Nakusudia kuanzisha Ranch/Kufuga ng’ombe wa nyama- Naomba ushauri

Je mbuzi unawasafiriisha kwa staili gani ?
Je hio mbegu ya mapacha ni nzuri kwenye kuongezeka uzito. Bei za hao wa Songea zipoje.
Changamoto ya mbuzi local kasi yao ya kuongezeka uzito ni ndogo Sana,faida yao ni kuzaa mapacha tu.Ukitaka mbuzi wanozaa mapacha na wanaongezeka uzito tafuta mbuzi wanoitwa Malya,wapo. Kwenye kituo cha utafiti cha mifugo cha Kongwa-Dodoma cha serikali,tatizo kuwapata unaweza kuweka oda Dec.2023 ukawapata Dec.2024 au usipate kabisa.
 
Kama Kuna mtu unayemfahamu Songea mwambie akutafutie,sipo huko, au subiri niwaulizie watu ninaowafahamu nikipata mawasiliano yao nitakupatia.Bei inategemewa 30,000-70,000 inategemea wakati gani wakati wa mavuno inapanda wakati wa mvua (kifuku)inashuka.
Ok! Nashukuru.Umenijuza mengi .
Naona mabanda yako mazuri kuna la kujifinza.
 
Mbegu ni jamii ya napier ila zenyewe ni hybrid.
Unapanda Kati ya shina na shina sm 50 na Kati ya mstari na mstari sm 70,kina cha shimo sm 30na upana wa shimo sm 20.View attachment 2838723View attachment 2838724View attachment 2838726View attachment 2838727View attachment 2838728View attachment 2838729

Unakata na kuwapa ng'ombe,mbuzi na kondoo au punda,pia yakiwa machanga kuku na sungura wanakula.
Yana 17%ya protini,yanafaa sana kwa ajili ya ng'ombe wa maziwa na kwa ajili ya unenepeshaji.

Hii nyasi ninayo ni nzuri sana. Vipi unapatikana wapi? Je unasafirisha?
 
Nawasalimu wote wana jukwaa,

Moja kwa moja kwenye hoja. Nakusudia kuanzisha ufugaji wa Ng’ombe, Mbuzi na Kuku.

Naomba kwa wenye uzoefu mnipe maoni yenu, hususani juu ya:

1. Mikoa sahihi kwa biashara hii
2. Faida na hasara za biashara yenyewe
3. Changamoto na fursa
4. Wanunuzi wakubwa wa ng’ombe na mbuzi wa nyama (soko)
5. Chochote ambacho unadhani natakiwa kulizingatia kabla ya kuingia mzigoni.

Natanguliza shukurani.
Mimi kama Range Scientist kutoka SUA nakuomba usome vizuri na ujibu maswali ya Malila (post #8) na yale ya Toofast (post # 9). Ukijibu hayo maswali vizuri utakuwa umepata andiko la mradi wa Ranch. Lakini Ranch haitakuwa na maana kama hautafanya beef cattle fattening. Na hapa cha kuzingatia, je! Ng'ombe utakuwa unazalisha mwenyewe hapo shambani au utakuwa unanunua waliokomaa tayari ili wewe ufanye kuwanenepesha tu? Ukitaka uwe na Ranch ya viwango tunaweza kukubaliana nikakutengenezea Ranch Planning (lakini hapa lazima ujipange maana kuna gharama). Ukishapata eneo nitakufanyia na rangeland inventories and monitoring kujua rangeland health and ecological integrity. Hapo nitakusaidia na kujua kama shamba lako linahitaji kupandwa nyasi upya au kuendeleza zilizopo? Pia kufanya herd projection, Karibu!
 
Mfugaji. .nguruwe 300 mpaka uende Indua kweli. Hao wanaliwa ndani ya wilaya moja teba hata wiki hawatoboi.
India na china uende ukifikisha nguruwe 5000 walau.
Eti kanasema kachinje nguruwe 10 per day ndiyo kapeleke China!
 
Unapanda mbegu au shina ?mbegu au shina. Kuna maswali pale hujayajibu.
Juncao na Napier grass zinapandwa kama miwa yaani zile cuttings zake. Vinakatwa vipande vipande vya kama futi 1 hivi! Hivyo ndivyo vinapimwa kwa kilo ambayo bei yake ni kati ya Tzs. 4000 -5000/= na kwenye kilo zinakuwa kama cuttings kati ya 10-16.
 
Vitu vya kuzingatia
1.upatikaji wa kutosha wa maji,pamoja na mifumo mizuri ya umwagiliaji Kwa ajili kukuzia shamba malisho

2.mbegu bora za wanyama,wanaoweza kufikia uzito mkubwa na wanaostahimili magomjwa

3.wafanyakazi wenye ujuzi(skilled)na wasio na ujuzi(non skilled(
Wenye ujuzi mfano :madaktari wa wanyama(doctor of veterinary medicine and animal health and production officers)
mafundi sanifu maabara ya wanyama(veterinary laboratory Technologist)
Wataalamu wa shamba malisho(range management officers)
Mhasibu(accountancy) na mtu wa uchumi(economist)
Mwendesha mitambo ya umeme mfano trekta
Mafundi mbalimbali mfano wa umeme,maji,magari na mashine

Wasio na ujuzi mfano:wachunga wanyama,
Walinzi wa Ranchi
Walimaji mashamba

4.Sehemu ya kisasa ya kuchinjia(abbatoir unit) au hata slaughtering slab si mbaya Kwa kuanzia

