa. Mimi nina BSc. Marketing Management
Hao Majamaa nishawahi endaga kwenye hizo wanazoita interview ilikuwa 2018.
By that time nilikuwa First Year. Walisema niende hapo Mikocheni karibu na Feza NURSERY.

Nashangaa nimefika nakuta watu wamevaa suti tu za dark blue, mara naskia muda wa training umefika. Ikabidi niulize mimi nimekuja kwenye interview mbona mnaniambia niende kwa training wakuu, nkaambiwa nitulizanw Mambo mazuri hayataki haraka.

Training ikaanza, nashangaa watu wa masuti wanaonesha ushirikiano mnoo, Mara mambo ya mtu Kulia mtu kushoto. Mara mambo ya Timu. Kiukweli nilikuwa naona usiku tuu (yaani sielewi)

Kiufupi, wana package zao kuanzia package ya 500k ambayo unapewa madawa ambayo yanatibu magonjwa tofauti, so kupata faida ni kwa kuziuza, na kushawishi watu wajiunge ili wanunue hizo package za 500k na kuendelea ili upate faida.

So, kama utaweza kufanya hio shughuli nenda. Usisahau tu Notebook na kitambulisho chako chochote 😅

Kila la kheri.
 
Back
Top Bottom