Nakaribisha maswali kuhusu Tiba / Dawa

Gorgeousmimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
9,296
7,662
Hellow wapendwa,

Nakaribisha maswali yoyote kuhusu dawa zozote zenye active ingredients (DRUGS). Kama una maswali kuhusu matumizi yake, matumizi yake pamoja na dawa nyingine, vyakula (interactions), athari zake (side effects) au hata kama unataka kujuzwa jinsi dawa inavyofanya kazi kutibu ugonjwa!!

Karibuni sana.

A

Swali
Nashukuru sana nina maswali 3
1. Nini tofauti kati ya Diabetes type-1 na diabetes type-2
2. Je, kwanini mtu mwenye diabetes type-2 anashindwa kufanya vizuri tendo la ndoa na nini dawa yake?
3. Je, kama tatizo limesababishwa na over weight. Je, akipunguza tatizo linakuwa limeisha?au kuna dawa anatakiwa kutumia pia?

Jibu
Hello chasuzy!
  • Diabetes type 1 inasababishwa na mwili kutokuwa na production ya insulin,hali hii mtu anazaliwa nayo na inaweza kuwa genetic pia.Wagonjwa wa diabetes type 1 wanahitaji sindano za human insulin.Diabetes type 1 haina tiba unatakiwa uchome sindano ya insulin maisha yako yote.


  • Diabetes type 2 wanakuwa na production ya insulin lakini si ya kutosha.Kitu kingine ni insulin resistance( jinsi unavyokula vyakula vya sukari/unhealthy ndivyo mwili unajaribu kuproduce insulin ili kuvunjavunja hio sukari na baada ya muda kwasababu ya overproduction uzalishaji wa insulin inapungua),mapungufu ya insulin receptors,matatizo ya insulin binding au insulin receptor haipati signal za kutosha.Diabetes type 2 unaweza kupona ukibadili lifestyle kwa kula vyakula healthy,kufanya mazoezi,na kujitibu ipasavyo.Usipofata tiba kwa uyakinifu unaweza kupata complications kwenye viungo vingine kwasababu sukari inaathiri nerves na mishipa ya damu mfano ya macho, pia mafigo.Kitu kingine ni pia wenye diabetes type 2 wanaweza kuworsen na kwenda kwenye diabetes type 1 kwasababu uzalishaji wa insulin unapungua na hatimae kupotea kabisa.


  • Nimegusia complication za diabetes kuwa zinaweza kuathiri nerves na mishipa ya dam na inahusiana na mishipa ya uume, ya miguu na kusababisha (diabetic foot)-unakosa sense kwenye miguu kwa sababu nerves ziko damaged au kuathiri mishipa miyembamba ya dam ya macho na kupeleka kutokuona vizuri hatimae upofu.


  • Insulin ni hormone inayotengenezwa kwenye pancreas.Kwa lugha nyepesi naweza kusema ni ufungo kwasababu insulin inasafirisha sukari kutoka kwenye damu na kwenda kwenye cells za mwili.Na pia inavunjavunja glucose to glucagon.
View attachment 236428

B
Swali
1: Mkuu,naomba kujua kama kuna permanent pharmacological remedy for masterbation-induced premature ejaculation,loss of morning erections and weak erections

2: Ni astringent gani nzuri itumike in management of external hemorrhoids

Jibu

Tunapopata msisimko wa kimwili, nerve impulses zinatumwa kutoka kwenye ubongo kwenda kwenye corpus carvenosa, ambapo signal substance Nitrogen monokside(NO) inazuia kuvunjwavunjwa kwa GTP(Guanine-5-triphosphate) - cGMP(Cyclic Guanine monophosphate) inayosababisha muscles zirelax na uume usimame.
  • Ili uume usimame ipasavyo venes must be compressed.Compressionmechanism ikiwa defect erection inapotea partially au totally kwasababu kunakuwa na venous leckage.
  • Kitu kingine ni nerveimpulses nilizozitaja kwenye first paragraph(sympathic and parasympathic motor neurons) zinaweza kuwa disturbed na kupeleka weak erection n.k So through masterbation you could triggering reflexes too often uncautionally or defeating compression mechanisms.
  • And these are just my speculations.Hakuna direct scientific explanation how can masterbation prior to premature ejaculation.
  • Unaweza kutumia scheriproct/alcos anal suppositories/cream kama management ya external hemorrhoid!

