Nani ni waziri wa wizara ya Nishati na Madini, January Makamba au William Ngeleja?

na kama raisi sio mkwere basi hata waziri wa hiyo wizara sio ngeleja,ni hao wasaidizi wa RA

""NAMUUNGA MKONO DR WILLIBORD PETER SLAA AGOMBEE URAISI 2015""

Mkuu hapo kwenye red sasa sawasawa, au ile uliyoandika mwanzo ulikuwa unatingisha kibiriti wanachadema wanzako; au ulisahau kuifuta tangu mwaka 2000.
 
Wakuu Salaam;
Katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia jinsi Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini Mh. January Makamba jinsi alivyokuwa na sauti ya kuwa msemaji mkuu wa wizara hiyo hasa katika mambo yahusuyo umeme. Yaani amekuwa na sauti hata kumshinda waziri mwenye dhamana na wizara hiyo Mh. William Ngeleja. Je kiutaratibu anachokifanya January ni sawa ama anavuka mipaka ya kazi yake? Au ni kuwa waziri wa wizara husika ha-perform ndiyo maana January anasikika sana?

hii wiraza maya mwisho nilijuwa inamilikiwa na rostam kwa ubia na lowasa lakini kijana wa makamba nazani swala la form za 2015 kuzingatia Godfather anaweza asifike anaona atoke kivyake kama justine beiber vile na swala la youtube
 
wakuu salaam;
katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia jinsi mwenyekiti wa kamati ya bunge ya nishati na madini mh. January makamba jinsi alivyokuwa na sauti ya kuwa msemaji mkuu wa wizara hiyo hasa katika mambo yahusuyo umeme. Yaani amekuwa na sauti hata kumshinda waziri mwenye dhamana na wizara hiyo mh. William ngeleja. Je kiutaratibu anachokifanya january ni sawa ama anavuka mipaka ya kazi yake? Au ni kuwa waziri wa wizara husika ha-perform ndiyo maana january anasikika sana?
hiyo yote ni mikakati ya kifisadi. Kwa kuwa bunge lililopita kwa kutumia kamatu zake ndio liliwatoa nishai richmond na dowans safari hii lowassa na rostam waliwafadhili wagombea wngi w aubunge kuingia bungeni na kwenda kukamat hizo kamati na ndio wanatekeleza mipango yao sasa.
 
hii wiraza maya mwisho nilijuwa inamilikiwa na rostam kwa ubia na lowasa lakini kijana wa makamba nazani swala la form za 2015 kuzingatia Godfather anaweza asifike anaona atoke kivyake kama justine beiber vile na swala la youtube
Habari za siku Shekh.
Tunaanza mfungo
 
Nadhani hujawaelewa wachangiaji, na pili huelewi mgawanyo wa madaraka.
Kazi ya bunge ni kuisimamia serikali itekeleze majukumu yake. Kamati za bunge haziwajibiki kwa wananchi au serikali moja kwa moja bali kwa bunge.Mzee Shelukindo alipofanya uchunguzi wa awali kuhusu Richmond alifikisha taarifa yake mbele ya bunge, na bunge likaitaka serikali ifaye uchunguzi, ndipo miujiza ya TAKUKURU ilipoanzia.
Baada ya kutoridhishwa, bunge likaunda kamati ya Mwakyembe na matokeo yake tunayajua. Ikafikisha mapendekezo kwa serikali ambayo iligoma kuyatekeleza, hapo hakukuwa na jinsi kutokana na katiba ya nchi inayompa Rais uwezo wa kila kitu.

Makamba kama kamati zingine za bunge zilizopo na zilizotangulia anatakiwa afikishe taarifa zake ndani ya bunge na si kuongea na vyombo vya habari kila siku. Yeye si msemaji au mtendaji wa wizara ya nishati na madini. Lakini pia fahamu January uwepo wake pale una maana kwa masilahi fulani. Kwahiyo kufanikiwa kwake si kwa ajili ya umma bali person gain. Kama ni kufanikiwa, kwanini Makinda hataki suala hili lijadiliwe bungeni? jiulize! nani anamkwaza January kama unavyotaka tuamini!
Yeye akiwa msaidizi wa Rais wa zamani anajua kila kitu kuhusu umeme, Dowans, Richmond na madudu mengine mengi tu. Hili suala la kujitokeza mara kwa mara ni kutafuta cheap popularity.
Jiulize kwanini Ngeleja anakwepa suala hili! anajua wazi kuwa kuna utata na unaweza kuiweka serikali pabaya zaidi. Sasa wanaitumia TANESCO kukamilisha mission. TANESCO ni serikali ile ile, wajumbe wake wanateuliwa na Rais kwa ushirikiano na waziri husika. Kuwapa kazi ya kumaliza Dowans ni kujivua madaraka na kuendesha mambo kwa remote. Tunajua hili.
Ndugu yangu nakuita humu sijakuona siku nyingi.


AKSANTE JAMII FORUMS.
 
Back
Top Bottom