Namna Rais Samia alivyofanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri na watendaji wakuu

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
Na Mwl Udadis, Dodoma

Wakati watanzania tunaendelea kufurahia spidi ya Rais Samia katika kutekeleza miradi, kuboresha huduma za jamii, kukuza diplomasia, kuibua fursa za kiuchumi na kuvutia wawekezaji, Rais amefanya mabadiliko kwa timu yake ya utendaji, mabadiliko haya kwa kifupi yamebebwa katika dhana zifuatazo;

1.Taaluma na ubobezi;
Moja kati ya sifa inayoonekana katika eneo la teuzi za watendaji katika wizara kwa maana ya Katibu na Naibu K/Mkuu ni taaluma na ubobezi, hii ni kete muhimu ambayo inakwenda kuongeza ufanisi kwa 100%.

2.Uzoefu na uchapakazi;
Licha ya umahiri katika mizani ya kitaaluma, teuzi zote zinaonyesha kuwabeba zaidi wale wenye rekodi ya uzoefu na uchapakazi usiotia shaka, kete hii muhimu sana inakwenda kuchochea kasi na kuwapa tabu wazembe wasioelewa falsafa ya kazi.

3.Vijana na wanawake; Bila kujali Dini, ukabila au ukanda, Uteuzi umeonyesha nia ya dhati ya Rais kuwapa fursa vijana na wanawake wenye uwezo mkubwa ili waitumikie nchi yao. Usawa ni chachu ya maendeleo endelevu.

4. Kuondoa mazoea na urafiki;
Katika hotuba ya uapisho Mh. Rais amekazia sana jambo hili, ugomvi au mgongano wa kimaslahi kati ya watumishi wenye tamaa haina nafasi tena katika awamu ya sita, ni kazi tu. Kufanya kazi kwa mazoea kunaweza kukuondoa wakati wowote kazini.

5.Kasi na mabadiliko;
Moja kati ya jambo kubwa lililoonekana katika uteuzi ni kuwa ili udumu katika nafasi ya utendaji lazima uwe mwenye mawazo ya kimageuzi na kasi ya utendaji wako iendane na dira ya Rais Samia, hii ni kete muhimu katika kuifikia kesho iliyo bora kwa ustawi wa nchi yetu.

Mwisho,
lakini si kwa umuhimu napenda kuwapongeza watendaji wote mliopewa imani kubwa na Rais wetu kwa niaba ya watanzania. Chapeni kazi kuijenga Tanzania yetu. Tunataka maendeleo jumuishi yaliyo endelevu.
 
Na Mwl Udadis, Dodoma

Wakati watanzania tunaendelea kufurahia spidi ya Rais Samia katika kutekeleza miradi, kuboresha huduma za jamii, kukuza diplomasia, kuibua fursa za kiuchumi na kuvutia wawekezaji, Rais amefanya mabadiliko kwa timu yake ya utendaji, mabadiliko haya kwa kifupi yamebebwa katika dhana zifuatazo;

1.Taaluma na ubobezi; Moja kati ya sifa inayoonekana katika eneo la teuzi za watendaji katika wizara kwa maana ya Katibu na Naibu K/Mkuu ni taaluma na ubobezi, hii ni kete muhimu ambayo inakwenda kuongeza ufanisi kwa 100%.

2.Uzoefu na uchapakazi; Licha ya umahiri katika mizani ya kitaaluma, teuzi zote zinaonyesha kuwabeba zaidi wale wenye rekodi ya uzoefu na uchapakazi usiotia shaka, kete hii muhimu sana inakwenda kuchochea kasi na kuwapa tabu wazembe wasioelewa falsafa ya kazi.

3.Vijana na wanawake; Bila kujali Dini, ukabila au ukanda, Uteuzi umeonyesha nia ya dhati ya Rais kuwapa fursa vijana na wanawake wenye uwezo mkubwa ili waitumikie nchi yao. Usawa ni chachu ya maendeleo endelevu.

4. Kuondoa mazoea na urafiki; Katika hotuba ya uapisho Mh. Rais amekazia sana jambo hili, ugomvi au mgongano wa kimaslahi kati ya watumishi wenye tamaa haina nafasi tena katika awamu ya sita, ni kazi tu. Kufanya kazi kwa mazoea kunaweza kukuondoa wakati wowote kazini.

5.Kasi na mabadiliko; Moja kati ya jambo kubwa lililoonekana katika uteuzi ni kuwa ili udumu katika nafasi ya utendaji lazima uwe mwenye mawazo ya kimageuzi na kasi ya utendaji wako iendane na dira ya Rais Samia, hii ni kete muhimu katika kuifikia kesho iliyo bora kwa ustawi wa nchi yetu.

Mwisho, lakini si kwa umuhimu napenda kuwapongeza watendaji wote mliopewa imani kubwa na Rais wetu kwa niaba ya watanzania. Chapeni kazi kuijenga Tanzania yetu. Tunataka maendeleo jumuishi yaliyo endelevu.
We mwl badala utetee walimu wenzie wanakufa sana huko kwa Mujibu wa Mpwayunga unatetea walamba Asali?
 
Back
Top Bottom