C
Swali
Asante kwa mada hii

Nina maswali

1. Nini dawa ya constipation?

2. Nina ndugu yangu mwanamke amejifungua mwezi mmoja uliopita anapata constipation ambayo inampelekea kutokwa na damu wakati wa kujisaidia haja kubwa, tatizo ni nini? dawa gani zitamsaidia kumbuka ananyonyesha?

3. Madhara ya constipation na/au hemmoroids ni yapi kwa mwanamke?

Jibu
Pole kwa kukusubirisha dia,Maswali yako yanahitaji majibu yenye maelezo mengi ndio maana nikachukua muda nilotulia ili kukujibu.

Dawa za constipation zipo tofauti kutokana na aina ya constipation,umri wa mtu na sababu za constipation.

Constipation inasababishwa na kupungua kwa bowel movements kwasababu ya kukosekana kwa fibers za kutosha kulainisha choo au kutokuwa na fluids za kutosha kwenye utumbo mpana.

Constipation imegawanyika katika makundi mawili makubwa nayo ni Primary constipation au secondary consitpation.

  • Primary constipation inasababishwa na mabadiliko katika lifestyle mfano hunywi vimiminika vya kutosha,kutokula vyakula vyenye fibers nyingi,kutokuwa physically active au ukiwa na irritable bowel syndrome.
  • Secondary constipation inasababishwa na kuwa constipate kwa muda mrefu na inatokana na magonjwa kama cancer coli,hormon and electrolye imbalance as well as drugs like opoids.Dawa kama opoids(morfin,codein like ukila kwa muda mrefu daily unaondokana na constipation.
  • Kuna tiba tofauti nazo ni:

  1. Emollient agents:Hizi agents zinajiunga na maji yaliyopo kwenye utumbo mpana na kuongeza volume ya contents zilizopo kwenye utumbo na kulainisha choo.Inachukua siku kadhaa mpaka upate choo cha kawaida na inaweza kutumika kwa muda mrefu bila ya kuwa na madhara kwenye mwili.
  2. Hyperosmotic laxatives:Hizi products zinasaidia kuzuia maji kwenye utumbo yasiwe absorbed kwenye mwili yaani vina absorb,kuongeza contents ziliopo kwenye utumbo na hence kuongeza colonic peristalsis mfano ni lactulose,
  3. Stimulant agents :Hizi agents zinafanya kazi kwenye kwa kujiunga kwenye receptor iliyopo kwenye utumbo.Zipo in tablets and supporitory form,Supporitory inafanya kazi within 20mins,tablets within 12hrs na inapaswa ule usiku ili upate choo siku ya pili yake.Dawa hizi hazitakiwi zitumike kwa muda mrefu kwasababu zinaweza kusababisha utumbo kutengeneza addiction. mfano bisacodyl,senna extract
  4. Lubricant agents:Hizi ni agents zenye kama mafuta mfano paraffin zinasaidia kulainisha choo
  5. Bulk-forming agents:Inaweza kuwa matunda yalokaushwa,whole grains(lin seeds, n.k Vitu kama hivo vinalainisha choo na kusaidia kutoka kwa urahisi
  6. Enema:Hizi ni fludis zinazoweka kwenye sehem ya hajakubwa,ziko chupa kubwa na ndogo.Kubwa ni kwaajili ya kuempty haja zote hasa kama uenda kufanyiwa examination ya utumbo.Ndogo zinatumika kwaajili ya kusaidia choo kitoke kwa urahisi.Ziko zenye mafuta pia. mfano(bisacodyl,microlax, lauryl sulphate,glycerol)
View attachment 236591

Dawa ninayomshauri kutumia ni lactulose au bulk forming agents kwasababu ananyonyesha akila dawa zingine kuna uwezekano ziende kwenye maziwa.Inachukua muda kama wa siku 2-3 kabla hajapata effect ya lactulose.

Namshauri pia ni vyema akinywa vimiminika vya kutosha na kula vyakula vyenye fibers nyingi.