5.Eneo kubwa la ardhi lenye rutuba ambalo si chini ya ekari 1500

6.Mbegu bora Kwa ajili ya shamba malisho

7.Mpangilio mzuri wa njia pamoja na uzio kuzunguka mashamba malisho

8.Sehemu maalumu ya kuhifadhi wanyama wagonjwa Kwa muda fulani(quarantine area)

9.Sehemu ya kupandishia na kushushia wanyama kwenye Ranchi toka kwenye gari(Loading and unloading area)

10.Sehemu ya kutulizia au kushika wanyama(restraining area) Kwa ajili ya matibabu,uchunguzi au kufanya shughuli ndogo ndogo kama kukata au kupunguza pembe

Yote Kwa yote mambo yapo mengi lakini hayo ndo ya msingi zaidi
Safi
 
Huzo nyasi za kulisha ng'ombe 15 zinapandwa kwenye eneo la ukubwa gani ?
naombashesabu ya kupanda heka moja kwa mfugo mbuzi.
Ukiwachungia humo humo kwa mwaka mzoma watskula mbuz wangapi .
Mbuzi wa kienyeji walioshiba.
Mkuu kwa ushauri ukipanda usipeleke mbuzi au ng'ombe kula shambani, wakatie uwape ndani. Halafu ukikata majani usiwape on the spot wape baada ya masaa 48 kupunguza maji, ili wapate dry matter nyingi.
 
Mkuu kwa ushauri ukipanda usipeleke mbuzi au ng'ombe kula shambani, wakatie uwape ndani. Halafu ukikata majani usiwape on the spot wape baada ya masaa 48 kupunguza maji, ili wapate dry matter nyingi.
Nashukuru kwa ushauri ila bado sijaanza rasmi. Kuna mbuzi wanne tu nyumbani hao nomepewa na mzazi mpendwa.
Natarajia kuanza kuwanunua january.
Nomejifunza sana hapa. Nawashukuru kazi ipo kwangu kuwatafuta mbuzi eneo tayari ninalo la kutosha.
Nita update taarifa ntakapo anza.
 
Changamoto ya mbuzi local kasi yao ya kuongezeka uzito ni ndogo Sana,faida yao ni kuzaa mapacha tu.Ukitaka mbuzi wanozaa mapacha na wanaongezeka uzito tafuta mbuzi wanoitwa Malya,wapo. Kwenye kituo cha utafiti cha mifugo cha Kongwa-Dodoma cha serikali,tatizo kuwapata unaweza kuweka oda Dec.2023 ukawapata Dec.2024 au usipate kabisa.
Vip mkuu hao mbuzi malya hawapatikani sehemu nyingine tofauti na Kongwa Dodoma?
 
Shamba lipo Ruvu karibu na Mlandizi-Kibaha.
Mbuzi nafuga Isiolo nililetewa kutoka Kenya.
Mbuzi wanozaa mapacha niliwanununa Mbinga -Ruvuma
Kondoo nafuga Dorper.
Ng'ombe wa maziwa nafuga Friesian.
Ng'ombe wa nyama nafuga Boran.
Utakapokuwa tayari tuwasiliane 0756625286.
Broni anafikia uzito WA kilo elf 1 baada ya muda hani
 
Changamoto ya mbuzi local kasi yao ya kuongezeka uzito ni ndogo Sana,faida yao ni kuzaa mapacha tu.Ukitaka mbuzi wanozaa mapacha na wanaongezeka uzito tafuta mbuzi wanoitwa Malya,wapo. Kwenye kituo cha utafiti cha mifugo cha Kongwa-Dodoma cha serikali,tatizo kuwapata unaweza kuweka oda Dec.2023 ukawapata Dec.2024 au usipate kabisa.

Nitaenda kuwatafuta. Vipi bei zao?
 
Kuna wadau wamekushauri vyema sana hapo juu sizani kama kuna haja ya kusema sana kikubwa nakuombea kwa Mungu ufanikiwe hitaji lako na uweze kufikia malengo yako unayoyahitaji ktk ufugaji huo, fwata yote uliyo elekweza mengi yamesha semwa. Nakuongezea Moja wapigie MBOGO RACHESE wana programe ya mafunzo kwa wafugaji wachanga na wameimaliza last week 0784 785 784 Mulla, na uingie kwenye page yao ya Instagrame utaona na kujuwa ingine inaanza lini, Mungu akubariki sana.
Wako wapi mkuu?
 
Kama ni ng'ombe fugia kuanzia sumbawanga,mpanda,hasa katavi huko kuna maeneo.

Japo Ningependa ufuge nguruwe ni rahisi na chap chap.
Ndio focus yangu nikipata hela fulani. Nitaanza na eneo la wastan la kutosha nguruwe wasipungue 40. Baadae niwe na eneo la kufugia nguruwe wasipungue 400. Wakifikia 300 unaanza kuwatoa kwa order ya kila siku. Hapo unasafiri kutafuta soko kwenye hotel iwe India,china au hapa hapa nchini. Lengo ni kuchinja nguruwe wasiopungua 10 kila siku na kuwasafirisha
Wazo lako zuri, lakini nahisi 400 bado ni wachache sana kuwasafirisha nje. Kwa nini usifikirie kuwa na idadi isiyopungua 5,000 na kuendelea?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom