Nani ale chakula meza moja na housegirl!

Hizi roho mbaya ziko zaidi kwa wanawake hususani wa siku hizi hasa hasa wale walioolewa na kuonja maisha mazuri ambayo hapo kabla walikuwa maskini na washamba sana. Otherwise ni malezi mabovu waliyolelewa nayo toka utotoni.
 
Mke wangu akifanya kitu kama hicho siku hiyo hiyo mke namrudisha kwao ama House girl aondoke tuishi bila house girl.
 
hawa watu wapo ila cha kufanya unamwambia hapohapo kwamba si sahihi,niliwahi kupata wageni ilikuwa ni familia ya watu sita baba mama na watoto wao wanne,wakakuta mimi na binti yangu wa kazi tunawaandalia chakula ikabidi nitenge watoto wakae dinning na binti yangu akawa anakula nao,huyu mama mgeni hakupata amani gafla akaanza kumtuma binti yule wa kazi kwa vile nilimuelewa nikamwambia aniagize mimi anachotaka kwani yule anakula,hapo pozi lilimuisha na baadae mume wake akashukuru kwamba mke wake atajifunza maana huwa anawatenda vibaya mabinti(mke hakusikia mume alichosema),kipindi kingine tukaenda kwao nikaona amefanya nilivyofanya kwangu sema akawa anajisahau anamwambia "dada acha kula kwanza njoo utoe vyombo" ambapo angeweza kufanya mwenyewe,tuwathamini na kuwapenda wadada wanaotusaidia kazi,

Hongera sana mimependa
 
Mhh tht's jamani too selfish...asubiri kuwekewa sumu..hivi kukaa nae meza moja unapungukiwa nini,
kwetu cz hatuna mtoto tuna houseboy alivokuja alikuwa anajitenga mda wa kula ,analia jikoni,hadi ikabidi kumkurupua aje tule wote,cjui alikotoka alifanyiwa style km hizo ..it's good kula wote bila kubaguana,mnakuwa huru
 
Nilihuzunika sana mama mwenye nyumba alipotamka maneno haya.

Hii imenitokea nilipoenda kwa rafiki yangu niliyesoma naye O level miaka ya 90. Nilishangaa kuona ingawa yeye ndiye aliyeandaa chakula, kilipofika mezani yeye alikuwa ameketi kwa mbali anangojea tumalize kula ili naye aje kusaza mabaki.
Nilishindwa kuvumilia baadae nikauliza-wakati tunaendelea kula - iwaje msichana wa kazi hajajumuika nasi mezani.
Shemeji aliibuka na kujibu, nanukuu 'nani ale chakula meza moja na housegirl? Niliposikia maneno hayo nilikaa kimya, maana shemeji alionekana wazi hapendi kula chakula pamoja na housegirl.
Chondechonde mnaoishi na hawa mugro, jamani tuwachukulie mamugro aka beki tatu kama binadamu, kama anakupikia mlo, anakulelea wanao, na mambo mengine mengi, inakuwaje unamchukulia kama mbwa au paka anayengojea bosi ale halafu yeye atupiwe mifupa au makombo! Tubadilike jamani hasa nyie kina mama wenye nyumba, mweeeeee!

Ulimbukeni wa kuoa mwanamke toka familia maskini. Akija kwako anaona kaukata! Au yeye alikuwa house girl sasa analipiza alivyokuwa akifanyiwa. Tuna ushahidi wa hayo
 
Umeskia ivyo mwanadam mwenzio.ananyanyasika kwa ajili ya mavi ukaendelea kula lolz...me ata nisingeendelea kula
Watu wanaroho mbaya ptuuuuuuuu
 
Mara nying mijanamke ya aina hii ni ile ambayo imekulia katika.dhiki sana sasa imebahatika kupata vijisent ndio.inajiona imefika ovyooooo
 
Kuna watu utafikiri wao ni special sana....wanashindwa kureason kabisa....huyo housegal ndiye unayemuachia nyumba...ndiye anayekutunzia watoto...anawalisha wanao eti leo huwezi kaa naye meza moja.....
Mungu awasamehe wote wenye tabia kama huyu mama...
 
mweeeeee![/QUOTE]

Nimependa mshangao umekaa kihehe watu wa iringa wala mbwa..hahahahah...