Hali ya yeye kutoka damu ni kiashiria kama choo ni kigumu na inawezekana ana bawasili(haemorrohid).Anaweza kutumia alcos-anal haipiti kwenye maziwa mtoto akinyonya.

D
Swali
Dokta pia nina maswali mawili kama ifuatavyo:

1. Swali toka kwa mke wangu.

Yeye idadi ya siku zake za hedhi haziko fixed. Zina-fractuate mara kwa mara. Zina-range kati ya 33 hadi 60. Yaan mwez huu zaweza fika 45 wakti mwezi ulopita zilikuwa 36 na mwezi ujao zaweza fika 54. Inatupa shida kupanga uzazi kwa kutumia karenda. Je, tatizo laweza kuwa nini? Na je kuna tiba?

2. Swali toka kwa msaidizI wetu wa kazi tunayeishi nae hapa nyumbani.

Yeye huwa anaishiwa nguvu kiasi cha kushindwa kufanya kazi zake za ndani ambazo ndizo alizoajiriwa kuzifanya. Tulimpeleka hospital kufanya checkup lakini hakukutwa na tatizo.

Huwa anapungukiwa sana na damu. Tukampima na sickle cell lakini pia kipimo kilionyesha hakuwa na sickle cell.

Kuna dokta alinambia huenda ana tatizo la kupoteza damu nyingi wakat wa hedh. Nilipomuuliza na baada ya kumfaniyia study, nikapata jibu kuwa ni kweli anatokwa na damu nying wakt wa hedh.

Study yangU niliifanya kwa kumchorea graph na nikagundua kuwa kila tarehe zinazofanana kwa kila mwez ndio hupatwa na tatizo lake linalomsumbua pamoja na maumivu makali ya tumbo.

Kupunguza tatizo la kuishiwa damu nikamuanzishia dozi ya dawa ya kuongeza damu. Namnunulia chupa mbili za dawa ya kuongeza damu (iron tonic ama hemovit), moja anaitumia katikati ya mwezi na nyingine anaitumia anapokaribia kuingia ktk hedhi.

Mwez huu umepita salama, sikumsikia akilalamika kusikia kizunguzungu na kuishiwa na nguvu. Limebaki tatizo la maumivu ya tumbo.

Je, tatizo lake la kupoteza damu nyingi wakat wa hedhi linatibika? Ama ndio atatakiwa awe anakunywa dawa za kuongeza damu kila anapokaribia kuingia ktk hedhi?

Jibu
Mkuu huyo dada wa kazi anatatizo linaloitwa MENORRHAGIA:Anaweza kutibiwa na vidonge vya uzazi wa mpango hio ni alternative moja.

Nyingine ni antifibrolytics kama tranexamic acid ni inhibitor ya fibrinolysis ili kupunguza kiwango cha damu kinachotoka au NSAID´s mfano ibuprofen au naproxen.

Mkeo ana tatizo linaloitwa OLIGOMENORRHEA:Hedhi inayokaa kati ya siku 35-miezi 6
Inasababishwa na aidha failure kwenye

  • Pitutary gland kupelekea low levels of estradiol,low FSH(Follicle stimulating hormone)/LH(Leutenizing hormone),au
  • Failure kwenye ovaries kupelekea low levels of estradiol,high FSH/LH,
  • Polycystisk ovranian syndrome(PCOS),
  • Kuzaliwa na mapungufu kwenye viungo vya uzazi.
  • Hypo/hyperthyroidism.

Tiba ni kwa Gondotropines au clomifen inayo induce gonadotropinrelease na ovulation baada ya kupata right diagnosis.
Diagnosis inatolewa kwa hormone analysis ya estradiol,FSH,LH,Prolactin na TSH.

E

Swali
Prednisolone Tablets,zinafanye kazi na side effects zake ni zipi?

Natanguliza shukrani.

Jibu

Prednisolone ni sythethic glucocorticoid ambayo inafanya kazi kwa kustimulate glucocorticoid receptor iliyopo kwenye cells tofauti za mwili.Glucocorticoid inapunguza inflammation response:Inapunguza inflammation kwa kupitia vyanzo kadhaa mfano inapunguza release ya chembechembe zinazosababisha inflammation itokee.

