Nani ni mashujaa wako kwa mwaka 2023? Binafsi wafuatao ndio mashujaa wangu

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,056
49,743
Kwa mwaka 2023 Kuna watu wametoa mchango mahsusi katika nyanja mbalimbali za kimaisha ambao umeleta mchango chanya Kwa Ustawi wa Jamii.

Hawa wanapaswa kutambuliwa kama Mashujaa wa Taifa angalu Kwa kipindi husika in this case mwaka huu wa 2023.

Hivyo basi historia itawaandika na kuwakumbuka katika Utumishi wao na mchango wao adhimu Kwa Taifa.

Kuna Mashujaa wengi Kila mtu Kwa nafasi yake ila Kwa mwaka 2023 Wafuatao ni Mashujaa Wangu ambao wametoa mchango adhimu au kufanikisha masuala maalumu yenye Tija na maslahi mapana Kwa Taifa.

1. Samia Suluhu Hassan
Rais wa JMT

Ukiacha jukumu lake la kulivusha Taifa kwenye masuala mbalimbali ila namtambua Kwa kufanikisha Maridhiano ya Kitaifa na hivyo kubatilisha Amri iliyowazuia Wapinzani na watu wengine kiunumla kutoa maoni Yao ya kukosoa au kujenga hata kutukana kwenye masuala mbalimbali ya Kitaifa iwe Kwa nia njema au vinginevyo.

Pia namtambua Kwa kuleta Mageuzi ya Kiuchumi yanayolenga kukuza sekta binafsi, kupunguza urasimu na kuleta Ufanisi Kwa maslahi ya Nchi. Jambo mahsusi ni Uwekezaji wa DP World Bandari ya Dar, Mageuzi ya Kilimo, kuundwa Wizara ya Mipango na uwekezaji, Tume ya Mipango na Kuanza mchakato wa Uandishi wa Dira ya Taifa 2050 miongoni mwa mambo mengi yakiyofanyika.

Samia ni Mama wa Mageuzi,Injinia ya Uchumi na Mwanga wa Demokrasia, nampa maua yake sawa na PhD za heshima 3 alizozipata.

View: https://twitter.com/Hakingowi/status/1741022499524026533?t=VpGcvXUgS4don51f5FZBpw&s=19

2. Prof. Mkenda.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali na Mbunge wa Rombo.

Bwana Huyu ameiongoza timu ya Wizara Kupitia kikosi kazi Kilichoundwa na Serikali Kuratibu na kuja na Mapendekezo ya kuanza rasmi Kwa Mtaala Mpya wa Elimu ambao uta reshape Taswaira ya Elimu ya Tanzania Kwa miaka 100 ijayo.

-Tayari Kazi imekamilika na utekezwaji wa kuanza kufundisha Elimu ya Mtaalamu Mpya ni 2024 ambapo Elimu ya lazima ni kidato Cha 4.

Aidha Mageuzi kama hayo pia yameendekea kufanyika Kwa Upande wa Elimu ya Juu chini ya mradi wa HEET. Chini ya Mpango huo wa Mageuzi ya Elimu ya Juu, Prof. Mkenda amesimamia maelekezo ya Rais kuhakikisha Kila Mkoa unakuwa na Chuo Kikuu au Tawi la Chuo Kikuu hivyo Ujenzi wa Miundombinu unaendelea kwenye vyuo vilivyokuwepo na Kwenye Mikoa 14 ambayo hapo kabla haikuwa na Chuo au Tawi la Chuo Kikuu hata Kimoja.

Kazi nzuri kabisa hii, historia itakukumbuka kama Prof. wa Mageuzi ya Elimu Nchini Tanzania.

4. Hussein Bashe.
Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Nzega Mjini.

Bwana huyu namtunuku PhD ya Mwanamageuzi wa Kilimo Kwa Kusimamia na Kuratibu Maono ya Rais Samia na Maono ya Baba wa Taifa ya kukifanya Kilimo Cha Tanzania kuwa Chenye Tija Kwa Wakulima na Taifa chini ya ajenda yake ya 10/30.

- Ameendelea Kusimamia Utekelezwaji wa ajenda ya Mageuzi ya Kilimo 10/30 Kwa Kumshawishi Rais Samia Kwa hoja na hivyo kuwezesha Wizara ya Kilimo kutengewa Bajeti kubwa kuwahi kutokea Toka Nchi hii imeasisiwa.

- Amesimamia Programu ya BBT Kwa Ajili ya Vijana

- Anasimamia Program ya Kilimo Cha Umwagiliaji Kwa kuhakikisha Kila mwaka zaidi ya hectare 95,000 zinaingia kwenye irrigation na kufikisha lengo la hectare Milioni 8 by 2030 kutoka hectare 700k za Sasa.

- Amefufua Mashamba ya mbegu na kuweka lengo la kupunguza utegemezi wa mbegu Kwa 50% by 2030.

- Ameanzisha programu ya Kuchimba visima 65,000 Kwa Ajili ya wakulima wadogo ambapo Kila mkulima atachimbiwa kisima na kufungiwa mfumo wa Umwagiliaji wa drip unaotumia umeme wa jua Kwa ekari 3.

Namtunuku PhD ya heshima ya Mwana mapinduzi wa Kijani na atatuvusha na kufanikisha ndogo ya Rais Samia ya Tanzania kuwa Ghafla la Chakula Afrika by 2030.

View: https://youtu.be/cko82ib-Ndk?si=hqBPy2L6WvGurS8y

4. Wallace Karia
Rais wa TFF.

Bwana huyu Kwa kutumia turufu ya ushawishi wa Rais Samia kwenye uga wa Kimataifa amewezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa Mashindano ya AfCon 2027&CHAN 2024.

-Kufanikisha Tanzania kufuzu kwenye mashindano ya Kimataifa ya AfCon 2024 ya Wanaume,WAFCoN 2024 ya Wanawake na Timu zetu za mpira wa miguu kupata mafanikio mbalimbali.

Namtunuku PhD ya Shuajaa wa Tanzania Kwenye michezo ya mwaka 2023.

5. Queen Sendiga.
MKuu wa Mkoa wa Manyara.

Taifa linatakiwa kutambua mchango wa mama huyu Kwa jinsi alivyopambana Kuratibu na kuokoa ndugu zetu walipatwa na majanga ya Mafuriko kule Hanang.

-Hamulala since Day one akiwa pamoja na wapambanaji wengine lakini katika salamu mbalimbali sijawahi sikia akitajwa licha ya Kuonekana mara kadhaa akiwa site kuonesha Uongozi.

Kwa niaba ya wote waliojitomea Kwa Hali na Mali namtunuku PhD ya Ushujaa wa Uokoaji bibie Queen Sendiga. Taifa litakumbuka mchango wako.

Kuna mambo mengi mazuri yamefanyika Kwa mwaka mzima Kwa watu waliopambana Kwa namna Moja au nyingine na wanastahiki heshima na kutambuliwa ila sio mbaya Kwa niaba Yao hao niliowatunuku PhD za Mashujaa wa Taifa wakasimaa kama ishara ya Juhudi za pamoja za kujenga Ustawi wa Nchi.

Mwisho niwape pole wale ambao Kwa namna Moja au nyingine walikumbwa na maumivu ya aina mbalimbali kwamba ni sehemu ya maisha ya binadamu. R.I.P wafiwa wa Hanang' na waliofariki kwenye Ajali.

Niwatajie mwaka Mpya 2024 wenye heri, tusiache kupambana.

My Take
Muktadha wa Hoja yangu ni National Perspective na sio personal perspective.
 
Kwa mwaka 2023 Kuna watu wametoa mchango mahsusi katika nyanja mbalimbali za kimaisha ambao umeleta mchango chanya Kwa Ustawi wa Jamii.

Hawa wanapaswa kutambuliwa kama Mashujaa wa Taifa angalu Kwa kipindi husika in this case mwaka huu wa 2023.

Hivyo basi historia itawaandika na kuwakumbuka katika Utumishi wao na mchango wao adhimu Kwa Taifa.

Kuna Mashujaa wengi Kila mtu Kwa nafasi yake ila Kwa mwaka 2023 Wafuatao ni Mashujaa Wangu ambao wametoa mchango adhimu au kufanikisha masuala maalumu yenye Tija na maslahi mapana Kwa Taifa.

1.Samia Suluhu Hassan

Rais wa JMT ukiacha jukumu lake la kulivusha Taifa kwenye masuala mbalimbali ila namtambua Kwa kufanikisha Maridhiano ya Kitaifa na hivyo kubatilisha Amri iliyowazuia Wapinzani na watu wengine kiunumla kutoa maoni Yao ya kukosoa au kujenga hata kutukana kwenye masuala mbalimbali ya Kitaifa iwe Kwa nia njema au vinginevyo.

