SoC03 Namna ya kupanga malengo ya fedha za kukusanya TRA ili kuwe na uwajibikaji, sio kila mwaka wanatuambia wamevuka lengo, kwa kujiwekea malengo madogo

Stories of Change - 2023 Competition
Jul 11, 2020
64
139
Zaidi ya mara moja tumeona Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikionesha kuwa imekusanya mapato Zaidi ya maalengo yao. Hali ambayo kwa haraka inaweza kuonesha kuwa TRA wako vizuri kwenye ukusanyaji wa kodi. Hata hivyo, watafiti wanaonesha fedha nyingi haikusanywi, na kuna upotevu mkubwa wa mapato ya Serikali maeneo mbalimbali.

Ni kwa namna gani TRA waweke lengo la fedha za kuzikusanya
Ili kupima ufanisi wa TRA ni muhimu kuseti malengo ya kodi kwa vipimo vya kimataifa. Namna nzuri ya kupima kodi ni kwa kuangalia uwiano wa kodi na pato la taifa(tax to GDP ratio), ambayo kimsingi ndio inapima ufanisi wa kodi zinazokusanywa. Uwiano ambao Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeshauri uwiano huo unatakiwa usipungue 15% ambapo kwa Tanzania tuko chini ya hapo, yaani kuna mapato mengi yanapotea.

Hivyo basi kwa kuwa tunaweza kukadiria ukuaji wa uchumi na GDP, malengo ya kodi yawe ni yale yanayoenda na GDP. Yaani kama tunatarajia uchumi kwa mwaka wa fedha 2023/24 utakuwa kwa thamani za kifedha ‘ABC’ basi TRA iweke malengo ya kukusanya sio chini ya (15% mara ABC). Tunapofikia lengo hilo maana yake tunakuwa moja kwa moja tumefanikiwa sio tu kufikia malengo bali pia kuwa katika ufanisi wa ukusanyaji kodi.

Ubaya wa mfumo uliopo
Mfumo wa malengo ya ukusanyaji kodi hayana uwazi kuwa TRA wanafanyaje hesabu kujua kiwango cha kodi wanachotarajia kukusanya kwa mwaka. Hali hii inasababisha wenyewe wajipangie kiwango cha chini na baadaye wanakuja kuonesha wamekusanya Zaidi ya 100% ya malengo. Yaani nis awa na mwanafunzi aliyelenga kupata F halafu anapata F inayokaribiana na D anatangaza kuwa kafaulu. Nielewe hapo kama nikitumia kiwango cha ufanisi wa kodi basi ni muhimu kutumika hiyo Tax-to-GDP Ratio ambayo inatuonesha mapato kiasi gani yanalipishwa kodi kwani inapokuwa chini ya 15% maana yake sehemu kubwa ya shughuli za serikali hazitozwi kodi na mfumo ni mbovu.

Hivyo basi utaona, hili suala la kupanga malengo ya kodi ya kukusanya kwa kuangalia makisio ya GDP yanaleta mantiki kwa kuwa itakuwa ni kila mtu anaweza kuona malengo ya nchi. Hapo itakuwa kwamba kama mwaka huu tumelenga 15%, mwaka ujao tunaongeza tunasema tutaenda kukusanya 16% ya GDP hii itakuwa safi kwa kuwa tutakuwa na uwezo mkubwa wa kuona ufanisi wa TRA na kupunguza rushwa kwa kuwa kwa namna zote wanapaswa kuhakikisha mapato hayapotei.

Umuhimu wa namna hii ya kukokotoa kiwango cha kukusanya kwa mwaka
Mbali na ubovu unaoendelea na mapato kupotea kama inavyooneshwa na tafiti mbalimbali, TRA hawajawahi kuwajibika kwa kuwa mara zote huwa wanasema ukusanyaji wao umevuka lengo kwa 100% hali inayofanya waonekane ni taasisi inayofanya kazi vizuri kwa serikali. Hata hivyo tunajua tabia za rushwa na tabia ya kutotoza kodi kwa baadhi ya watu hali inayofanya watu waone kabisa mapato mengi yanapotea.

Kwa mfano, uchumi usio rasmi kwa kiasi kikubwa unashindwa kufikiwa na TRA. Aidha, maeneo ya migodi na bandari zimeripotiwa kuwa na ubadhirifu mkubwa. TRA imekuwa haizungumziwi sana hata baada ya ripoti za CAG kwa kuwa watanzania hawana ufahamu sana wa masuala ya kifedha na uchumi kiasi cha kuchambua mambo hayo. Hivyo, hata waandishi huwa hawaendi mbali kuonesha shida iliyopo kwenye kodi na TRA.

Itauma ila ndio dawa ya kuhakikisha TRA wanawajibika
Tuseme sasa huu ni mwisho wa uzembe na TRA waanze kuona kabisa wanatuangusha kiasi gani kwa kuwa hadi sasa tumebaki na baadhi ya taasisi tu mathalani ATCL na Mashirika mengine ya serikali ambayo yanaonekana hayafanyi kazi vizuri. Kwa upande wa mamlaka, tumekuwa tukilaumu TANESCO na mamlaka za maji, nishati na kadhalika kwa kuwa athari zake zinaonekana Dhahiri. Mimi nasema, hii itawauma lakini kuna ndio namna ya kupima ufanisi wa TRA ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikionekana inafanya vizuri ilhali tunajua si kweli.