Glucocorticoid inatengenezwa pia mwilini kwenye adrenocortopic hormone.Ukiwa unatumia glucocorticoid bila mpangilio hasa systemic inasababisha negative feedback kwenye kwahio uzalishaji wake kwenye pitutary glands una pungua.

Unaweza kuepka hilo kwa kula dawa wakati wa asubuhi kwasababu production ya cortisol mwilini inakuwa juu asubuhi ili kuepuka adrenal suppression
.Na ukiwa unataka kuacha kutumia dawa unaacha kwa kuwithdraw taratibu kwa wiki kadhaa,ukiacha ghafla tu mwili hautopata muda kwa kuanzisha utengenezaji wa glucocorticoid kama awali kwenye pitutary glands na inaweza kupeleka dalili za ukosaji wa glucocorticoids ambayo hupeleka maumivu kwenye joints and muscles.

Glucocorticoid inafanya kazi kwenye baadhi ya viungo kama mifupa inazuia osteoblast kwenye bone tissue na kupeleka kuongezeka kulika kwa bone tissue na kupeleka kusababisha ugonjwa kama OSTEOPOROSIS ni sideeffect mmojawapo ya matumizi ya glucocorticoid kwa muda mrefu.Na ndio maana tunashauri ukiwa unatumia prednisolone kwa muda mrefu ule calcium tablets with vitamin D[SUB]3[/SUB] ili kuepuka chances za kupata Osteoporosis,Calcium inasaidia kujenga mifupa kuwa imara na Vitamin D[SUB]3 [/SUB]inaongeza absorption ya calcium kutoka kwenye utumbo mpana.
Effects nyingine ni kama metabolic effects:Kuongezeka kwa sukari(bloodsugar),Tendency ya kupata infection haswa ukiwa unatumia dozi kubwa inasababisha immunosuppressive effect.Na kuongeza tendency ya kupata viralinfecton kama herpes au fungiinfection kama candida.

Side effects ziko tofauti nimeshaorodhesha osteoporosis na high bloodsugar/diabetes juu lakini ukumbuke zinapatikana baada ya matumizi ya muda mrefu na nyingine ziko kwenye picha niloiweka.
View attachment 236146
Dawa hii inatumia kutibu magonjwa mengi mno kuanzia astma/chronic obstructive pulmonary disease,allergies,reumathoid arthithis,mpaka cancer(in combination with other drugs).Kama ilivyo kila dawa kuna faida na kuna hasara.

Tukipata tiba tunaipa kipaumbele afya yetu na ugonjwa unaotukabili.Side effects zina variety na ziko individual si kila mtu atapata athari nilizoorodhesha ila ni possibilty.Usiache kutumia dawa bila kushauriana na watu wa afya.Uwe na siku njema.

F
Swali
Dr. naomba kujua dawa ambazo zinaongeza hormone za kiume na side effects Zake, shukurani

Jibu
Athari ziko tofauti mkuu kutokana na aina ya tiba unayopata,muda wa tiba,umri wa muhusika na jinsia.Nakuorodheshea athari zinazoweza kuwapata jinsia ya kiume:
  • Chunusi ni side effect mmojawapo ya kawaida
  • Salt and water retention,inaweza kusababisha muongezeko wa mwili hasa mwanzoni mwa tiba na hata wa madini ya calcium mwilini
  • Mabadiliko kwenye gender character na sexual impairment:Hii inaweza kuuwa direct and indirect impairment ya kwenye genitals na kwenye mfumo wa uzazi.Mfano direct stimulation inaweza kusababisha prostatic hypertrophy na hata kusababisha prostate cancer.High doses inaweza kusababisha uume kusimama muda mrefu na kuuma (priapism).Extreme high doses zinasababisha pia release ya gonadotropin kuzuilika kutoka kwenye pitutary gland na kupelekea mapungufu kwenye uzalishaji wa mbegu za kiume na hata ugumba.
  • Athari zinaweza kwenda vice versa pia na kusababisha feminism mfano gynecomastia(kuota kwa matiti kwa wanaume.Hii inasababishwa na kuvunjwavunjwa kwa androgens kwenda kwa estrogen ambayo inachochea ukuaji wa matiti.
  • Alopeci ni athari nyingine:Huu ni ugonjwa wa kukosa vinyoleo mwilini
  • Mabadiliko ya kisaikolojia ni kawaida:Kuongezeka kwa ham ya kukutana miwili au kupungua(libido)
  • Psychotic reactions kama depression,aggression kwa utumiaji ulokithiri
  • Hepatotoxicity(sumu kwenye ini)
  • Matatizo kwenye moyo,inaongeza LDL-cholesterol,inaweza kusababisha heart attack ukizidisha matumizi
  • Hematological changes:Kuongezeka kwa chembechembe nyekundu za damu.Na hii inasababishwa na uwezo wa androgen kustimulate erythopoesis.
  • Kuongezeka kwa misuli na hii huweza kusababisha rupture kwenye misuli .Chronic fibromyalgia
 