Pia namtambua Kwa kuleta Mageuzi ya Kiuchumi yanayolenga kukuza sekta binafsi,kupunguza urasimu na kuleta Ufanisi Kwa maslahi ya Nchi.Jambo mahsusi ni Uwekezaji wa DP World Bandari ya Dar,Mageuzi ya Kilimo, kuundwa Wizara ya Mipango na uwekezaji,Tume ya Mipango na Kuanza mchakato wa Uandishi wa Dira ya Taifa 2050 miongoni mwa mambo mengi yakiyofanyika.

Samia ni Mama wa Mageuzi,Injinia ya Uchumi na Mwanga wa Demokrasia,nampa maua yake sawa na PhD za heshima 3 alizozipata.

2.Prof.Mkenda.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali na Mbunge wa Rombo.

Bwana Huyu ameiongoza timu ya Wizara Kupitia kikosi kazi Kilichoundwa na Serikali Kuratibu na kuja na Mapendekezo ya kuanza rasmi Kwa Mtaala Mpya wa Elimu ambao uta reshape Taswaira ya Elimu ya Tanzania Kwa miaka 100 ijayo.
-Tayari Kazi imekamilika na utekezwaji wa kuanza kufundisha Elimu ya Mtaalamu Mpya ni 2024 ambapo Elimu ya lazima ni kidato Cha 4.

Aidha Mageuzi kama hayo pia yameendekea kufanyika Kwa Upande wa Elimu ya Juu chini ya mradi wa HEET.Chini ya Mpango huo wa Mageuzi ya Elimu ya Juu,Prof.Mkenda amesimamia maelekezo ya Rais kuhakikisha Kila Mkoa unakuwa na Chuo Kikuu au Tawi la Chuo Kikuu hivyo Ujenzi wa Miundombinu unaendelea kwenye vyuo vilivyokuwepo na Kwenye Mikoa 14 ambayo hapo kabla haikuwa na Chuo au Tawi la Chuo Kikuu hata Kimoja.

Kazi nzuri kabisa hii,historia itakukumbuka kama Prof.wa Mageuzi ya Elimu Nchini Tanzania.

4.Hussein Bashe.
Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Nzega Mjini.

Bwana huyu namtunuku PhD ya Mwanamageuzi wa Kilimo Kwa Kusimamia na Kuratibu Maono ya Rais Samia na Maono ya Baba wa Taifa ya kukifanya Kilimo Cha Tanzania kuwa Chenye Tija Kwa Wakulima na Taifa chini ya ajenda yake ya 10/30.
-Ameendelea Kusimamia Utekelezwaji wa ajenda ya Mageuzi ya Kilimo 10/30 Kwa Kumshawishi Rais Samia Kwa hoja na hivyo kuwezesha Wizara ya Kilimo kutengewa Bajeti kubwa kuwahi kutokea Toka Nchi hii imeasisiwa.
-Amesimamia Programu ya BBT Kwa Ajili ya Vijana
-Anasimamia Program ya Kilimo Cha Umwagiliaji Kwa kuhakikisha Kila mwaka zaidi ya hectare 95,000 zinaingia kwenye irrigation na kufikisha lengo la hectare Milioni 8 by 2030 kutoka hectare 700k za Sasa.
-Amefufua Mashamba ya mbegu na kuweka lengo la kupunguza utegemezi wa mbegu Kwa 50% by 2030.
-Ameanzisha programu ya Kuchimba visima 65,000 Kwa Ajili ya wakulima wadogo ambapo Kila mkulima atachimbiwa kisima na kufungiwa mfumo wa Umwagiliaji wa drip unaotumia umeme wa jua Kwa ekari 3.

Namtunuku PhD ya heshima ya Mwana mapinduzi wa Kijani na atatuvusha na kufanikisha ndogo ya Rais Samia ya Tanzania kuwa Ghafla la Chakula Afrika by 2030.

4.Wallace Karia
Rais wa TFF.

Bwana huyu Kwa kutumia turufu ya ushawishi wa Rais Samia kwenye uga wa Kimataifa amewezesha Tanzania kuwa mwenyeji wa Mashindano ya AfCon 2027&CHAN 2024.
-Kufanikisha Tanzania kufuzu kwenye mashindano ya Kimataifa ya AfCon 2024 ya Wanaume,WAFCoN 2024 ya Wanawake na Timu zetu za mpira wa miguu kupata mafanikio mbalimbali.

Namtunuku PhD ya Shuajaa wa Tanzania Kwenye michezo ya mwaka 2023.

