Nakuheshimu sana Mbowe, lakini sasa huwezi, wape vijana walete mawazo mapya

U
Mbowe ni kiongozi mzuri wa kisiasa katika taifa hili,pia amefanya kazi kubwa katika kuujenga upinzani mpaka hapa ulipofikia.

Mimi binafsi namuheshimu Mbowe kama mtu alie groom viongozi wazuri.Kwa bahati nzuri viongozi hao wanamaono ya hali ya juu.Amefanya kila mbinu safi na pia chafu ili kuikuza CDM.Na kwa kiwango kikubwa amejitahidi vyakutosha.

Amewaibua viongozi kama Mnyika,Mdee,Heche,Sugu,na wengine wengi.Katika mafanikio Mbowe aliyoweza kuyapata kwa kiwango kikubwa nikuaminika ndani ya chama.Mbowe amefanikiwa sana katika hili,chochote atakachosema,amua wanachama walio wengi watamuunga mkono.Na kwa hili kwakweli inafaa kumpongeza maana amewaweka wanachama wake pamoja.

Mbowe aionapo fursa lazima aitumie,tunafahamu ushawaishi alionao kwa kuwahamisha wanachama wengine,kutoka katika vyama vyao na kuingia chadema.Mfano wa wanachama alio wahamisha ni Lissu,Lwakatare,Lema,Msigwa,Prof Safali,Lowasa na wengine wengi.Kafanya yote hayo ili kuikuza taasisi anayoiongoza,kiukweli inapaswa apewe pongezi nyingi.

Lakini Mbowe amekuwa nikiongozi anaependa madaraka,hayupo tayali kuona akiongozwa na wengine hasa katika chama.Mbowe lazima atafakari mustakabari wa chama,atambue anataka sasa hivi kukipeleka chama wapi?.

Mbowe lazima atambue kwa miaka mitano ijayo hatoweza kuiongoza CDM kushika dola.Na pia lazima atambue ushawishi alio nao nje ya chama unazidi kushuka.Lazima kama kiongozi awe anajichunguza anapoelekea atafanikiwa zaidi au ataporomoka zaidi?.Kiukweli kwa maono yangu nafikiri Mbowe asipokuwa makini chama kitamshinda.

Sioni dalili zozote za Mbowe kuandaa viongozi watakao kuja kumrithi,na viongozi nao waona ndani ya chadema kiatu cha Mbowe kitawapwaya.Lakini nafahamu Mbowe anafanya haya yote kwa makusudi ili aendelee kuitawala Chadema miaka takribani 20 ijayo.

Mbowe amekuwa kiongozi asie na maono ndani ya bunge,Mbowe hajui katika bunge yampasa kufanya nini,kwa wakati gani.Mikutano nje ya bunge imepigwa marufuku,nasehemu pekee yakukijenga chama ni ndani ya bunge.

Tunapokuwa na kiongozi asie kuwa na maono yoyote katika kuzua mijadara bungeni,kuleta hoja binafsi bungeni,kutofahamu kanuni nyingi uendeshaji wa bunge,akili yake kutoona fursa haraka yakuzuia baadhi ya hoja bungeni huyo hafai kuwa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni(KUB).

Mbowe nafasi hii inakuchea,nafasi hii huiwezi,nafasi hii ya KUB wewe sio size yako.Lazima utafakari kwa makini nakukaa pembeni katika nafasi hii.Mbowe waachie vijana kama Myika,Lissu,Lijuakali,Bulaya,Mdee waongoze nafasi hii.

Tumeona namna ulivyoshindwa kuhimiri nafasi hii katika miaka mitano iliyopita.Umeshindwa kupeleka hoja binafsi zakudai tume huru bungeni.Umeshindwa kutambua kiu ya wanabadiliko wakweli huanza na nini ili kushika dola.

Mbowe kiukweli bila kumung'unya maneno nafasi hii huiwezi wape damu mpya nao tuone watatufikisha wapi.Sasa hivi hata kuuzungumzia ufisadi bungeni imekuwa kazi kwako,wape uongozi vijana ambao hawakushiriki kumleta Edo chadema.

Waanze kujenga na kurudisha hadhi ya chama bungeni,kama bunge la 2005-2010,ambapo liliendeshwa na hoja juu ya hoja.

Mbowe ninaheshimu mchango wako katika chama,lakini KUB kamwe huiwezi,wape vijana watuletee hoja tunazozihitaji.

Mimi nimetimiza wajibu wangu kwa kukueleza Mh Mbowe nafasi ya KUB achia na wengine.

Ewe mtanzania weka masrahi ya taifa mbele kwa kuwaeleza viongozi wako ukweli.

Note.
Sina kadi ya chama chochote,sio mpenzi wa chama chochote.

