Naishi nikisubiri kifo, nimechoka sana

Mashaurijr

JF-Expert Member
Oct 8, 2016
639
1,020
Wakuu habari za mihangaiko,

Kiufupi nimechoka sana. Maisha yangu siyaelewi nimepambana vyakutosha, nimejitesa sana ili nipate mafanikio badala yake nimepata shida nyingine vidonda vya tumbo au ulcers.

Nime hustle sana nikawa bize mpaka nikaachika na mpenzi wangu niliyempenda sana lakini wapi, kila nikipiga hatua tatizo linatokea narudi nyuma.

Nimepaniki sana, nimekuwa nakunywa pombe hatari ila bado naona kama haziwezi kunisahaulisha. Natumia kijiti ila bado naona kama hakifanyi kazi vizuri kunisahaulisha malengo niridhike tu na maisha ya kawaida lakini wapi, mimoshi tu inaniletea kikohozi bure.

Sikutamani kabisa nife sijamiliki gari kali mabiashara makubwa mjengo wa maana, ila sasa naona kukata tamaa kukinifunika, bangi zikinikolea, madawa ya kulevya na kifo kikija mapema, na moto mkali wa jehunum ukinichoma kwa madhambi yangu.
 
Kuna mwenye magari na magorofa ila hana afya na hawezi kula vyakula akajiachia akafurahi.
Kama huombi barabarani una pa kulala na unaweza kusimamia na kujitosheleza milo yako mitatu, kama una uwezo wa kujinunulia dawa au kujipeleka hospitali ukiumwa ....mshukuru Mungu maana wapo ambao hata leo wameshinda njaa hawajala.

Kama bado una miguu miwili na mikono, una akili, huna ugonjwa sugu au ugonjwa mkubwa wa kukufanya ushindwe kutoka kujitafutia basi mshukuru Mungu kila iitwapo leo maana huo ni utajiri tosha.
 
Tunapaswa kumwona daktari tunapokuwa wagonjwa.

Mawazo ya kujiua yanaweza kuwa dalili ya ugonjwa wa akili au wa kihisia. Kama tu magonjwa mengine, hupaswi kuaibika. Ugonjwa wa akili au wa kihisia unaweza kutibiwa.

Jaribu kufanya hivi: Tafuta msaada wa daktari anayefaa haraka iwezekanavyo.

C&P from Jw.org/sw
 
Back
Top Bottom