5.Queen Sendiga.
MKuu wa Mkoa wa Manyara.

Taifa linatakiwa kutambua mchango wa mama huyu Kwa jinsi alivyopambana Kuratibu na kuokoa ndugu zetu walipatwa na majanga ya Mafuriko kule Hanang.
-Hamulala since Day one akiwa pamoja na wapambanaji wengine lakini katika salamu mbalimbali sijawahi sikia akitajwa licha ya Kuonekana mara kadhaa akiwa site kuonesha Uongozi.

Kwa niamba ya wote waliojitomea Kwa Hali na Mali namtunuku PhD ya Ushujaa wa Uokoaji bibie Queen Sendiga.Taifa litakumbuka mchango wako.

Kuna mambo mengi mazuri yamefanyika Kwa mwaka mzima Kwa watu waliopambana Kwa namna Moja au nyingine na wanastahiki heshima na kutambuliwa ila sio mbaya Kwa niaba Yao hao niliowatunuku PhD za Mashujaa wa Taifa wakasimaa kama ishara ya Juhudi za pamoja za kujenga Ustawi wa Nchi.

Mwisho niwape pole wale ambao Kwa namna Moja au nyingine walikumbwa na maumivu ya aina mbalimbali kwamba ni sehemu ya maisha ya binadamu.R.I.P wafiwa wa Hanang' na waliofariki kwenye Ajali.

Niwatajie mwaka Mpya 2024 wenye heri,tusiache kupambana.
Hiyo namba 1, umeonyesha umbayuwai na unafiki wa kiwango cha SGR kwa hali ya juu sana..!! Nyie hao hao mlimsifia JPM kwa kupambana na anayekosoa, ETI LEO HII UNAMSIFIA ALIYEONDOA HILO...!! Mtaacha lini unafiki wa wazi hivi??? Kwanini kila anachofanya rais mnadhani ni cha kusifia tu hadi pale anapoondoka madarakani na anayerithi kiti akibadili naye mnamsifia kwa kubadili..!!??
 
Acha kunichafulia Uzi kama huna Cha ku comment
Wewe tutusa umetaka tutaje mashujaa wa 2023

Shujaa ni Maguful
2023: Tundu Lisu kaomba kwenda kaburini Chato

2023: Makonda kateuliwa Uenezi CCM Taifa na akaenda kaburini Chato

2023: Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Kinana aenda kaburini Chato

2023: Dr Dotto Biteko ateuliwa Naibu Waziri mkuu

2023: ChoiceVariable apigwa mkwara na Kilio baada ya kumchafua Magufuli

Magufuli Shujaa Anayeishi rip

Mtanikumbuka 😂😂😂🌟
 
Wewe tutusa umetaka tutaje mashujaa wa 2023

Shujaa ni Maguful
2023: Tundu Lisu kaomba kwenda kaburini Chato

2023: Makonda kateuliwa Uenezi CCM Taifa na akaenda kaburini Chato

2023: Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Kinana aenda kaburini

2023: Dr Dotto Biteko ateuliwa Naibu Waziri mkuu

2023: ChoiceVariable apingwa mkwara na Kilio baada ya kumchafua Maguful

Magufuli Shujaa Anayeishi rip

Mtanikumbuka 😂😂😂🌟
Magufuli ni Shujaa wako 2023? Marehemu ni Shujaa wako kafanya kipi mwaka huu wa 2023.

Acha kukurupuka kama mkojo wa ndama.
 
Mashujaa wangu ni Mheshimiwa Dkt Mama Samia Suluhu Hasssan Na Dkt Tulia Acksoni Mwansasu.

Hawa pia ni mashujaa .makamu wa Rais pamoja na waziri mkuu kwa kufanya kazi kubwa ya kumsaidia Mh Rais.

Baraza la mawaziri pia ni mashujaa .Ni ngumu sana kumuacha kumtaja na kutambuanmchangi mkubwa wa watu kama Mh ummy mwalimu, Mohammedi mchengerwa, Husseni Bashe,Mwigulu Nchemba na wengine wengi.

Wengine ni wakuu wote wa Vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuhakikisha kuwa Taifa letu linakuwa salama.

Bila kuwasahau wakulima wenzangu ambao tunatumia jembe la mkono kulilisha Taifa letu na kuhakikisha kuwa usalama wa chakula unakuwa wa kutosha na hivyo kuleta amani na utulivu nchini kwa kuwa huwezi ukamuongoza au kusikilizwa na mtu mwenye njaa ya chakula.
 
Back
Top Bottom