Naomba kujua namna ya kuingiza silaha (Bastola) kwa matumizi binafsi

Silaha inabidi iwe imenunuliwa kihalali huko na document ziwe vizuri kama ni ya kupewa bure kuwe kuna mkataba wa makabidhiano , unao onyesha bei.

Hatua ya kwanza hata kama silaha haijaja, unaenda Central police kuomba
a) Import permit license.
b) Withdraw permit ili kupata hizi inabidi uwe na Number ya silaha. Kwa hiyo wanaweza kukutumia number hata kwa whatsapp ukaanza process.

Kama mtu anakuja nayo kwa ndege anatakiwa awahi sana airport ili iwekwe sehemu ya usalama, na akifika Dar anaiacha airport .

Baada ya hapo unatafuta wakala anayeruhusiwa kuingiza silaha, akaichukue pamoja na kulipia ushuru,

c) Gharama za wakala ni
500,000
d) Ushuru ni 69% ya bei
Iliyopo kwenye receipt
(Bei ya manunuzi)

Wakala ataitoa airport itakuwa kwa wakala hadi utakapo pata kibali cha kumiliki silaha, ikakaa zaidi wa wiki wana charge storage.

Baada ya hapo utaanza taratibu za kuomba kumiliki silaha zinazoanzia serikali ya mtaa kwako mpaka polisi, utaomba aina ya silaha unayotaka kumiliki ambayo utataja ile uliyonunua Nje.,

Kwa hiyo utapima mwenyewe gharama za kuagiza na kununua hapa. Kikubwa bei ya kulw iwe ni ndogo kodi iwe ndogo.

Hapa bei ya ndogo ni 4m - 4.5 m.

Ukianza kumilili gharama ya leseni ni tshs 15,000 kwa mwezi au unaweza lipa 180,000 jumla kwa mwaka
 
Anza kwanza kuomba kibali cha kumiliki silaha ukishapata NDIO ununue .Ikishafika nchini unapofanya clearance waonyeshe kibali unaondoka na silaha yako.

Taratibu nenda ofisi ya POLISI WILAYA AU MKOA WATAKUPA MAELEKEZO

Wakati wa kuomba silaha inabidi uwe umeshainunua maana lazima uitaje aina na namba nk. Kwwnye maombi!
 
Habari wanajamvini

Nimepita Tanganyika Arms kwa lengo la kujua utaratibu wa kuingiza silaha (bastola) kwa ajili ya matumizi binafsi lakini sikufanikiwa kupata majibu. Naomba muongozo kwa anayefahamu utaratibu wa kuingiza kifaa hiki.
Mimi mambo ya bastola ndo sitaki maana ntaua wengi bila kukusudia
 
jopss,
Shukrani sana mtaalam kwa majibu yako maridhawa. Ntashukuru kama nitaweza kupata mawasiliano ya mawakala wanaotambulika.
 
jopss,
Shukrani sana mtaalam kwa majibu yako maridhawa. Ntashukuru kama nitaweza kupata mawasiliano ya mawakala wanaotambulika.

Nashukuru,

Kama upo Dar es salaam nenda mtaa wa Samora eneo la Clocktower katikati ya TRA na Exim Bank
kuna duka la silaha wao ni wakala pia.

Website yao ni:
www.tanganyikaarms.co.tz

samora.png
 
Back
Top Bottom