Nani anamkumbuka Mzee Majambo?

Duh longtime pale Dunga street kinondoni B alikuwa akipita inakuwa balaa, umenifanya nikumbuke Gari la koni na wimbo wake wa "kikuku kinanukiaaaa" lilikuwa linapita mtaani kwetu kila J5
 
Hata mimi namkumbuka HASWA KINYAGO CHAKE CHA MENO YA FUVU LA NG'OMBE. Nimeishi Mwananyamala B kwa Mama Zakaria na huku pia alizunguka sana na karanga zake hadi Msikiti wa Mwinyijuma karibu na alipoishi huyo mama Zakaria myamwezi aliefuga sana mbuzi na punda na kumiliki bar mbili (Lumpa Bar) karibu na kwa mzee Billy Bandawe
 
Kiboko ya vikojozi wa enzi hizo. Ukisikia majambo ni mbio ndani. Long time kitambo yani.
 
Preta hii sio yenu wa mikoani au wakuja.....hii yetu watoto wa dar tuliozaliwa uswazi! majambo noma,nilikuwa nikimsikia anakuja lazima nikajifiche uvungu wa kitanda!

Ha ha..........hivyo sawa.....maana nilishajiuliza........mbona simjui.......
 
Mkuu.
Niliishi Dunga pia.
Babu alikuwa anatembea kwa mguu jiji zima.
Mfano pale kwetu alikuwa akitokea msasani, kisha anaingia Drive-in,kisha Moroko ananyooka kama anaenda Magomeni, kisha anakatisha kulia anaingia Dunga street. Anakujatokea magenge ya Msufini kisha huyooo Msisiri anaishia zake Mwananyamala.

Alikuwa msanii kwa ujumla.
Watu wazima pia waliinjoi kumuona.
Isipokuwa alikuwa na kawimbo kake kanasema "mimi majambo nakula watu" kisha anakanyaga kishindo kuliza kengele/ manyanga yake nje nje njee!.
Hicho ndicho kilichokuwa kinatutisha watoto.
Na pia hapakuwa na mtoto anaesalia nje.
Yaani vikojozi na wasio vikojozi woote tulitimua mbio kuogopa kuliwa na Majambo.

Nb.
mkuu, Dunga iko Moroko siyo Kinondoni b.

Duh longtime pale Dunga street kinondoni B alikuwa akipita inakuwa balaa, umenifanya nikumbuke Gari la koni na wimbo wake wa "kikuku kinanukiaaaa" lilikuwa linapita mtaani kwetu kila J5
 
Namkumbuka Marehemu Mzee Majambo.
Aliishi Mwananyamala A, Mtaa wa Peramiho; nyumba ya kwanza kabisa pembeni mwa Mwinjuma Rd.
Kwa kuuza karanga na vichekesho alijenga nyumba kubwa tu.
Nilimfahamu akiwa mtu mzima tayari, na alikuwa chongo ila aliyejaa viroja; hasa siku Yanga imeshinda
 
Preta hii sio yenu wa mikoani au wakuja.....hii yetu watoto wa dar tuliozaliwa uswazi! majambo noma,nilikuwa nikimsikia anakuja lazima nikajifiche uvungu wa kitanda!

Eti wa Mikoani...kwani Dar sio mkoa?
 
Last edited by a moderator:
Namkumbuka sana nilikuwa namuogopa sana kama sikosei ni miaka 70s - 80s alikuwa anavaa meno sijui ya mnyama gani na pembe, kibwaya na mkononi anashika mkia alikuwa anauza karanga kweny kikapu.

Ukimuita majambooo anakuja anawauzia karanga halafu anacheza.
 
Mkuu.
Niliishi Dunga pia.
Babu alikuwa anatembea kwa mguu jiji zima.
Mfano pale kwetu alikuwa akitokea msasani, kisha anaingia Drive-in,kisha Moroko ananyooka kama anaenda Magomeni, kisha anakatisha kulia anaingia Dunga street. Anakujatokea magenge ya Msufini kisha huyooo Msisiri anaishia zake Mwananyamala.

Alikuwa msanii kwa ujumla.
Watu wazima pia waliinjoi kumuona.
Isipokuwa alikuwa na kawimbo kake kanasema "mimi majambo nakula watu" kisha anakanyaga kishindo kuliza kengele/ manyanga yake nje nje njee!.
Hicho ndicho kilichokuwa kinatutisha watoto.
Na pia hapakuwa na mtoto anaesalia nje.
Yaani vikojozi na wasio vikojozi woote tulitimua mbio kuogopa kuliwa na Majambo.

Nb.
mkuu, Dunga iko Moroko siyo Kinondoni b.

Mkuu una kumbukumbu nzuri sana kuhusu Mzee Majambo..
 
Back
Top Bottom