Nani yupo sahihi..Kibonde ama Kayanda

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,306
6,514
Jamaa wanabishana kwenye kipindi cha Jahazi...Kisa ni baada ya waandishi wa habari kuzuiwa kuingia Mahakamani kuripoti kesi ya Mzee Mwinyi...Lugha iliyotumiwa kuwazuia waandishi hao ni "Kesi hii haiwahusu".
kibonde anasema Lugha hiyo ni sahihi..
Kayanda anasema lugha hiyo si ya kistaarabu.....
 
Kesi haituhusu vipi kwani ile kesi ya talaka?ndio inasikilizwa chamber,si ile ya madai.....kesi zote zinazoenda mahakama ya wazi na huru haiwi siri tena!!Kibonde anawewesekea u DC!ataishia kuoga maji ya kopo tu Mabibo milele na kubwabwaja Clouds ....hizo post za mdebwedo zimeisha this time,katiba inakuja hakuna tena kulipana fadhila!
 
kayanda yuko sahihi.
Kama kesi hii haikuhitajika kusikilizwa na raia wa tanzania, basi ingekuwa busara kuhamisha mahakama na kwenda kuifanyia myumbani kwa mwinyi.
Kuipeleka mahakamani inawapa raia wote haki ya kuisikiliza.
Kama anavyosema kayanda kesi ya mtu kubaka ng'ombe pia haiwahusu.
Baada ya urais mwinyi ni raia kama wengine.
 
kibonde sijui anajipendekeza yani anajifanya anajua kila kitu mimi nimemsikiliza hata hana point yani jamaa sijui ana tatizo gani
 
Jamaa wanabishana kwenye kipindi cha Jahazi...Kisa ni baada ya waandishi wa habari kuzuiwa kuingia Mahakamani kuripoti kesi ya Mzee Mwinyi...Lugha iliyotumiwa kuwazuia waandishi hao ni "Kesi hii haiwahusu".
kibonde anasema Lugha hiyo ni sahihi..
Kayanda anasema lugha hiyo si ya kistaarabu.....
Kibonde ni kilaza na ni gamba,hivi Ma dk huyu jamaa hajaingia kwenye 18 zenu tu?maana alitukana sana wakati wa mgomo!
 
Jf inachekesha sana . Kila siku watu wanadai kibonde kilaza na hawamsikilizi. Na pia hawasikilizi clouds fm. Lakini wakija humu wanachambua yaliyozungumzwa na kibonde na hiyo clouds fm. GREAT THINKER achane unafiki. Kwani ukisema unamsikiliza kibonde unapungukiwa nini?
 
Inawezekana waandishi kweli walikua hawahusiki.

But kauli ingeweza kua ya kiungwana tu na waandishi wakaelewa. Kuliko kumwambia mtu moja kwa moja kua "hayakuhusu"
 
Kuna yale watakayowaambia yanawahusu? Ni lazima tukumbuke kwamba,milango ya uhuru wa vyombo vya habari Tanzania bado funguo za kufuli zake zimeshikiliwa na wajinga wachache.Uhuru wa kupata habari umefichwa kwenye koti la mahakama...Tunawakumbusha waandishi wa habari na jamii kwa ujumla,tusiimbe tu wimbo wa mamlaka ya Rais kwenye katiba mpya,tuliangalie upya suala la nafasi na uhuru wa vyombo vya habari nchini.
 
Binafsi nasikitika kwa mtu mwenye akili kubwa kama Anold Kayanda kufanya kazi na vilaza hawa, jamaa yupo vizuri sana. sasa nashindwa kujua ni kukosa ajira ua ni nini? Kiukweli namkubali sana huyu jamaa. Majina huumba, Kibonde ni Kibonde kweli kama neno lenyewe linavyojieleza
 
Back
Top Bottom