Nampongeza Aweda kwa kujilipua na hoja ya madawa ya kulevya ya (Mengi vs Nzowa )ITV , lakini....

pamoja na aliyoyasema lakini aliupotosha umma kuhusu maraisi wa Mexico, rais wa sasa wa Mexico anaitwa Enrique Peña Nieto, na si Felipe Calderón kama alivyosema yeye wakati anachangia kuhusu tatizo la madawa ya kulevya nchini
 
bado tuna safari ndefu sana
ile tuhuma ingekuwa nchi nyingine usingemwona akiendelea na kazi sheria na uchunguzi vingechukua nafasi yake
 
Kwani inakatazwa?Si ni bora yeye kuliko wale ambao hawaisaidii jamii na badala yake wanaishia kuibuka na kuhadaa wananchi?

Mimi nawashangaa sana watanzania wenzangu yani tunafikia kuamini kuwa yeyote anaye pigania haki za jamii yake basi anataka uoongozi. Inauma sana kuona uwezo wetu wa kufikiria umegota kkuamini hivyo maana yake mtu akipigwa ntu asiamulie kwani atambiwa anataka cheo tuachane na mawazo hayo Aweda he was right to ask such question.
 
pamoja na aliyoyasema lakini aliupotosha umma kuhusu maraisi wa Mexico, rais wa sasa wa Mexico anaitwa Enrique Peña Nieto, na si Felipe Calderón kama alivyosema yeye wakati anachangia kuhusu tatizo la madawa ya kulevya nchini

Ni kweli aligeuza marais wa nchi hiyo. Rais aliyestaafu alimtaja kama rais wa sasa na Rasi wa sasa akamtaja kama Rais mstaafu.
 
okey tumekupata bwana Aweda kwa kuja na Id yako nyingine kuja kujifagilia mwenyewe humu JF juu ya kuattend kwako ITV katika mdahalo

Ukiona mtu anawaza hivi ujue ndo mchezo wake. Mtendee haki Aweda kwa kutoa ushahidi wa dai lako. Kwa hiyo, kila thread inayomfagilia Slaa, Lema, Nape, Mbowe, Mwigulu ni wao wamejiandikia kwa ID faki? This called Inferiority complex
 
Kamanda Aweda ameonyesha ujasiri na umahiri wa hali ya juu,hata kama kwao Mbulu level yake ni huko Dar kwenye jimbo la akina "Zungu" wanao tuhumiwa kwa uuzaji "unga"

Msingida,
Uko sahihi Aweda anapaswa kubaki Dar, Mbulu si kuna wengine? Yeye amsaidie Mnyika na Mdee hapa mjini.
 
Jana Aweda alinifurahisha sana kwenye ile kipindi yao ya malumbano ya hoja ya kwenye ITV kuliko mtu mwingine yeyote.
Mada ilikuwa inasema, MADAWA YA KULEVYA KUANGAMIZA VIJANA WETU NA WATANZANIA, NINI KIFANYIKE?

Kamanda wangu Aweda aliibua bifu la Reginald Mengi na Godrefy Nzowa. Nzowa alikuwa amekaa kwenye kiti cha mchokozo mada. Aweda alimwaliza Godfrey Nzowa swali gumu ambalo halikujibiwa. Godfrey Nzowa ni bosi wa kuzuia madawa ya kulevya tena akajisifia kuwa yeye ni bosi wa Tume ya kuzuia madawa ya kulevya kwa miaka saba.

Swali la AweDA,
kuna mtu moja anayeheshimika sana kwenye jamii ya watanzania anaitwa Reginald Mengi na alimtaja wazi. Miaka 2 iliyopita alikutuhumu wewe Nzowa kuwa ulikuwa umetega mtego wa kumbambikia mtoto wa Bwana Reginald Mengi kwa madawa ya kulevya. Je, ni kweli? Halafu akawekaga na chumvi kweye kidonda kwa kuongezesha kuwa ninavyo jua mimi, wewe bado hujakanusha taarifa hiyo. akamalizia kwa kusema tunaomba utupe majibu leo.

Binafsi sijui habari ya Mengi kumtuhumu Nzowa kutaka kumbambikia mtoto wa Mengi kwa madawa ya kulevya ilishia wapi?.

