Nahoji kwanini gharama za hoteli ambazo mabasi ya mikoni huingia ni kubwa sana?

Kama unaingia hotelini kununua biskuti ina maana hukupanga safari yako. Kama ungekuwa umepanga safari yako ungenunua biskuti toka kule ulikotoka.

Hata hivyo naona TRA hawataki kukusanya kodi kwenye hizi hotel na mfano ni hotel za Korogwe mauzo ni makubwa sana lakini wanatumia coupon yaani risiti za mkono badala ya EFD Receipt; TRA fanyeni kazi yenu kuna VAT ya kutosha kwenye hizo TRANSIT HOTEL
hiyo Rockhill kwa cku wana piga mil.sio chini ya 3
 
Nikuhusu hatua ya mabasi yaendayo mikoani kuwaibia na kuwatesa abiria.

Madereva wa mabasi yaendayo mikoani BUNDA, ISAMILO, ZUBERI na mengineyo nengi kuwapeleka abiria sehemu ya chakula ambayo ni Miradi ya wakubwa na kuuziwa chakula na vinywaji bei kubwa kuliko kawaida.

Ktk eneo maarufu hapa mkoani singida ambapo mabasi mengi huwapeleka abiria kupata huduma ya chakula mambo yako hivi
- Wali maharage, 3,000,
- wali nyama ng‘ombe 5,000
- chips mayai 4,000,
- Azam milk litre moja 4,500
- soda za pepsi na cocacola take away 1500
- biscuit ndogo za sh 200 zinauzwa 500

Pamoja na bidhaa nyingi ambazo sikuzitaja kuuzwa bei iubwa kulko kawaida. Mbaya zaidi hawatoi receipt/risiti hata kwa dawa.

pia kwa wale wanaotumia bara bara ya ARUSHA-DSM kuna Hotel huwa mabasi yanaingia kama CARTAGE,MOMBO,LIVERPOOL ,na huko kote bei ni Ghali sana kwa waendao mikoa ya LINDI,MTWARA kuna sehemu inaitwa NANGURUKURU huko napo hali ni mbaya vitu Ghali balaa.

Swali langu kwa serikali, kwamba haya hamyajui au mmejitia upofu ili raia wasokua na hatia waendelee kuteseka kwa maslahi ya watu binafsi.

Hivi TRA haya mnayajua, na kama mnayajua mmechukua hatugani ili kunisuru maisha ya mafukara na masikini wanaosafiri kwa shida mbali mbali.

Mnadhan mnajengenga dhana gan kwa sisi wanyonge tulowapa mamlaka yakusimamia na kuingoza taifa letu?

Utafiti mdogo niloufanya zaidi ya robo tatu ya abiria wote niliosafiri nao wameishia kunua biscuit ya miatano na azam juisi ya mia saba masikini ya mungu ukiwatazama nyuso zao kila mmoja wao anaonesha huzun mkubwa.

Niiombe serikali yangu kulitazama suala hili kwa jicho la tatu maana ni unyanyasaji na unyonyaji na kuzidi kutengeneza chuki isiyo sha kati ya wenye nacho na wasakatonge!.
Zamani tulisafiri na chupa ya chai na mihogo iliyopikwa nyumbani aidha tulifungashiwa viporo.Jifunze zamani tuliishi VP.
 
na hii ni hatari zaidi kwa tunaosafiri mara kwa mara. ukiwa waenda mwanza magari huwa yanasimama gairo au dodoma kuna hoteli humo barabarani chai ya rangi ya shilingi 200 wao wanauza 500, andazi au chapati 1000, ukigusa sahani ya chakula lazima udondoshe 5000 au 7000. nilipoona hali hii kwenye hoteli zote hizo niliamua.
kula machungwa tu ninaposafiri kwenda mikoani hata nikila kumi natumia 2000 tu.
kiukweli hili serikali waliangalie kuna wizi wa hadharani kabisa huko barabarani tunaposafiri.
 