Angalizo
Njia ya kuongeza mapato sio lazima kuanza kutoza kodi Zaidi wale wasioweza kukwepa au kuongeza vyanzo vingine ambavyo vinaumiza uchumi. Ieleweke kwamba tafiti ya ActionAid ilionesha Tanzania inapoteza takribani Tsh. Trilioni 19 kila mwaka kutokana mambo mbalimbali ikiwemo misamaha ya kodi isiyo na tija, kesi za kodi zisizoisha, na mifumo mibovu. Ambapo tafiti hiyo imeonesha tukiweza kupata kodi hiyo, uwiano wa kodi na pato la taifa unaweza kufikia 28% hali ambayo itatuweka pazuri kiuchumi kwa kuwa tutakuwa na uwezo wa kuboresha huduma na kulipa madeni yetu vizuri ambayo kwa sasa yanaongezeka kila uchao. Soma tafiti hapa (https://tanzania.actionaid.org/sites/tanzania/files/publications/Sealing_the_gaps report.pdf)

Kuondoa misamaha ya kodi, kuweka sheria za kodi njema ambazo zitapunguza masuala ya kupelekana mahakamani mara kwa mara. Kutumia teknolojia, hasa internet kutaongeza mapato ya kodi kwa kuwa hata gharama ya kukusanya kodi itashuka. Yaani hatutahitaji kuajiri nguvu kazi kubwa na kikosi kazi kukusanya kodi ikiwa tumefanya namna ya kuchochea matumizi ya fedha zisizo cash, yaani malipo ya kimtandao nk.

Nina uhakika asilimia nyingi sana, kwamba tukienda kwa namna hii ya kuseti mipango, tutakuwa katika nafasi nzuri ya kuifanya TRA iwajibike kama taasisi nyingine na kuleta maendeleo kwenye taifa letu.
 
Kwanza kuna nipishane na wewe kidogo kwenye eno moja. Nachokifahamau Serikali kwa kupitia Waziri wa Fedha Bungeni hupeleka muswada wa mabadiliko ya sheria wa mwaka unaofata na kuweka malengo ya serikali ikiwa pamoja na makusanyo na matumizi.

Na hapo ndipo TRA wanapopewa share yao kwa kuwa ndiyo chanzo kikuu cha mapato ya serikali mgao wao unakuwa mkubwa kulinganisha na sekta zingine kama local Government n.k.

Hivyo napingana na wewe kuwa TRA wanajiwekea malengo wao siyo kweli kwa ufahamu wangu wao wanapewa nini wakusanye katika mwaka husika kupitia Muswada utakaopitishwa na Bunge letu.
 
Nilisema kura za majaji ndio zina nguvu.

Ona mwamba alipigiwa kura 3 na kaibuka mshindi😄😄
 
TRA makadirio yai ni
Estimated govt Tax revenue = last year collection x 1.5 - ulaji 30% of collected amount.
 
Mbona andiko la kawaida sana au ndio ile dhana ya majaji kuja na majina yao mfukoni.
 
Mbona andiko la kawaida sana au ndio ile dhana ya majaji kuja na majina yao mfukoni.
Majaji hawawezi kufanana uwezo wa kuchambua na kutoa maoni ya ubora.

Ukiona wameenda pamoja basi ujue hicho kitu kimeshawishi uchambuzi wa kila mmoja na kuyaweka maoni yao pamoja hatimaye yanakuwa kitu kimoja na kukubalika.

Pia kama sisi tunavyopiga kura hapa tukijua hili andiko ni nzuri kutokana na utashi wetu na wao inakuwa hivyo hivyo.
 
Kwanza kuna nipishane na wewe kidogo kwenye eno moja. Nachokifahamau Serikali kwa kupitia Waziri wa Fedha Bungeni hupeleka muswada wa mabadiliko ya sheria wa mwaka unaofata na kuweka malengo ya serikali ikiwa pamoja na makusanyo na matumizi.

Na hapo ndipo TRA wanapopewa share yao kwa kuwa ndiyo chanzo kikuu cha mapato ya serikali mgao wao unakuwa mkubwa kulinganisha na sekta zingine kama local Government n.k.

Hivyo napingana na wewe kuwa TRA wanajiwekea malengo wao siyo kweli kwa ufahamu wangu wao wanapewa nini wakusanye katika mwaka husika kupitia Muswada utakaopitishwa na Bunge letu.
Mwandishi nadhani hajasoma SP ya TRA ambayo anazo hizo projections zote tena si kwa kipindi fulani tu, bali kwa miaka kadhaa mbele.

Pia, nikubaliana na ww kwamba kiini cha wapi TRA watakusanya ni matokeo ya Sheria ya Finance inyopitishwa kila mwaka na BUNGE.
 
Back
Top Bottom