Guys house girls are everything to us... They mean a lot...unamwachia nyumba with everything in it.... Sio hilo tu unakuta na watoto pia... Plz respect them..hasa kama weekend hv 'sunday' waachen wakatembee nao waione Dunia inazungukaje!!!
mweeeeee![/QUOTE]
 
Nimesikia eti kuna wengine wanatumia mikojo kama liquid ya kupikia!

na wengine wanatumia mashine zao kuwanyonyesha watoto (h - boys!)

mmh.. hawa jamaa hawa nao wana vimbwanga vyao jamani!

Hatukatai wapo wengi wenye viroja
Ila haifai kunyanyapaa
Maana yake kama hali nao si ajabu anakula makombo/ mabaki, sio poa
 
Nilihuzunika sana mama mwenye nyumba alipotamka maneno haya.

Hii imenitokea nilipoenda kwa rafiki yangu niliyesoma naye O level miaka ya 90. Nilishangaa kuona ingawa yeye ndiye aliyeandaa chakula, kilipofika mezani yeye alikuwa ameketi kwa mbali anangojea tumalize kula ili naye aje kusaza mabaki.
Nilishindwa kuvumilia baadae nikauliza-wakati tunaendelea kula - iwaje msichana wa kazi hajajumuika nasi mezani.
Shemeji aliibuka na kujibu, nanukuu 'nani ale chakula meza moja na housegirl? Niliposikia maneno hayo nilikaa kimya, maana shemeji alionekana wazi hapendi kula chakula pamoja na housegirl.
Chondechonde mnaoishi na hawa mugro, jamani tuwachukulie mamugro aka beki tatu kama binadamu, kama anakupikia mlo, anakulelea wanao, na mambo mengine mengi, inakuwaje unamchukulia kama mbwa au paka anayengojea bosi ale halafu yeye atupiwe mifupa au makombo! Tubadilike jamani hasa nyie kina mama wenye nyumba, mweeeeee!

Huyo mama hakujibu vizuri. Ila na wewe ni mgeni mwenye kiherehere. Ndo nini kuuliza mambo ya taratibu za nyumba za watu? Usikute uliuliza kwa sauti hadi huyo mschana akasikia. Kiherehere
 
Kuna watu utafikiri wao ni special sana....wanashindwa kureason kabisa....huyo housegal ndiye unayemuachia nyumba...ndiye anayekutunzia watoto...anawalisha wanao eti leo huwezi kaa naye meza moja.....
Mungu awasamehe wote wenye tabia kama huyu mama...

Anamwachia ahudumie wanae ila kukaa nae meza moja issue?

Kweli akili zake matope
 
Daah iv kumbe bado kuna watu wanabagua ma housgel!! Hii haijakaa vizuri hata kidogo
 
Umenikumbusha SUA miaka hiyo neno mugro linamaanisha housegal....sasa itakuwaje pale akigundua mumewe anambandua huyo mugro je hawatakula meza moja ..au ?? huyo mama ni mbaguzi tu hana jipya..!
 
Mm housgirl wangu ni kama mwanangu nae huniita baba! Hawa ni watu muhimu kuliko kawaida tuwaheshimu na tuthamini kazi na michango yao kwetu na tunawalipa kidogo jamani! Ubinadamu kazi
 
yaaani mimi najisikia vibaya hawa watu wakiteseka
wamenilea tangu chekekea mpaka leo niko first year
na kwetu ukija huwezi kujua nani dada wa kazi nani binti wa mwenyenyumba
wote tunapendezeshwa kwa usawa kuanzia chini hadi juu
ingawa mimi ni wa mwisho na wa kike pekeee no kudekadeka kazi kama kawa
na kama nipo home dada huwa anapumzika siku ya jumamosi me ndo nashika usukani yaani mpaka uchunguze sana ndo utajua
na binti hata kwenda kwao hataki tuko nae mwaka wa 7 anasema kuacha kwake kazi hadi atakapoolewa

vp kuna dalili kama anamchumba?
 
Back
Top Bottom