Dah ni kweli kabisa vyakula bei Kubwa sana inatupa shida kwa watu tunaopenda kula, natumia gharama ya wali na kuku wa kienyeji helfu 10 hapo Moro, Lakin Moro wamezidi bei Kubwa mno
 
Sumatra ni majipu nadhani wana Mgao maana tena yale magari yanayojidai 1st class ndiyo yanatabia ya kuwapitisha watu maeneo wasiyoyataka.

Mtu umeisha gongwa kwenye nauli bado wanatufanyiahujuma kwa tuuza kwa wenye mahotel.
 
Wakuu wa TRA ktk sehemu husika za Hoteli hizo lazima wanachukua cha juu kwani hakuna sababu ya msingi ya Hoteli hizo kutotumia mashine za EFD, TAKUKURU na hili mpaka magufuli akuonyesheni kuwa ni jipu lililoiva?
 
Hlo ni jipu lililoiva kuna hotel za aljazera na starcom/comfot barabara ya morogoro iringa bei ipo juu kwenye vyakula had vinywaj na chakula king kinapashwa means ni kipolo risit ndo usitegemee
 
Mkuu upo sahihi mkumbwa junior na hilo ni kwa sababu ambazo Dereva na Konda wa mabasi mengi wanaelewa pasipo kuwa na bei hiyo wao hawatapata commission ya siku au mwisho wa mwezi.

Ukiangalia kwa mbaaali utaona baadhi ya hotel kama njia ya Dar - Arusha, Dar - Mwanza zimefungwa ukiuliza kirafiki kwa hao driver na Konda watakwambia nini sababu.

USHAURI:
Mimi huwa natumia njia hii hapa;
Mara nyingi nafaham siku flani nasafiri, hivyo siku moja kabla naenda kununua Digestive Biscuits au mkate flani wa Real Wheat Brown Bread, korosho, chupa yangu ya soda + maji.

Nikiwa ndani ya basi nashangaa wengine mnavokurukupa na chips mayai.
 
wale madereva wanaopeleka basi pale hulipwa kila mwisho wa mwezi kuanzia laki na nusu na kuendelea na kula bure kila anapopita pale yeye na Tingo wake..
 
Hii ni biashara, Kati ya dereva na mwenye hotel mbali ya kula bure ana posho pia bila kujali uwezo na hali ya abiria cha msingi ni maadalizi mbona wanaosafiri na treni wanaweza, fanya maandalizi ya mahitaji yako ya njiani hasa kama unasafiri na watoto, vyalkula vingi ni viporo jamani hivi mabasi yote yakishapita nani ataingia kula kwa bei hiyo? Wanalaza kesho wanaamsha tena hapo lazima tumbo lijibu. Tuache uvivu, ubungo terminal maji bei 700 - 1,500 chukua kabisa. Maandalizi ni tatizo kwetu
 
Ni kweli kabisa si haki kama mtoa hoja anavyodai. Nimejaribu kuchunguza kwa kuongea na baadhi ya makondakta. Nilichogundua ni kwamba mbali ya wafanyakazi wa hayo mabasi kula bure dereva pia huwa anapewa fedha. Ndiyo maana wanabadilisha hoteli kulingana na kiwango anacholipwa dereva na hoteli husika. Hii njia ya Mbeya Dar kuna hotel zinaitwa Kitonga na El Tazeera, huduma mbovu ila gharama ni balaa.
 
MAGUFULI INGIA KWENYE HIZI HOTELI. SIDHANI KAMA ZINALIPA KODI STAHIKI.

DEREVA HUWA ANAPEWA 20 TO 25 NA SAHANI TANO ZA CHAKULA. AMBAZO ANAGAWA KWA KONDA , UTINGO NA RAFIKI.

NI JIPU KUBWA SANA HILI.
 
Back
Top Bottom