Ni mimi mjukuu wa Luhanyula.
Umetumwa na ccm wewe!kawaulize lumumba hawalali kila chaguzi % zinapungua sababu ya Mbowe.CUF wamepata wabunge bara sababu ya Mbowe.CUF wameshinda urais Zanzibar.Mbowe atakuwa mwenyekiti mpaka mkoloni mweusi ccm akimbie nchi
 
Sasa ipo tofauti gani kati ya CCM na Upinzani kama mwenendo ni ule ule mbowe miaka elfu kidogo yeye tu mwenyekiti na ana watu wake badala ya kuangalia ukweli wao ni kumtetea tu sawa na makofi ya wabunge wa CCM
 
Inamaana huoni mbele?
Mwenyekiti wa chama ajaye ni John Heche.
KUB kwa mujibu wa jumuiya ya madola (mfumo wa kibunge) ni lazima awe mwenyekiti wa chama kama ni miongoni mwa wabunge.Kwa hiyo hii nafasi haigombewi wala haitolewi kwa utashi wa mtu
asante kwa elimu nzuri mkuu!
 
U
Umetumwa na ccm wewe!kawaulize lumumba hawalali kila chaguzi % zna inapungua sababu ya Mbowe.CUF wamepata wabunge bara sababu ya Mbowe.CUF wameshinda urais Zanzibar.Mbowe atakuwa mwenyekiti mpaka mkoloni mweusi ccm akimbie nchi
Acha mawazo mgando kuamini kila mtu anae leta mada hapa katumwa na ccm.

Wengine hatuna kadi ya chama chochote kile,na mahali pakuleta maoni yetu ni hapa.

Hilo la Cuf hakuna mtu anae lipinga,na hakuna anae mwambia mbowe aachie uwenyiki wa CDM.Hapa tunamsihi tu atafakari kwa kina.Lakini kiini cha hoja ni Mbowe kuachia KUB uwape viongozi wenye maono zaidi bungeni.

Pia hakuna anae mkataza kuwa kiongozi mpaka "mkoloni mweusi" ccm ashindwe.Lakini tambua huruka ya binadamu huhitaji kuona sula mpya katika utawala wowote ule.

Na ndio mana wapo viongozi walio fanya makubwa katika nhi zao lakini mwisho wa siku waliachia madaraka kwa aibu.

Heshima alio nayo Nyerere ni kwa sababu alikuwa anasoma nyakati,nakujua watu wanahitaji nini kwa muda gani.

Ukweli ni kuwa Mbowe KUB imempwaya,ukweli lazima usemwe.
 
kiukweli niliwahi sema, viongozi wengi africa hujijenga wao wenyewee, hawajui ipo siku hawatokuwepo, hili ndilo lililogharimu taifa hili kwa kukosa viongozi makini na chanzo ni Nyerere.

Nyerere alijijenga mwenyewe ktk nchi, aliamini ataongoza Tz daima lkn siku anajiuzulu aliiacha nchi imepinda, hakuacha viongozi wenye itikadi ya kitaifa zaidi.

Mbowe naye hivyohivyo, pamoja na kwamba ni mchagga lkn kashindwa kuifanya chadema taasisi imara, uimara wa chadema ni wakupabda na kushuka.
Chama hakina makao makuu yanayoeleweka, hakina hata redio, gazeti.

Katika hili mbowe amepwaya, anaamini yeye ataishi daima hapa duniani.

Siku usipokuwa makini hata hao vijana unaowaongoza watakugeukaa.

Take care Mbowe.
 
U
Umetumwa na ccm wewe!kawaulize lumumba hawalali kila chaguzi % zinapungua sababu ya Mbowe.CUF wamepata wabunge bara sababu ya Mbowe.CUF wameshinda urais Zanzibar.Mbowe atakuwa mwenyekiti mpaka mkoloni mweusi ccm akimbie nchi
Kweli wewe Bongolala
 
Obama alipofika Ghana mara ya kwanza baada ya kushinda urais wa marekani alisema Ghana ndiyo nchi inayotoa dira na mwelekeo wa demokrasia katika Africa jamaa wakapiga makofi na kushangilia sana baadae akawaambia imetosha Africa kutengeneza Strong Men akataka Africa itengeneze Strong Institutions ambazo zitamfanya yeyote atakayekalia kiti cha uongozi ile taasisi inampa ndugu, uwezo, mamlaka na dira ya kutawala, akileta shida taasisi inamcheua sasa hapa kiongozi anajijengea uwezo ye mwenyewe na taasisi haina nguvu, watu wanafukuzwa kwenye taasisi kwa sababu wamepishana kimtazamo na kiongozi
 
U
Umetumwa na ccm wewe!kawaulize lumumba hawalali kila chaguzi % zinapungua sababu ya Mbowe.CUF wamepata wabunge bara sababu ya Mbowe.CUF wameshinda urais Zanzibar.Mbowe atakuwa mwenyekiti mpaka mkoloni mweusi ccm akimbie nchi
Chadema imepata wabunge kutegemea kura za CUF usilidanganye jukwaa mkuu. Pale ambako CUF na CHADEMA waliweka mgombea ccm wameshinda. Ukweli kwa sasa Mbowe ni Janga hapo chadema. Muda mrefu hili litadhihirika. Na kama Lowasa ana nia ya dhati ya kumtoa Magufuli ikulu. Lazima reform ifanyike uongozi wa juu wa Chadema.