Thanks Mkuu. Hivi diazepam vipi ufanyaji wake wa kazi mwilini.
Diazepam iko classified kama benzodiazepinederivate. Benzodiazepines zinajiunga kwenye receptor mwilini iliyopo kwenye ubongo inayoitwa GABA-receptor.

Na inasababisha muongezeko wa inflow ya chloride ions kwenye nervecells.Matokeo yake inapooza baadhi ya parts za ubongo. Hali hio inaweza kuleta;

Pshycological effects
: Nazo ni anxiety withdrawal au sedative effect (kusaidia mwili urelax kama mfano unatakiwa kufanyiwa surgical procedure)

Hypnotical effect:
Inachosha ubongo kwahio inaweza kutumika kama sleeping inducer (dawa ya usingizi), Au inaweza kutumika kama muscel relaxer na kusaidia na cramps/spasms!
 
Vipi sedenaflin hufanya kazi?

Unamaanisha sildenafil(VIAGRA)? Sildenafil ni PHOSPHODIESTERASE-5-INHIBITOR. Kazi yake ni kuinhibit/kuzuia enzyme phosphodiesterase type-5(PDE5) kwenye corpus carvenosum(sehem ya uume), Corpus carvenosa ni part ya erectile tissue iliyopo kwenye uume inayohifadhi damu kwenye uume unaposimama.

Tunapopata msisimko wa kimwili, nerve impulses zinatumwa kutoka kwenye ubongo kwenda kwenye corpus carvenosa, ambapo signal substance Nitrogen monokside(NO) inazuia kuvunjwavunjwa kwa GTP(Guanine-5-triphosphate) - cGMP(Cyclic Guanine monophosphate) inayosababisha muscles zirelax na uume usimame.

Kumbuka cGMP inavunjwavunjwa na PDE5. Kwahio PDE5 ikiwa inhibited na phosphodiesterase inhibitor/sildenafil kunakuwa na muongezeko wa cGMP inayosababisha uume kusimama.
 
Nini ushauri wako kuhusu matumizi ya sedative compounds?
Sedative compounds zinatakiwa zitumike kwa umakini na si kwa muda mrefu kwasababu zinasababisha TOLERANCE na ADDICTION.Nikisema TOLERANCE namaanisha unahitaji kuongeza dosage kila baada ya muda ili kupata effect ya dawa.

Inaweza kusababisha pia "hangover" unalala bila ridhaa yako mchana mfano ukiwa unaendesha gari n.k Hali hio inaweza kuwatokea hasa watu wazima >65 yrs kwa sababu wao wanamuongezeko wa apidose tissue, sedatives hasa benzodiazepines zinajikusanya hapo na kuwa released taratibu kwenye damu over time/mchana. Na ndio maana half life yake hasa benzo kwa watu wazima ni ndefu kuliko kwa vijana.
 
gorgeousmimi

Kuna compound mbili zilizo katika fungu la sedatives of which mara nyingi wanachomwa watu walio katika death row...naomba kujua ethics za kitabibu katika upatikanaji wake! Kama hutojali nitakuuliza swali la nyongeza baada ya jibu lako zuri Mheshimiwa!
 