Bahati mbaya Godfrey Nzowa hakujibu na alikaa kimya kama hajasikia na wasimamizi wa kipindi hawakumbana hata kidogo.

Hongera Aweda, lakini taratibu kamanda wangu si unajua kuna tindi kali siku hizi??? Hivi kama wanapanga kumbambikia mtoto wa Mengi madawa ya kulevya, si watamdhuru na yeye Aweda? Namshauri tu kamanda wetu. Nampa Big up.

Mjasiria mali,
Kuna kitu lazima tukiweke vizuri hapa. Bila kuwa na utayari wa kupigania nchi hii nina uhakika watoto wetu, wajukuu na vilembwe watatushangaa sana na mimi sitaku kuwa kati ya watu ambao kizazi kijacho kitawashangaa sana kwa jinsi walivyoliharibu nchi yetu.

Jinsi ulivyoandika ni kama Pongezi lakini nikisoma maelezo yako vizuri ni kama wewe umetishika na hunitii moyo badala yake unataka kunionea huruma - mapambano ni lazima. Hakuna mtu mwenye hati miliki na dunia, muda ukifika lazima tuendoke. Mafisadi hawawezi kutuua mpaka Mungu akubali kwanza.

Lazima tuwe tayari kwa lolote kwa faida ya kizazi kijacho. Sisi leo tuko kama tulivyo kwa sababu kuna watu waliotutangulia ambao walijitoa mhanga kwa ajili yetu.
Natumai umenisoma.
 
Mimi nawashangaa sana watanzania wenzangu yani tunafikia kuamini kuwa yeyote anaye pigania haki za jamii yake basi anataka uoongozi. Inauma sana kuona uwezo wetu wa kufikiria umegota kkuamini hivyo maana yake mtu akipigwa ntu asiamulie kwani atambiwa anataka cheo tuachane na mawazo hayo Aweda he was right to ask such question.

Matema Beach,
Nashukuru kwa comment yako. Watu hawanitendei haki kwa kunibambikia majimbo ya kugombea ubunge wakati mimi sijatangaza nia ya kugombea udiwani, uenyekiti wa mtaa/kijiji wala wala ubunge ktk maeneo hayo yanayotajwa tajwa. muda uliopo ni kuwajenga mtandao wa chama.
 
okey tumekupata bwana Aweda kwa kuja na Id yako nyingine kuja kujifagilia mwenyewe humu JF juu ya kuattend kwako ITV katika mdahalo

Hata wewe nakushukuru kwa kunisingizia.

Ndugu yangu, kama dk 20 iliyopita, nimepokea simu kutoka Radio one wakinialike tukajadili kilimo kwanza leo saa kumi na nusu kwa muda wa saa moja na nusu mpaka saa 12 jioni, nina kiporo star tv ambayo niliitwa nikashindwa kwenda na Alhamisi nitaenda tena kutegemeana na mada nitakayoipenda.
Sasa nitaanzisha thread ngapi ndugu yangu?
Pili, Kumbuka kuwa ITV peke yake unapoongea unaskilizwa na watanzania zaidi ya mil 3 at per, halafu bado nihangaike na ID Feki ndugu yangu kuja JF ili isomwe na watu wangapi? watafika mil 3?

Tatu, kwani kama nina hoja nina kataliwa kuja kuijadili hapa JF Mwenyewe? Mbona nilishafanya hivyo? Soma thread zangu utakuta mifano hai ya hoja niliitoa ITV nikaileta tena mwenyewe hapa JF nikijirefer mwenyewe. Wasiojiamini hufanya hivyo, mimi ninajiamini.

Mwisho, kwa vile signature yako inaonesha wewe ni kada wa ccm, sikushangai kunisingizia.

Asante.
 
Matema Beach,
Nashukuru kwa comment yako. Watu hawanitendei haki kwa kunibambikia majimbo ya kugombea ubunge wakati mimi sijatangaza nia ya kugombea udiwani, uenyekiti wa mtaa/kijiji wala wala ubunge ktk maeneo hayo yanayotajwa tajwa. muda uliopo ni kuwajenga mtandao wa chama.

Hata ukigombea ndugu Aweda nihaki yako ya kikatiba na wala usiludi nyuma kuwatetea watanzanaia wanyonge kwa mawazo mfuu ya hawa magamba. Na unacho kifanya ni njia mojawapo ya kuonyesha jamii kuwa unaweza kuuwatetea hata kama ukiwa kiongozi wao ukizingatia hautumii pesa katika kuuiffanya jamii ikutambue. Mbona watu wanashinda makanisani na misikitini wakitoa pesa walizo tuibia kwenye mazabahu ya Mungu hawasemwi? au kwasababu ni matajiri wa pesa, ndugu yangu duniani hapa hakuna utajiri mzuri kama wa fikra,hekima, busara, utu na upendo na vyote hivi vinaoneka pale unapo fanya kutetea wanyonge kama unavyo fanya wewe. Songa mble bro never give up kwani Mungu yupo pamoja na watetezi wa haki. VIVA CDM
 
Madawa ya kulevya yanaangamiza watoto wetu.
Hata mimi niliangalia, je, mada ya jana madawa ya kulevya kuendelea kuangamiza vijana wetu, nini kifanyike? AWEDA alimwuliza Nzowa kuwa wewe unatuhumiwa kubambika kesi ya mtoto wa Mengi je, jibu hoja. Yule dada alitaka kumsaidia tu Nzowa. Ukweli swali lilikuwa ndani ya mada kabisa, tena sana.

Ndio maana tunatakiwa tuwe na waandishi habari makini na wasio na uoga wa ajabu.
Swali lilikuwa ndani ya mada kabisa, maana jibu lake lingewahakikishia watanzania kwamba mtu anayeongoza taasisi/kikosi/tume inayopambana na madawa ya kulevya ni msafi.
 
TATIZO LA VIJANA WA CHADEMA..... sio kutokuwa weledi,bali ni kila kitu kuzungumzwa kisiasa na kujitafutia umaarufu binafsi na wa chama. wanafika mahali wanatanguliza siasa zaidi kuliko kuli-approach tatizo na kuli address.
huu ukamanda wa kuishia kuvaa gwanda na kujilipua kwa kutumia vumbi wala hautaifikisha nchi yetu popote.
ule mjadala haukuwa na malengo ambayo AWEDA alijaribu kuyaongelea... he was just out of the point and shamefull
 
Kwa hili la Madawa ya kulevya yanayoangamiza watoto wetu, tuache uccm na uchadema kwanza - vijana wetu kwanza. ktk hili Aweda alikuwa sahihi kuhoji usafi wa NZOWA. Tuache ushabiki.
 
Kwa hili la Madawa ya kulevya yanayoangamiza watoto wetu, tuache uccm na uchadema kwanza - vijana wetu kwanza. ktk hili Aweda alikuwa sahihi kuhoji usafi wa NZOWA. Tuache ushabiki.
hukuangalia kipindi nadhani.
siongelei usahihi au upotovu wa kauli na swali la aweda bali approach ya mada iliyokuwa mezani kwa wakati ule.. nilikuwa naona anahemkwa tu na kutaka sifa binafsi kuliko kuumizwa na tatizo husika... there is where my point is..
 
TATIZO LA VIJANA WA CHADEMA..... sio kutokuwa weledi,bali ni kila kitu kuzungumzwa kisiasa na kujitafutia umaarufu binafsi na wa chama. wanafika mahali wanatanguliza siasa zaidi kuliko kuli-approach tatizo na kuli address.
huu ukamanda wa kuishia kuvaa gwanda na kujilipua kwa kutumia vumbi wala hautaifikisha nchi yetu popote.
ule mjadala haukuwa na malengo ambayo AWEDA alijaribu kuyaongelea... he was just out of the point and shamefull

Wewe kama si muuza unga utakuwa mtumiaji.Vijana wanaangamia kwa utumiaji madawa ya kulevya wakati vyombo vya kudhibiti vikiwa vimetulia na kuwalinda wahusika.Wakati umefika tuondokane na fikra za kichama tuwe na ubinadamu.Jaribu kutembelea wodi za waathirika utajua ukubwa wa janga.
 
Back
Top Bottom