Chama kina zaidi ya miaka 20 ofisi ya makaomakuu iko kama gofu lililotelekezwa na mkoloni. Watu wanaoona sawa kufanya kazi kwenye ofisi ya aina hiyo wanaweza vipi kuleta mawazo m badala.
 
Porojo tupu, hoja zile zile zilizoshindwa wakati wa MM's mnadhani leo zitasaidia?

Its time to shut up you puddy,

Kuna vyama vingi chagua kimoja unachoona kimefanikiwa zaidi ya Chadema ukishabikie.

Mbowe ni Mwenyekiti hadi amalize kipindi chake 2017 na tukiona anafaa tunamchagua tena, hakuna wa kutuzuia awe Jecha au Lukuvi.
 
Mbowe ni kiongozi mzuri wa kisiasa katika taifa hili,pia amefanya kazi kubwa katika kuujenga upinzani mpaka hapa ulipofikia.

Mimi binafsi namuheshimu Mbowe kama mtu alie groom viongozi wazuri.Kwa bahati nzuri viongozi hao wanamaono ya hali ya juu.Amefanya kila mbinu safi na pia chafu ili kuikuza CDM.Na kwa kiwango kikubwa amejitahidi vyakutosha.

Amewaibua viongozi kama Mnyika,Mdee,Heche,Sugu,na wengine wengi.Katika mafanikio Mbowe aliyoweza kuyapata kwa kiwango kikubwa nikuaminika ndani ya chama.Mbowe amefanikiwa sana katika hili,chochote atakachosema,amua wanachama walio wengi watamuunga mkono.Na kwa hili kwakweli inafaa kumpongeza maana amewaweka wanachama wake pamoja.

Mbowe aionapo fursa lazima aitumie,tunafahamu ushawaishi alionao kwa kuwahamisha wanachama wengine,kutoka katika vyama vyao na kuingia chadema.Mfano wa wanachama alio wahamisha ni Lissu,Lwakatare,Lema,Msigwa,Prof Safali,Lowasa na wengine wengi.Kafanya yote hayo ili kuikuza taasisi anayoiongoza,kiukweli inapaswa apewe pongezi nyingi.

Lakini Mbowe amekuwa nikiongozi anaependa madaraka,hayupo tayali kuona akiongozwa na wengine hasa katika chama.Mbowe lazima atafakari mustakabari wa chama,atambue anataka sasa hivi kukipeleka chama wapi?.

Mbowe lazima atambue kwa miaka mitano ijayo hatoweza kuiongoza CDM kushika dola.Na pia lazima atambue ushawishi alio nao nje ya chama unazidi kushuka.Lazima kama kiongozi awe anajichunguza anapoelekea atafanikiwa zaidi au ataporomoka zaidi?.Kiukweli kwa maono yangu nafikiri Mbowe asipokuwa makini chama kitamshinda.

Sioni dalili zozote za Mbowe kuandaa viongozi watakao kuja kumrithi,na viongozi nao waona ndani ya chadema kiatu cha Mbowe kitawapwaya.Lakini nafahamu Mbowe anafanya haya yote kwa makusudi ili aendelee kuitawala Chadema miaka takribani 20 ijayo.

Mbowe amekuwa kiongozi asie na maono ndani ya bunge,Mbowe hajui katika bunge yampasa kufanya nini,kwa wakati gani.Mikutano nje ya bunge imepigwa marufuku,nasehemu pekee yakukijenga chama ni ndani ya bunge.

Tunapokuwa na kiongozi asie kuwa na maono yoyote katika kuzua mijadara bungeni,kuleta hoja binafsi bungeni,kutofahamu kanuni nyingi uendeshaji wa bunge,akili yake kutoona fursa haraka yakuzuia baadhi ya hoja bungeni huyo hafai kuwa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni(KUB).

Mbowe nafasi hii inakuchea,nafasi hii huiwezi,nafasi hii ya KUB wewe sio size yako.Lazima utafakari kwa makini nakukaa pembeni katika nafasi hii.Mbowe waachie vijana kama Myika,Lissu,Lijuakali,Bulaya,Mdee waongoze nafasi hii.

Tumeona namna ulivyoshindwa kuhimiri nafasi hii katika miaka mitano iliyopita.Umeshindwa kupeleka hoja binafsi zakudai tume huru bungeni.Umeshindwa kutambua kiu ya wanabadiliko wakweli huanza na nini ili kushika dola.