Last edited by a moderator:
Nasumbuliwa na chunusi sugu.
Nina umri wa miaka 31.
Nimejaribu kubadiri dawa za tube za kupaka pamoja na sabuni lakn bado chunusi kubwakubwa zinazidi,wengine wanasema labda kuna uchafu kwenye damu!
nimepima vipimo vyote ikiwemo HIV hakuna!
Naomba ushauri..
Natanguliza shukrani!
 
gorgeousmimi

Kuna compound mbili zilizo katika fungu la sedatives of which mara nyingi wanachomwa watu walio katika death row...naomba kujua ethics za kitabibu katika upatikanaji wake! Kama hutojali nitakuuliza swali la nyongeza baada ya jibu lako zuri Mheshimiwa!
Samahani mkuu sitoweza kujibu swali lako uloliuliza na nina sababu kadhaa nitakazokuainishia kama vielelezo.
  1. Sijui unataka kujua kuhusu lethal injection kwaajili gani na kwa dhamira gani,you could be suicidal na mimi kukujibu naweza kuwa ndo nakupa tiketi ya kujimaliza au wengine wenye dhamira hio kuitekeleza.
  2. Jinsi itakakavyo athiri watu hapa JF doctor,kwasababu kuna watu wa aina tofauti na wenye utawa tofauti wa kufikiri!Utanisameh kwa hilo!
Niko against ACTIVE DEATH so sitojihusisha na suala hilo in any matters!
 
Naomba kufahamu athar ya matumiz mabaya ya vidonge vya uzaz wa mpango
Sina uhakika kama nimekuelewa swali lako ipasavyo lakini nitajitahidi nikujibu kadri niwezavyo.Vidonge kwa uzazi wa mpango vinatakiwa vitumike aidha kwenye mzunguko mzima wa siku 28 au siku 21,kisha mapumziko ya wiki ambapo mwanamke anapata hedhi.

Matumizi mabaya kwa uelewa wangu itakuwa aidha huvili ipasavyo au unavila kwa wingi.Kama huvitumii ipasavyo hutopata ile kinga unayotarajia kupata kutoka kwenye vidonge hivo.Itaongeza risk ya mtu kupata athari kama kichefchef,kubadilika kwa mpangilio wa siku za hedhi,maumivu kwenye matiti,mood-swings,kupungua kwa hamu ya tendo.

Longer term effects ni tromboembolisme(inahusiana na urithi zaidi),Ovarian cancer n.k
 
nini dalili na tiba sahihi ya U.T.I
Hellow utaifakwanza,
Dalili za U.T.I ni maumivu wakati wa kwenda haja ndogo(hali ya kama kuwakwa na moto ukijisaidia) na kwenda chooni mara kwa mara.Ni muhimu kabla hujaanza na tiba yoyote vichukuliwe vipimo vya mkojo ili kuhakikisha kama una U.T.I na ni ya aina gani!!
DAWA AMBAZO ZINAWEZAKUTUMIKA NI ANTIBIOTICS
  1. Trimetoprim
  2. Mecillinam/Pivmecillinam
  3. Nitrofurantoin
  4. Inaweza kutumika pia aminopenicillins kama amoxicillin!
 
Samahani mkuu sitoweza kujibu swali lako uloliuliza na nina sababu kadhaa nitakazokuainishia kama vielelezo.
  1. Sijui unataka kujua kuhusu lethal injection kwaajili gani na kwa dhamira gani,you could be suicidal na mimi kukujibu naweza kuwa ndo nakupa tiketi ya kujimaliza au wengine wenye dhamira hio kuitekeleza.
  2. Jinsi itakakavyo athiri watu hapa JF doctor,kwasababu kuna watu wa aina tofauti na wenye utawa tofauti wa kufikiri!Utanisameh kwa hilo!
Niko against ACTIVE DEATH so sitojihusisha na suala hilo in any matters!

Umekuwa too defensive anyway! Labda ethics zinakutaka hivyo!

Nitumie fursa hii pia kukupongeza kwa kuamua kutumia taaluma yako kutoa ushauri wa matumizi sahihi ya dawa. Ni imani yangu pia watatokea na wengine wenye taaluma nyingine ambao wataanzisha miraba yao ya ushauri humu...
 
Duphastone naomba jua kazi yake kwa mjamzito??na salbutamol pale anapopewa mtu ambaye mimba inatishia kutoka!!!
 
51 Reactions
Reply
Back
Top Bottom