Nahitaji wajuzi kidogo kuhusu elimu ya majini na utajiri

Strong25

Senior Member
Dec 6, 2021
169
357
Swali hivi nikweli mizimu ama majini yanaweza kumtajirisha mtu..? kama ni kweli ni yapi madhara yake na faida kama sio je hawa tunaoambiwa wana pesa za majini wanazipata wapi..? (NOTE..nahitaji pia hizo mambo)
 
Utajiri unakuja kwa kujituma,kujilipuaa
Sasa we unataka ulale tu alafu umwambie jini akuangushie mijihela

Ova

sio kwamba jini ndo likuletee pesa bila kufanya kazi__baskia yapo ambayo yanakusaidia katika utafutaji wako
 
Mizimu au majini yanaweza kumtajirisha mtu Jibu ni ndio ila kwa makubaliano maalum. Endapo utafanya kama walivyotaka basi mafanikio kwako yatakua kama mvua ila ukienda kinyume utakua mtu wa majuto na kusaga meno.
Ila kuhusu mizimu inabidi uende kwenye mizimu inayo shaabiana au uhusiana na ukoo wenu.
Mfano wewe ni mtu wa Handeni ukienda lushoto inafaa maana ni mkoa mmoja na pia mababu zenu labda huko zamani walikua wanaingiliana kwenye mambo ya mila.
Ni mambo ambayo yapo na yanafanya kazi vizuri tu ila vijana wa mjini wanasema hawataki mambo ya zamani.
 
Back
Top Bottom