Mbowe kiukweli bila kumung'unya maneno nafasi hii huiwezi wape damu mpya nao tuone watatufikisha wapi.Sasa hivi hata kuuzungumzia ufisadi bungeni imekuwa kazi kwako,wape uongozi vijana ambao hawakushiriki kumleta Edo chadema.

Waanze kujenga na kurudisha hadhi ya chama bungeni,kama bunge la 2005-2010,ambapo liliendeshwa na hoja juu ya hoja.

Mbowe ninaheshimu mchango wako katika chama,lakini KUB kamwe huiwezi,wape vijana watuletee hoja tunazozihitaji.

Mimi nimetimiza wajibu wangu kwa kukueleza Mh Mbowe nafasi ya KUB achia na wengine.

Ewe mtanzania weka masrahi ya taifa mbele kwa kuwaeleza viongozi wako ukweli.

Note.
Sina kadi ya chama chochote,sio mpenzi wa chama chochote.

Ni mimi mjukuu wa Luhanyula.

Nani aliyekuambia kwamba Mbowe ana mpangowa kuendela kuwa kiongozi wa CDM kwa miaka mitano ijayo?
 
Ndio demokrasia mkuu,hakuna anae katazwa kumuunga mkono kiongozi yeyote yule.Lakini KUB imempwaya Mbowe.
Kama ilivyopwaya nafasi ya Spika Ndugai,Naibu Spika Tulia,M/kiti Chenge na msaidizi wake Mary Mwanjerwa unategemea nini hapo kuna hoja yoyote itajadiriwa kwa maslahi ya Taifa.
 
Kosa kubwa la Mbowe CHADEMA ni chama kutokuwa na Media mpaka leo hii wala kutomikili majengo yake yenyewe na kutokuwa na asset nyingi zisizohamishika.

CHADEMA walipaswa kuwa na ofisi zao(majengo yao) kwa baadhi ya mikoa au hata mikoa yote.Hili jambo la chama kushindwa ku-invest mpaka leo hii mimi halinifurahishi kabisa.
kamanda unachekesha. wajenge majengo au kuwa na TV kwa manufaa ya nani ? wewe unaona pale kuna mtu anayeshughulikia maslahi ya taifa au wananchi. wengi wao ni wasaka noti tuu.kwa faida yao na familia zao
 
kiukweli niliwahi sema, viongozi wengi africa hujijenga wao wenyewee, hawajui ipo siku hawatokuwepo, hili ndilo lililogharimu taifa hili kwa kukosa viongozi makini na chanzo ni Nyerere.

Nyerere alijijenga mwenyewe ktk nchi, aliamini ataongoza Tz daima lkn siku anajiuzulu aliiacha nchi imepinda, hakuacha viongozi wenye itikadi ya kitaifa zaidi.

Mbowe naye hivyohivyo, pamoja na kwamba ni mchagga lkn kashindwa kuifanya chadema taasisi imara, uimara wa chadema ni wakupabda na kushuka.
Chama hakina makao makuu yanayoeleweka, hakina hata redio, gazeti.

Katika hili mbowe amepwaya, anaamini yeye ataishi daima hapa duniani.

Siku usipokuwa makini hata hao vijana unaowaongoza watakugeukaa.
hi
Take care Mbowe.
Mkuu asante kwa mchango wako.Ingawa GADAFI alifanya mazuri mengi kwa nchi yake lakini bado kuna wananchi walimuona muda wake umekwisha.Walipopata pakuanzia basi ndo ikawa kama ilivo leo hii huko Libya.

Porojo tupu, hoja zile zile zilizoshindwa wakati wa MM's mnadhani leo zitasaidia?

Its time to shut up you puddy,

Kuna vyama vingi chagua kimoja unachoona kimefanikiwa zaidi ya Chadema ukishabikie.

Mbowe ni Mwenyekiti hadi amalize kipindi chake 2017 na tukiona anafaa tunamchagua tena, hakuna wa kutuzuia awe Jecha au Lukuvi.
Mkuu Mbowe KUB inampwaya,Lazima tuseme ukweli ingawa haupendwi kusikiwa na wengi.
 
mark my words:CHADEMA isipochukua nchi mwaka huu(2015) itachukua miaka mingi sana kuchukua nchi (mbowe 2015). sasa cdm hajachukua nchi lowasa anasema amepoteza mchezo si pambano tukutane 2020. kwa nini wanachadema wanafail kufanya tasimini sababu ya kushindwa kwao kabla hawajawaaminisha wafuasi wao kuwa watashinda uchaguzi? mtoa mada umewapa mwanga japo ni vigumu kutekeleza coz mbowe ni cdm na cdm ni mbowe....
 
Back
Top Bottom