Nahitaji mwanamke wa kuzaa naye. Nina mke lakini kwa bahati mbaya kwa majaaliwa ya Maanani hakujaaliwa kupata kizazi na baada ya kuhangaika kwa muda mrefu nchini na nje madaktari wametuambia kuwa si rahisi kuweza kuzaa kulingana na tatizo alilonalo. Baada ya kulitambua hilo, na kwayeye kuthamini juhudi zangu za kumshughulikie yeye kwa ghrama zote kote duniani na kushindikana hatimaye tumekubaliana kuwa nitafute mwanamke nizae naye. Si hitaji kuoa kwakuwa siwezi kuwa na wanawake wawili na siwezi kumwacha niliyenaye kwakuwa hastahili kuachwa. Niko tayari kumtunza mwanamke atakayekubali hilo kwa 100% kwa kila kitu chake na kizazi chake atakapojaaliwa kwakuwa uwezo upo, nia ipo na sababu ipo. Ningependa kuadopt pia lakini kama binadamu ningependa nione damu yangu pia kila mtu analifahamu hili. Ni maamuzimagumu kufanya lakini tumefanya pamoja. Aliyetayari juu ya hili twaweza wasiliana. Niko makini juu ya hili.
umeongea pointi sana dearest kwa kusali kwa imani inawezekana kabisa kizazi kikaachia na mkeo akapata mtoto ila unatakiwa uwe unaomba halafu hata usisubiri we endelea tu na maisha siku itakayotiki hata hutoamini macho yako. ila unapoanza kumwambia awashrikishe kina rev masanilo naona unaleta utani sasa